Mheshimiwa Rais sidhani kama kupenda Kwako kila mara ' Kumtajataja ' hadharani TISS DG Dkt. Kipilimba ni sawa Kiuweledi

Mwandiko ni tatizo,kwanini unafanya maandishi yako kuwa madogo?Kiukweli huwa napata tabu kusoma mabandiko yako kutokana na size ya maandishi!

Pole na sifikirii kubadili kwani nadhani kama yangekuwa na shida nisingepata ' Wafuasi ' wengi wa ' Mabandiko ' yangu hapa Jamvini. Nenda CCBRT kawaambie warekebishe macho yako ili uwe unamsoma vyema GENTAMYCINE wa Mtandaoni JamiiForums vinginevyo utakuwa unakosa ' Uhondo ' wangu ambao kila siku upo na ninao hapa.
 
Basi kwaheri
 
Basi kwaheri

Mwandiko wangu ungekuwa unakusumbua ungekuwa na uwezo wa Kusoma ' posts ' zangu na Kuzijibu hivi? Nikisema kuwa kama kuna Watu ambao wanaongoza kwa ' Unafiki ' duniani ni Watanzania msiwe mnanibishia kwani sijakosea na nipo sahihi kwa 100% zote.
 
ANGALIZO

Naomba kama unajijua kabisa kuwa uwezo wako wa kuona vitu vya umbali / unyeti / umuhimu wake basi katika huu ' Uzi ' kaa nao mbali kabisa na waachie wenye ' akili ' zao na ' Wachambuzi ' wa masuala haya ya Kijasusi ambao wapo ( tunao ) wengi humu na Sisi Mangumbaru na Mapopoma wengine tuwe watazamaji tu kuliko Kuchangia halafu ukajikuta umevapa / umekosea.

HOJA KUU

Nashukuru sana Mwenyezi Mungu kwamba karibia awamu zote za nchi hii nilikuwepo japo ya Hayati Baba wa Taifa ilinikutia nikiwa bado katika Ndoo ya Kuogea na nalilia Uji wa Buruga ( namaanisha nikiwa bado Kichanga kabisa ) ila kwa awamu ya Mzee Mwinyi niliishuhudia bila kusahau ya Mzee Mkapa na ya Mzee Kikwete na sasa nipo hii ya Mheshimiwa Dkt. Magufuli natiririka na naserereka nayo.

Katika Awamu zote hizo sikuwahi hata Siku moja kuwasikia hao Watangulizi wake Rais Dkt. Magufuli wakiwa na tabia ya kupenda ' Kumtajataja ' au hata kupenda kuonyesha kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Idara Nyeti nchini ya Usalama wa Taifa ( TISS ) yupo eneo ambalo Wao wapo ila ilikuwa ni mpaka tu labda Mtu akutonye / akuambie.

Nimejuiuliza maswali mengi sana kwani Marais wote Wastaafu walikuwa hawapendi kuwatajataja Wakuregenzi wao Usalama wa Taifa ( TISS DG ) lakini kwa Awamu hii ya Gwala / Tano Rais Dkt. Magufuli anapenda mno ' Kumtaja ' na hata kupenda ' Kumuinua ' Kitini Mkurugenzi wa sasa Dkt. Modestus Kipilimba na bado sijapata jawabu / jibu ila najua kupitia ' Majiniasi ' waliotukuka wa Jamvi hili la JamiiForums leo nitayapata.

Sikuishia tu hapo kama kawaida yangu huwa napenda kwenda ' deep ' zaidi kufanya ' references ' na Mataifa mengine mbalimbali kuanzia na haya Jirani ( tunaofanana kwa Vingi ) kisha hupenda pia kuangalia na yale Mataifa makubwa ambayo yana uwezo mkubwa wa Kuanzia Uchumi, Kijeshi na Kiusalama kuliko Tanzania yetu hii na sijaona mahala ambapo Marais wao huwa wanawataja hovyo tena hadharani Wakurugenzi Wakuu wa Idara zao ' Nyeti ' za Usalama wa Taifa ila kwa Tanzania naona hii tabia inaanza Kuzoeleka.

