Mheshimiwa Rais naomba usinichoke: Kifo cha Waziri Dhahiri wilayani Mwanga kimenistua!

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,524
Mpendwa Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninakusalimu katika Jina la Bwana wetu Yesu Kristo; aliye Alfa na Omega; Mfalme wa Wafalme na Bwana wa Mabwana!

Ninamuomba sana Mungu kuwa usomapo ujumbe huu ushukiwe na neema itokayo kutoka kwa Mungu wetu aliye juu ambaye kwa neema na rehema zake alikuweka wewe kuwa Rais wa Nchi hii katika kipindi hiki.

Mheshimiwa Rais, jana niliona waraka ukisambazwa mitandaoni. Ulikuwa umeandikwa na Lembrus Mchome aliyesaini kama Katibu wa Chadema Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro.

Waraka ule unaeleza kuwa kijana mmoja aitwaye Waziri Dhahiri alikamatwa na Polisi asubuhi akiwa mzima na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Kata ya Lembeni, Mwanga lakini alifariki dunia jioni akiwa Kituoni hapo kutokana na kipigo!

Leo ninaona tena Jamii Forum wakisambaza taarifa hii:



Mheshimiwa Rais, tukio hili linazua maswali mengi na pia sio tu kuwa linasikitisha, bali linajenga hofu miongoni mwa jamii! Ieleweke kuwa kila mtu katika Nchi hii anaweza kutuhumiwa na kukamatwa na kupelekwa katika Kituo cha Polosi. Kutuhumiwa siyo kuhukumiwa! Askari Polisi ni kada iliyofunzwa vizuri nidhamu ikiwemo kutoa na kupokea amri.

Mheshimiwa Rais, hii siyo mara ya kwanza kusikia habari za watuhumiwa kukamatwa wakiwa hai halafu wakafia mikononi mwa Polisi. Lakini, inajenga hofu zaidi hasa pale inapoonekana kwamba idadi kubwa ya wanaokamatwa na kufia mikononi mwa Polisi wanakuwa ni wanasiasa au wanajihusisha na siasa kutoka Vyama vya Upinzani! Dunia yetu ya sasa haiwezi kuielewa Serikali ambayo wananchi wake wakiwemo wa Vyama vya Upinzani wanateswa na kufia katika vituo vya Polisi! Dunia hii haiwezi kutuelewa hata sisi tulio Maaskofu endapo tutaendelea kunyamaza kimya na kuendelea kushangilia Kufufuka kwa Yesu wakati kuna watu wanateswa na kuuawa katika Siku ya Pasaka! Kikubwa zaidi ni kuwa hata Mungu wetu aliyetuweka kuwa waangalizi wa roho za watu hapa duniani hatatuelewa sisi Maaskofu na Wachungaji na hakika atakuja kutudai hesabu kutokana na ukimya wetu. Soma Biblia kutoka kitabu cha Ezekieli 33:1-20.

Ninapokuandikia ujumbe huu Mheshimiwa Rais, ninaogopa sana Nchi yetu inakoelekea. Mimi ninaamini kuwa na wewe hujapendezwa na tukio hili la mauaji ya kijana yule! Mimi ninaamini kuwa na wewe taarifa hizi zilipokufikia mwili wako ulisisimka kwa kuogopa! Hii ni kwa sababu ninaamini kuwa hukuamrisha watu wateswe hadi kufa katika vituo vya Polisi. Siku chache zilizopita nilimwandikia ujumbe Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ulioeleza hofu yangu kuhusu kauli za vitisho kutoka kwa baadhi ya Makamanda wa Jeshi la Polisi. Nilieleza wazi kuwa kauli kama zile zinaweza kupelekea wananchi kuchukulia kuwa Jeshi la Polisi lilikuwa limepanga mauaji endapo mtuhumiwa au watuhumiwa wakafa kwa bahati mbaya au kutokana na makosa ya kiutendaji.

Mheshimiwa Rais, vitendo hivi vinajenga hofu katika Nchi yetu. Hofu hii hupelekea kujenga chuki na visasi miongoni mwa jamii. Chuki na visasi vikizidi wananchi watawachukia viongozi wao, wataichukia Serikali yao na hatimaye watamchukia hata Rais wao. Vitendo kama hivi vikishajenga hofu vitazuia uhuru wa kujieleza na kushauri. Watu wataogopa kushauri pengine watabaki Maaskofu wachache kama mimi ambao wataendelea kushauri bila hofu, woga, huba, wala upendeleo! Lakini ijulikane kuwa hata hao Maaskofu wakishanyamazishwa, Nchi itabaki kuwa na kundi kubwa la wanafiki. Wanafiki ni watu wale wasiosema ukweli, wasioeleza uhalisia, wanaosema mambo ni shwari wakati shwari.

