Mheshimiwa Rais, Tutembelee nasi Kanda ya Kaskazini

chuwaalbert

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
3,598
2,117
Sasa ni karibu mwaka mmoja na nusu tangu Mheshimiwa Rais uingie Ofisini. Tunapenda ututembelee nasi wa Mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Tumeona unafanya hivyo sehemu nyingine za nchi.

Tena unatumia barabara, unachokifanya ni kizuri kwa sababu unajionea mwenyewe hali halisi ya maisha ya wananchi. Unasimama, unawahutubia, unasikia shida zao na unatafuta majibu ya shida hizo hapo kwa hapo.

Tuna hamu ya kukuona Handeni, Kilindi, Simanjiro, Kiteto, Babati, Mbulu, Ngorongoro, Karatu, Monduli, Longodo, Arumeru, Hai, Siha, Rombo, Moshi, Mwanga, Same, Korogwe, Muheza, Tanga, Pangani na Lushoto. Kwa kwei tina ham ya kukuona mkuu.
 
Duh binafsi sizani kama hiyo hamu ya kumuona huku ni kubwa kiasi hicho. Hasa kwa Kilimanjaro. Nadhani bora aje waziri mkuu ni afadhali zaidi. Ki ukweli kwa Kilimanjaro nachelea kusema kwamba hamu ya kumuona kama ni kubwa....Vinginevyo akija basi ni vema akawa makini sana na maneno atakayoyatumia ktk hotuba zake
 
Back
Top Bottom