Kwa maoni au mtazamo wangu mdogo tu ( mnaojua zaidi mtanisaidia ) kwa asili ya hizi nchi zetu tena ambazo zina ' Majaribu ' na ' Matatizo ' mengi ya Kimsingi huku kukiwa na ' Maadui ' wengi wa ndani na nje sidhani na siafiki kabisa tena kwa 100% kwa Wakurugenzi wetu hawa wa hii Idara / Taasisi muhimu kama si nyeti ya Usalama wa Taifa ( TISS ) kutajwatajwa hovyo kwa Watu na hata kujulikana kwakuwa Tanzania ya sasa imejaa Watu wa ajabu ajabu wenye ' maslahi ' yao ' hasi ' na nchi hii hivyo kuna uwezekano na Wao wakaanza Kumjua na Kumzoea kisha hali ikaja kuwa mbaya zaidi huko mbeleni.

Na sidhani pia kama hata ' Kiuweledi ' hivi anavyofanya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. Magufuli la kupenda ' Kumtajataja ' Mkurugenzi Mkuu wa Idara / Taasisi ya Usalama wa Taifa ( TISS DG ) Dkt. Kipilimba ni sahihi na kama itapendeza nadhani Watu wa ' Itifaki ' ambao nina uhakika kuwa wengi wenu tunatiririka na kuserereka pamoja 24/7 hapa JamiiForums hili mtaliangalia kwa hayo mapana yake ili utaratibu ule ule uliozoeleka wa zamani wa hawa Wakurugenzi kutojulikana sana au kutajwatajwa hovyo uendelee kwani Kwangu Mimi kwa ' Mazingira ' ya nchi yetu ulikuwa ni utaratibu murua / mujarab / sahihi kabisa kuliko huu wa sasa aliouanzisha Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. Magufuli.

Huu ulikuwa ni mtizamo wangu Mimi kama GENTAMYCINE ila nitashukuru na Watu wengine nao wakija hapa wakichangia huku wale ambao ' watanikosoa ' basi wanikosoe ha ' Hoja ' nzito nzito kwani hata Mimi nataka Kujifunza jambo hapa kutokana na kwamba yawezekana huu utaratibu wa sasa ukawa ndiyo sahihi kuliko ule ambalo nimeukariri / nimeuzoea. Nia na madhamuni tupate afya ya Kimjadala na ya Kimantiki juu ya hili ' Suala ' kusudi mwisho wa Siku wote tupate ' maarifa ' na ' ufahamu ' zaidi.

Karibuni!

Nawasilisha.
Uoga ulio pitiliza ndio sababu inayo mfanya atajetaje majina ya watu na vyeo vyao.
 
Kajipange upya ' Mpuuzi ' mkubwa Wewe!
Inonyesha kabisa kuwa huna busara kabisa kichwani mwako kama mtu mzima kutwa kwenye mitandao ni kutukana watu basi ni moja ya dalili kuwa umepitia maisha magumu sana utotoni mwako huku ukijifanya umeishi ikulu ya Entebe.Picha kamili iko kwenye maandiko yako na kujifanya unajua sana.Na hiyo ndiyo picha yako kamili kuhusu wewe unayejiita jina la dawa inayotibu magonjwa ya mfumo wa mkojo kundi la aminoglycosides.......developmental pyschology yako inatupa picha kamili jinsi ilivyozaliwa mpaka hapo ulipo.Pole sana na yote uliyopitia na ndiyo imekufanya jinsi ulivyo Mungu akusadie sana.
 
Mwandiko wangu ungekuwa unakusumbua ungekuwa na uwezo wa Kusoma ' posts ' zangu na Kuzijibu hivi? Nikisema kuwa kama kuna Watu ambao wanaongoza kwa ' Unafiki ' duniani ni Watanzania msiwe mnanibishia kwani sijakosea na nipo sahihi kwa 100% zote.
Mkuu si uweke normal tu kama waandishi wengi tu humu!Mimi binafsi nimesoma bandiko hili kwa tabu!
Lilikuwa ombi tu!
Baada ya ombi ukaniambia niende nikatibiwe macho,ndio maana nikaona isiwe tabu ngoja nikae kando tu!
 
