Mheshimiwa Rais, Serikali imeshindwa kuiwezesha MSD, msiwarushie mipira Wafawidhi

Mpingamkoloni

Member
Feb 14, 2021
13
32
Mimi si mtumishi wa Afya, lakini mateso anayopata mtoto wa dada wa kunyonya (mtumishi wa afya), yamenifanya nitambue wapi serikali inakosa.

Ni jambo la ajabu sana kuona kuna uharamisho mkubwa wa kusema uwongo miongoni mwa viongozi wakuu wa Serikali hasa Afya. Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema jitahadharisheni, Mimi ninawaambieni dhambi Kuu kabisa katika Madhambi Makuu ni 1. Kumshirikisha Allah pamoja na mtu mwingine 2. Wazazi kukufanya Aaq 3. Na kusema uwongo

Hivi kama umeshindwa kutoa huduma fulani kwanini useme uongo na kutwisha mizigo watu?

Serikali inatambua kabisa kwamba vituo vya afya havina madawa na vifaa tiba kwa sababu ama MSD hajanunua dawa makusudi au hajawezeshwa kuwa na dawa. Ajabu hivi karibuni Waganga wafawidhi wameandikiwa barua zenye hoja lukuki ya kuwarushia lawama kwamba wao ndio chanzo cha dawa kutokuwapo kwenye hospitali za mikoa, wakati ukweli utabaki kuwa serikali haijaiwezesha MSD. Ukipitia hoja za wakaguzi wao utacheka, zimejaa vioja. Utatambua kuwa hoja hizo zilishapangwa mapema. Sijui nia ilikuwa kumridhisha Mhe. Ndugai?

Majuzi waganga wafawidhi wameandikwa kupoteza mabilioni ya shilingi. Wakahukumiwa na jamii bila kuwapo na ukweli kwa sababu hawana namna ya kutokubali kusingiziwa mambo.

Viongozi wa Wizara ya Afya, Mhe. Gwajima, Mhe. Mollel na Mhe. Makubi kupitia makundi mbalimbali hata ya kijamii wamesikika au wameonekana wakiandika (Telegram na WhatsApp, jumbe zao zipo, naweza zirusha hapa) wakiwasema vibaya viongozi wa chini wa Afya hususani Wafawidhi na hata wale wanaowazunguka Wizarani, wakiwalaumu kwa kila kitu, utadhani hakuna jema wanalofanya. Ukizungumzia Waganga Wafawidhi wanafanya mema mengi ingawa ingawa hawalipwi mshahara wowote kulingana na vyeo hivyo vinavyowasumbua.

Uongozi wa sasa wa Wizara ya Afya ni wa kulaumu kila siku, hawana nafasi ya kusikiliza kabla ya kutoa ushauri au kukaripia. Halafu kila siku wanataka watumishi wawe wa kuhifadhi taarifa, mara hifadhi hiki, mara hifadhi kile, mara hifadhi hiki, yaani sasa ni kuhifadhi tu, nadhani sasa watapaswa wapunguze kutibu ili muda mwingi watumie kuweka kumbukumbu za vidonge vilivyotumika na kumbukumbu zinazofanana na hayo. Hili hata Grace Maghembe amepata joto ya jiwe, lakini Allah hamtupi mja wake, leo kakimbia hizo lawama ambazo hazikuwa zamstahili.

Pamoja na mafanikio na changamoto zote za afya tutapiga kelele nyingi, na kupeana hongera za uongo kwamba serikali imepeleka pesa nyingi MSD na kwamba sasa wana dawa za kutosha, huku wote tunatambua huo sio uhalisia. Kwanini tudanganye? Kule MSD tumejaza net za mbu lakini hakuna dawa. Hata tumpeleke Malaika (sembuse mwanajeshi) hakuna kipya tutafanya. Tujitathmini.

Sasa mnawalaumu waganga wafawidhi mfano kwamba wamepoteza mapato kupitia fomu 2C za NHIF wakati tunajua kabisa hizi hospitali zikienda MSD hazipati hizi dawa ambazo na ndio maana zinaishia kujazwa kwenye form 2C. Hivyo ni kawaida kwa wagonjwa wa bima ya afya kwa sasa wakienda hospitali za umma wanaishia kupewa form 2C ili wakachukue dawa maduka ya nje, kwa sababu hata kama dawa hazipo MSD taratibu za manunuzi kwenda kwa watenda ziko wazi lakini taratibu, wanasiasa na wakaguzi wana mtazamo tofauti. Ukikutana na CAG anakuuliza kwa nini hujaenda kwa mtenda, ukikutana na waziri anakuuliza kwanini umenunua kwa mtenda, mwingine anasema mtenda anauza dawa kwa gharama kubwa, mwingine anasema kwanini hukwenda kununua dawa MSD bila kwenda kuangalia kama MSD alikuwa na dawa husika kwa kipindi hicho; yaani ni fujo tu kila mtu anataka ufanye atakalo. Lakini zile pesa za hizi hospitali mbona mkikusanya kwenye lile kapu la hospitali za mkoa hamuwarudishii? Watajiendeshaje?

Mnawatesa waganga wafawidhi kwa kuwasingia wanawaibia dawa. Utaibaje kitu ambacho hakipo?

Quran inasema ugonjwa wa kusema uwongo ndio ugonjwa mbaya kabisa na maovu yote yamefungwa katika chumba kimoja kwa kufuli, na uwongo ndio ufunguo wake. Mtu mwenye busara kamwe hawezi kusema uwongo hata kwa matamanio yake mwenyewe na pia Allah hamwongozi aliye mwongo.

Hii Wizara angalau Ummy aliiweza, hakuwa confrontational. Rais iangalie vizuri Wizara hii, isikatishe moyo watu.
 
Back
Top Bottom