Rais Samia, Ruhusu na saruji kutoka Kenya

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Leo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa tamko la kuruhusu Uagizaji wa Sukari kutoka Uganda, nampa pongezi sana.

Mheshimiwa Rais ujue pia Cement huku kanda ya ziwa imefika bei ya shilingi 24,000 kwa mfuko mmoja wakati jirani zetu Kenya wanauza 12,000 kwa mfuko mmoja. Tungependa kuona Serikali ikitupia jicho eneo hili ili watanzania wapate Cement kwa bei nafuu huku kanda ya ziwa.

Si vizuri kuamua kuwalinda wenye viwanda vya Cement kwa gharama ya watanzania maskini.

Serikali iruhusu Cement kutoka Kenya na iondoe masharti magumu ya uagizaji wa Cement
 
Leo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa tamko la kuruhusu Uagizaji wa Sukari kutoka Uganda nampa pongezi sana.
Mheshimiwa Rais ujue pia Cement huku kanda ya ziwa imefika bei ya shilingi 24,000 kwa mfuko mmoja wakati jirani zetu Kenya wanauza 12,000 kwa mfuko mmoja tungependa kuona serikali ikitupia jicho eneo hili ili watanzania wapate Cement kwa bei nafuu huku kanda ya ziwa. Si vizuri kuamua kuwalinda wenye viwanda vya Cement kwa gharama ya watanzania maskini.

Kasi ya ujenzi kwa sasa iko juu nchi nzima ,mafundi ujenzi na wakandarasi ni mashahidi kwa hiyo uhitaji ni mkubwa kuliko uzalishaji.

Kwa muktadha huo no busara serikali kuruhusu saruji kutoka nchi za jirani.
 
Wasifa ye tu uhuni wanaofanyaga. Waganda au wakenya wananunua sukari Brazil halafu wanakuja kutuuzia
 
Leo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa tamko la kuruhusu Uagizaji wa Sukari kutoka Uganda nampa pongezi sana.
Mheshimiwa Rais ujue pia Cement huku kanda ya ziwa imefika bei ya shilingi 24,000 kwa mfuko mmoja wakati jirani zetu Kenya wanauza 12,000 kwa mfuko mmoja tungependa kuona serikali ikitupia jicho eneo hili ili watanzania wapate Cement kwa bei nafuu huku kanda ya ziwa. Si vizuri kuamua kuwalinda wenye viwanda vya Cement kwa gharama ya watanzania maskini.
Serikali iruhusu Cement kutoka Kenya na iondoe masharti magumu ya uagizaji wa Cement
Wewe ni dalali au?
Kwani sababu ya simenti kupanda bei ni nini? Kuna upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini? Sukari inaeleweka, bidhaa hiyo haizalishwi kwa wingi hapa nchini.
Na siamini hata kidogo, kwamba mfuko wa simenti toka Kenya unauzwa Tsh 12,000/ huo ni uongo mtupu. Viwanda vya Kenya huagiza 'clinker' toka nje kwa bei rahisi au bila 'custom duty'. Unataka bidhaa hiyo iletwe hapa ishindane na bidhaa ya viwandani kwetu isiyokuwa na unafuu wowote? Si bora uwahimize hao serikali iwaruhusu viwanda vyetu na wao wapate ahueni ya uzalishaji?
 
Ili kuleta unafuu wa maisha kwa wananchi, serikali iruhusu bidhaa yoyote kutoka mahali popote. Lakini pia wakati ikifanya hivyo ipunguze kodi kwenye viwanda toka kodi 40 zilizopo sasa, zibakie angalao 5 tu.

Serikali ndiye muuaji mkubwa wa viwanda.
 
Wewe ni dalali au?
Kwani sababu ya simenti kupanda bei ni nini? Kuna upungufu wa bidhaa hiyo hapa nchini? Sukari inaeleweka, bidhaa hiyo haizalishwi kwa wingi hapa nchini.
Na siamini hata kidogo, kwamba mfuko wa simenti toka Kenya unauzwa Tsh 12,000/ huo ni uongo mtupu. Viwanda vya Kenya huagiza 'clinker' toka nje kwa bei rahisi au bila 'custom duty'. Unataka bidhaa hiyo iletwe hapa ishindane na bidhaa ya viwandani kwetu isiyokuwa na unafuu wowote? Si bora uwahimize hao serikali iwaruhusu viwanda vyetu na wao wapate ahueni ya uzalishaji?
Wewe ni kibarua kwenye kiwanda kipi. Hamwezi kila siku mkadai gharama za uzalishaji ni mkubwa na kupandisha bei ya Cement. Mpaka sasa uzalishaji wa Cement viwandani ni mdogo kutokana na mahitaji ya Cement kwa matumizi ya ndani. Usuchunge kibarua chako kwa gharama ya watanzania masikini wanaotaka kujenga nyumba kwa gharama nafuu. Viwanda Vingi vya Cement Kenya vinatumia nishati ya mkaa wa mawe kutoka Tanzania na bado bei zao ni nafuu wakati nyie mnatupiga bei
 