Anachokifanya Rais ni ulimbukeni na ni hofu ya mtu asiyejiamini.
Hawa watu wanafanya mambo mengi mazuri kwa manufaa ya nchi yao na raia wote...na kama ilivyo kawaida ya binadamu huwa tunakosea na wao kadhalika.
Rais Magufuli ni raia wa kawaida na hakupikwa au hakupitia kikaangoni kumuandaa kuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yetu ndio maana tunashuhudia mambo mengine ya kulitia taifa aibu kama haya.
Watu wa Itifaki inabidi wamshauri kuhusiana na tabia,mwenendo na hulika ya kuwa Mkuu wa Nchi.

Mipasho,ubabe,udaku na mengine ya aina hii sio sifa ya kiongozi wa nchi.
 
Inonyesha kabisa kuwa huna busara kabisa kichwani mwako kama mtu mzima kutwa kwenye mitandao ni kutukana watu basi ni moja ya dalili kuwa umepitia maisha magumu sana utotoni mwako huku ukijifanya umeishi ikulu ya Entebe.Picha kamili iko kwenye maandiko yako na kujifanya unajua sana.Na hiyo ndiyo picha yako kamili kuhusu wewe unayejiita jina la dawa inayotibu magonjwa ya mfumo wa mkojo kundi la aminoglycosides.......developmental pyschology yako inatupa picha kamili jinsi ilivyozaliwa mpaka hapo ulipo.Pole sana na yote uliyopitia na ndiyo imekufanya jinsi ulivyo Mungu akusadie sana.

Masahihisho sijaishi IKULU ya ENTEBBE bali nimeishi IKULU ya NAKASERO na sijaishi tu huko bali hata ' Udogoni ' mwangu pia niliwahi kuwepo mara kwa mara IKULU yako ya Magogoni kama sehemu ya Wanafamilia wa Kiukoo na ' Muasisi ' mwenyewe Mwalimu Nyerere. Bado unataka nikupe na mengineyo au niishie tu hapa? Halafu na kwa kukuonyesha kuwa pamoja na kuwepo kote huko ila sijabadilika na maisha yangu yameendelea kuwa yale yale ya kuishi ' Simple Life ' huku na Mimi pia nikipambana kutafuta maisha yangu na nisiishi kwa migongo ya hao niliopitia mikononi mwao akina Museveni na Hayati Nyerere. Na hata hivi karibuni tu kutokana na Historia pia ya Kirafiki ya muda mrefu hasa Kipindi alichokuwa hapa Tanzania napanga pia kwenda Kumtembelea Rais wa Rwanda Kagame. Nakumbuka Kauli ya Hayati Baba wa Taifa alikuwa akipenda kutuambia kuwa kama kuna Watu ambao tunatakiwa kuwapenda basi ni hawa Majirani zetu hasa wa Kijiografia kwani Sisi sote ni Ndugu moja sema tu ni ' Hila ' za Wazungu ( Wakoloni ) ndizo zimetutenganisha kama pia siyo Kutugawa hivi. Naomba niishie hapa tafadhali na nikuache na ' Upumbavu / Upopoma ' wako huo ambao unakusumbua.

Kazi Kwako!
 
Mimi kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa ni public figure ndio maana katika shughuli mbalimbali za kitaifa huwa anaambatana/hukaa pamoja na wakuu wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama. Mkurugenzi wa Idara huteuliwa na uteuzi huo huwa sio siri, ukimgoogle jina lake unapata taarifa mbalimbali kuhusu yeye personally na Idara anayoiongoza. Kwa kusema hayo nadhani hakuna shida yeye kutajwa kwasababu anafahamika. Labda kama protocol hairuhusu (which i cant argue)
 