Kwa mtazamo wangu Mheshimiwa Rais, kitendo cha kutoa uhai wa mtu ni kizito sana! Suala hili limekuwa la kijamii, wananchi watatiwa moyo na kufarijika kusikia sauti ya viongozi wao wakuu kama vile Waziri mwenye dhamana au hata Waziri Mkuu. Lakini hata kama kwa hekima yako ukiamua Makamu wa Rais au hata wewe mwenyewe ulisemee itakuwa faraja kubwa sana kwa jamii na kwetu sisi viongozi wa kiroho.

Ninajua wewe Mheshimiwa Rais usingependa watu waonewe na hivyo ninao ujasiri wa kuamini kuwa utahakikisha ukweli unajulikana kuhusu tukio la kuuawa kwa kijana Waziri na kwamba haki inatendeka na watu wanaohusika wanawajibika wenyewe kabla wewe Mheshimiwa Rais haujachukua hatua ya kuwawajibisha!

Ujumbe wangu kwako wewe pamoja na Makamu wa Rais na Waziri Mkuu unapatikana katika Biblia kitabu cha Zaburi 101.

Ninakutakia amani kutoka kwa Kristo aliyefufuka ambaye sasa anatawala pamoja na Mungu katika umoja na Roho Mtakatifu.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches).
FB_IMG_1555921165845.jpeg
 
Magufuli ni kati ya wale wasiojua kuwa maneno huumba.
Kile kiburi alichowapa polisi pale Kurasini kuwa eti wasishughulikiwe kwa madhara wanayosababisha wakiwa kazini, ndio matokeo yake haya!

Kiongozi lazima uwe na akiba ya maneno, unene kwa tahadhari uwe na kinywa kilichotahiriwa. Unajivunia nini kama Amiri jeshi uliyewekwa na watu halafu unaona watu hao hao wakiumizwa na jeshi walilokupa kuliongoza.

Vinywa vetu hubariki vikitumika v'izuri lakini hulaani vinapotumika vibaya.
Damu hiyo naidaiwe mikononi mwa raisi.
 
Magufuli ni kati ya wale wasiojua kuwa maneno huumba.
Kile kiburi alichowapa polisi pale Kurasini kuwa eti wasishughulikiwe kwa madhara wanayosababisha wakiwa kazini, ndio matokeo yake haya!

Kiongozi lazima uwe na akiba ya maneno, unene kwa tahadhari uwe na kinywa kilichotahiriwa. Unajivunia nini kama Amiri jeshi uliyewekwa na watu halafu unaona watu hao hao wakiumizwa na jeshi walilokupa kuliongoza.

Vinywa vetu hubariki vikitumika v'izuri lakini hulaani vinapotumika vibaya.
Damu hiyo naidaiwe mikononi mwa raisi.

Hapa unamuonea Rais. Kama nakumbuka 2014 pale arusha kuna kijana alikamatwa na police kwa kuwa na shule isiyosajiriwa. Jioni ile tuliambiwa kijana amekufa kwa pneumonia. Hahahahaaa. Tulishagaa.

Ni hivi: Baadhi ya police wanatumia nguvu kubwa Juu ya mharifu na hili ni kuvunja haki za binadamu.serikali iangalie ni namna gani kukomesha vitendo hivi
 
Kwa kauli zake alizozitoa mchana kweupe tena mbele ya vyombo vya habari alisema askari wauaji walindwe, na amekua anapewa ushauri wa hovyo sana kuhusu ulinzi na IGP mmoja mstaafu.
kwakifupi hatuna kiongozi pale
 
Hapa unamuonea Rais. Kama nakumbuka 2014 pale arusha kuna kijana alikamatwa na police kwa kuwa na shule isiyosajiriwa. Jioni ile tuliambiwa kijana amekufa kwa pneumonia. Hahahahaaa. Tulishagaa.

Ni hivi: Baadhi ya police wanatumia nguvu kubwa Juu ya mharifu na hili ni kuvunja haki za binadamu.serikali iangalie ni namna gani kukomesha vitendo hivi
Kama kamanda mkuu anaona vizuri kumpoteza mtu anaye mpinga kwanini polisi wasifanye kweli.
 
kwa kauli zake alizozitoa mchana kweupe tena mbele ya vyombo vya habari alisema askari wauaji walindwe, na amekua anapewa ushauri wa hovyo sana kuhusu ulinzi na IGP mmoja mstaafu.
kwakifupi hatuna kiongozi pale
Mkuu anatamani amrudishe tena Mahita ndiye mshauri wake mkuu.
 
Back
Top Bottom