Wasifa ye tu uhuni wanaofanyaga. Waganda au wakenya wananunua sukari Brazil halafu wanakuja kutuuzia
Kuna shida gani? Wewe unachotaka si kupata sukari? Kama sukari inapatikana kwa bei nafuu toka Brazil, hata wafanyabiashara wa Tanzania waagize.

Cha muhimu, serikali iwapunguzie kodi wenye viwanda. Kodi zilizopo huko ni wizi mtupu. Kodi 40, halafu utegemee bidhaa iwe na bei rahisi au ishindane na bidhaa kutoka nje?
 
Mheshimiwa Rais ujue pia Cement huku kanda ya ziwa imefika bei ya shilingi 24,000 kwa mfuko mmoja wakati jirani zetu Kenya wanauza 12,000 kwa mfuko mmoja
Nafurahi kuona kwenye bandiko lako kumejaa maneno yenye hekima. Hakuna vitisho kwa rais amabaye ni kama Mungu kwa mujibu wa katiba yetu.

Akiamua anaweza kuwaua watu wa Kanda ya ziwa wote na asishitakiwe popote
 
Wewe ni kibarua kwenye kiwanda kipi. Hamwezi kila siku mkadai gharama za uzalishaji ni mkubwa na kupandisha bei ya Cement. Mpaka sasa uzalishaji wa Cement viwandani ni mdogo kutokana na mahitaji ya Cement kwa matumizi ya ndani. Usuchunge kibarua chako kwa gharama ya watanzania masikini wanaotaka kujenga nyumba kwa gharama nafuu. Viwanda Vingi vya Cement Kenya vinatumia nishati ya mkaa wa mawe kutoka Tanzania na bado bei zao ni. Juzi tu hapa wameparurana wao kwa wao, wenye viwanda vya simenti wakimgomea mwenzao anayezalisha 'clinker nafuu wakati nyie mnatupiga bei
Ukitaka tuzungumzie uzalishaji wa simenti Kenya nitakufundisha vizuri sana, kwa sababu ninauelewa vyema na wala hauna gharama nafuu yoyote kama unavyoeleza hapa wewe. Unafuu wao ni kuagiza 'clinker' Egypt kwa bei nafuu zaidi, halafu hailipiwi ushuru kwa vile ni soko la COMESA.
Juzi tu hapa wenye hivyo viwanda vya simenti wamemgomea mwenzao anayetaka awauzie 'clinker' ili waache kuagiza nje. Wewe hapa unakuja na mipasho tu usiyoielewa.
Ni bora zaidi mimi kuwa kibarua kwenye viwanda vyetu kuliko wewe mlanguzi/dalali unayetaka kupandika kwenye mgongo wa waTanzania kwa manufaa yako binafsi na hao wanaokutuma kutoka huko nje.
 
Nini maana ya kuwa na Clinker yenye kodi kubwa and then bei cement ipande juu kiasi hicho. Hata kama unajifanya mtaalamu kiasi hicho na kuniita mimi mlanguzi bado wewe unatetea hicho kibarua chako kwa gharama ya Mtanzania masikini. Sisi tunataka Cement kwa bei nafuu sio hizo blah blah zako.
 
Kuna shida gani? Wewe unachotaka si kupata sukari? Kama sukari inapatikana kwa bei nafuu toka Brazil, hata wafanyabiashara wa Tanzania waagize.

Cha muhimu, serikali iwapunguzie kodi wenye viwanda. Kodi zilizopo huko ni wizi mtupu. Kodi 40, halafu utegemee bidhaa iwe na bei rahisi au ishindane na bidhaa kutoka nje?
Inasikitisha sana kuwa na vilaza kama wewe
 
Back
Top Bottom