Masahihisho sijaishi IKULU ya ENTEBBE bali nimeishi IKULU ya NAKASERO na sijaishi tu huko bali hata ' Udogoni ' mwangu pia niliwahi kuwepo mara kwa mara IKULU yako ya Magogoni kama sehemu ya Wanafamilia wa Kiukoo na ' Muasisi ' mwenyewe Mwalimu Nyerere. Bado unataka nikupe na mengineyo au niishie tu hapa? Halafu na kwa kukuonyesha kuwa pamoja na kuwepo kote huko ila sijabadilika na maisha yangu yameendelea kuwa yale yale ya kuishi ' Simple Life ' huku na Mimi pia nikipambana kutafuta maisha yangu na nisiishi kwa migongo ya hao niliopitia mikononi mwao akina Museveni na Hayati Nyerere. Na hata hivi karibuni tu kutokana na Historia pia ya Kirafiki ya muda mrefu hasa Kipindi alichokuwa hapa Tanzania napanga pia kwenda Kumtembelea Rais wa Rwanda Kagame. Nakumbuka Kauli ya Hayati Baba wa Taifa alikuwa akipenda kutuambia kuwa kama kuna Watu ambao tunatakiwa kuwapenda basi ni hawa Majirani zetu hasa wa Kijiografia kwani Sisi sote ni Ndugu moja sema tu ni ' Hila ' za Wazungu ( Wakoloni ) ndizo zimetutenganisha kama pia siyo Kutugawa hivi. Naomba niishie hapa tafadhali na nikuache na ' Upumbavu / Upopoma ' wako huo ambao unakusumbua.

Kazi Kwako!
Pamoja na maelezo yako hayo bado unatatizo la kimaisha huko ulikopitia umepata ukatili sana kama Mange Kimambi alivyo sasa na wewe hakuna tofauti.Maandishi yako toka siku ya kwanza ndani ya JF yanadhihirisha hayo.Na kwa taarifa yako familia ya mwl naijua vizuri sana na watoto wake wengi wamepata tocha sana kisaikolojia na ndiyo maana unamuona Pilot Andrea anaishi yale,Makongoro kama unavyomuona vile na wengine wengi tu kwasababu Mwl aliwaambia viongozi wa watoto wake toka shule kuwa watoto wake wasipate special attention kisa tu ni watoto wa rais.na ndipo viongozi wengi walikuwa wanaogopa hata kuwapa nafasi watoto wa mwl kisa wanaogopa wataulizwa na baba yao na wengi wameacha hata kazi zao kisa vyeo havipandi mishahara haipandi huku wakiona wenzao wa level moja au darasa moja wakipanda nafasi za juu.Na wewe ni wale wale tu mlioumizwa kisaikolojia sasa umebaki kupunguza hasira zako kwa kuwatukana na kuwabeza watu wengine na hiyo tunaita Ego Defense.(placing unacceptable impulses in yourself onto someone else )
 
Kuna Mtu yoyote yule labda amekuuliza kama unaijua Familia ya Mwalimu Nyerere au hapana? Pumbavu.
 
ANGALIZO

Naomba kama unajijua kabisa kuwa uwezo wako wa kuona vitu vya umbali / unyeti / umuhimu wake basi katika huu ' Uzi ' kaa nao mbali kabisa na waachie wenye ' akili ' zao na ' Wachambuzi ' wa masuala haya ya Kijasusi ambao wapo ( tunao ) wengi humu na Sisi Mangumbaru na Mapopoma wengine tuwe watazamaji tu kuliko Kuchangia halafu ukajikuta umevapa / umekosea.

HOJA KUU

Nashukuru sana Mwenyezi Mungu kwamba karibia awamu zote za nchi hii nilikuwepo japo ya Hayati Baba wa Taifa ilinikutia nikiwa bado katika Ndoo ya Kuogea na nalilia Uji wa Buruga ( namaanisha nikiwa bado Kichanga kabisa ) ila kwa awamu ya Mzee Mwinyi niliishuhudia bila kusahau ya Mzee Mkapa na ya Mzee Kikwete na sasa nipo hii ya Mheshimiwa Dkt. Magufuli natiririka na naserereka nayo.

Katika Awamu zote hizo sikuwahi hata Siku moja kuwasikia hao Watangulizi wake Rais Dkt. Magufuli wakiwa na tabia ya kupenda ' Kumtajataja ' au hata kupenda kuonyesha kwamba Mkurugenzi Mkuu wa Idara Nyeti nchini ya Usalama wa Taifa ( TISS ) yupo eneo ambalo Wao wapo ila ilikuwa ni mpaka tu labda Mtu akutonye / akuambie.

Nimejuiuliza maswali mengi sana kwani Marais wote Wastaafu walikuwa hawapendi kuwatajataja Wakuregenzi wao Usalama wa Taifa ( TISS DG ) lakini kwa Awamu hii ya Gwala / Tano Rais Dkt. Magufuli anapenda mno ' Kumtaja ' na hata kupenda ' Kumuinua ' Kitini Mkurugenzi wa sasa Dkt. Modestus Kipilimba na bado sijapata jawabu / jibu ila najua kupitia ' Majiniasi ' waliotukuka wa Jamvi hili la JamiiForums leo nitayapata.

Sikuishia tu hapo kama kawaida yangu huwa napenda kwenda ' deep ' zaidi kufanya ' references ' na Mataifa mengine mbalimbali kuanzia na haya Jirani ( tunaofanana kwa Vingi ) kisha hupenda pia kuangalia na yale Mataifa makubwa ambayo yana uwezo mkubwa wa Kuanzia Uchumi, Kijeshi na Kiusalama kuliko Tanzania yetu hii na sijaona mahala ambapo Marais wao huwa wanawataja hovyo tena hadharani Wakurugenzi Wakuu wa Idara zao ' Nyeti ' za Usalama wa Taifa ila kwa Tanzania naona hii tabia inaanza Kuzoeleka.

Kwa maoni au mtazamo wangu mdogo tu ( mnaojua zaidi mtanisaidia ) kwa asili ya hizi nchi zetu tena ambazo zina ' Majaribu ' na ' Matatizo ' mengi ya Kimsingi huku kukiwa na ' Maadui ' wengi wa ndani na nje sidhani na siafiki kabisa tena kwa 100% kwa Wakurugenzi wetu hawa wa hii Idara / Taasisi muhimu kama si nyeti ya Usalama wa Taifa ( TISS ) kutajwatajwa hovyo kwa Watu na hata kujulikana kwakuwa Tanzania ya sasa imejaa Watu wa ajabu ajabu wenye ' maslahi ' yao ' hasi ' na nchi hii hivyo kuna uwezekano na Wao wakaanza Kumjua na Kumzoea kisha hali ikaja kuwa mbaya zaidi huko mbeleni.

Na sidhani pia kama hata ' Kiuweledi ' hivi anavyofanya Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano Dkt. Magufuli la kupenda ' Kumtajataja ' Mkurugenzi Mkuu wa Idara / Taasisi ya Usalama wa Taifa ( TISS DG ) Dkt. Kipilimba ni sahihi na kama itapendeza nadhani Watu wa ' Itifaki ' ambao nina uhakika kuwa wengi wenu tunatiririka na kuserereka pamoja 24/7 hapa JamiiForums hili mtaliangalia kwa hayo mapana yake ili utaratibu ule ule uliozoeleka wa zamani wa hawa Wakurugenzi kutojulikana sana au kutajwatajwa hovyo uendelee kwani Kwangu Mimi kwa ' Mazingira ' ya nchi yetu ulikuwa ni utaratibu murua / mujarab / sahihi kabisa kuliko huu wa sasa aliouanzisha Amiri Jeshi Mkuu na Rais Dkt. Magufuli.

Huu ulikuwa ni mtizamo wangu Mimi kama GENTAMYCINE ila nitashukuru na Watu wengine nao wakija hapa wakichangia huku wale ambao ' watanikosoa ' basi wanikosoe ha ' Hoja ' nzito nzito kwani hata Mimi nataka Kujifunza jambo hapa kutokana na kwamba yawezekana huu utaratibu wa sasa ukawa ndiyo sahihi kuliko ule ambalo nimeukariri / nimeuzoea. Nia na madhamuni tupate afya ya Kimjadala na ya Kimantiki juu ya hili ' Suala ' kusudi mwisho wa Siku wote tupate ' maarifa ' na ' ufahamu ' zaidi.

Karibuni!

Nawasilisha.
Anatajwa MUNGU sembuse Kipilimba? Tatizo mnahamisha posts za magoli (). Kwamba badala ya kujiuliza maswali ya msingi kama yafuatayo, tujadili ATAJWE au ASITAJWE?

1. Kwanini kuna uvujaji mkubwa wa taarifa za kiusalama kwenda kwenye Idara za Usalama wa Taifa za takriban nchi zote zinazotuzinguka? Nimebuni neno "mtungo wa kijasusi" kwa jinsi kila Idara ya Usalama wa Taifa ya nchi jirani inavyoweza kunasa taarifa za Idara yetu kirahisi tu.

2. Kwanini takriban 80% ya workforce ya Idara yetu ya Usalama wa Taifa inaundwa na watu waliookotwa mtaani hivi karibuni, hawakwenda Malindi kufanya JBC, na wapo wapo tu kitengoni hawajui A wala B?

3. Kwanini tatizo la taarifa za uongo limetokea kuwa kubwa na linazidi kukua kiasi cha Sponsor kutegemea taarifa kutoka vyanzo visivyo vya kiusalama?

4. Katika historia ya TISS, haijawahi kutokea wakurugenzi wawili kwa mkupuo kuwa demoted, lakini hilo limetokea kwa ex-DDGIS na ex-DEO?

Maswali ni mengi lakini haya yanatosha kwa muda huu. Ndugu zangu Watanzania, ninyi ndio waajiri wa kila Afisa wa Idara ya Usalama wa Taifa. Ninyi ndio mnawalipa mishahara na OPs. Wanawajibika kwenu. Na msipowasimamia, mkawaacha waendelee na ubabaishaji mkubwa uliopo, mtakaoumia na kujilaumu ni nyie.

Nasubiri waje kutukana hapa, maana uwezo wa kintelijensia walionao umeishia kwenye kuweka matusi mitandaoni.
 
Pengine hoja yako iwe funzo kwa wateule wake,rais anahaki ya kumtaja huyo bwana sehemu yyte ila nje ya huyo ambaye kamteua yeye hana nafasi ya kumtaja mtumishi wa idara hiyo sehem nyingine yyte,pia nawashauri waliopo chini yake hawawez mtaja mtumishi wa idara hiyo kweny sehemu yyte ya hadhara na huyo mtu utajwa na rais pekee waliobakia hawaruhusiwi i mean waziri mkuu hawez mtaja,popote wala makamu hawez mtaja au mtambulisha popote! Ila awapo mkuu wa nchi huyo bwana anaweza tajwa, ila kwa kiongozi anae jua jukum la kazi la idara hii huwa sio vizuri kumtaja kwani pamoja na uwepo wake popote awapo rais yy huwa yupo kazini kwa kushirikiana na wale walinzi walio toka idara yake!
 
Awamu za nyuma za Analogy mambo haya yalikuwa magumu leo ni digital amtaje asimtaje watu watajua tu tangu akiwa Nida lkn pia huyo ni DG tiss si mtu anayehitajika kuwa covered ila siku akiwapanga watumishiwa tiss na kuwaarika kwa chakula ikulu kama alivyofanya na trafiki hapo ndio itakuwa issue mbaya maana wanatakiwa kuwa covered ili wafanye kazi japo wengine kama wale special group linalovaa suti mbele ya kamera. Lakini wauza magazeti na mchicha ;bodaboda manesi engineers nk walio kitengo hao hatakaa awataje si tu kuwataja wengine hatakaa awajue lkn huyo DG aweza hata kuhamia hata Sumatra asilete madhara hata kuwa opposition leader sema akikiuka masharti tu anaingia saverhouse

DUUH
 
Back
Top Bottom