Mheshimiwa Rais, naomba tamka haya na taifa litapona

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,553
44,722
Kwa sasa mtu mwenye ushawishi mkubwa na mwenye uwezo was kuleta mageuzi ni mheshimiwa rais John pombe Magufuli kwani hakuna kikundi Wala taasisi wala mtu mwenye nguvu zaidi yake katika Siasa na maisha ya kawaida hivyo hotuba zake zinachukuliwa kwa uzito mkubwa sana nakuomba:

1. Tangaza kila week wale wanaobaka na kuwalawiti watoto wapewe adhabu Kali. Ukitangaza mara tatu au nne itakuwa ni trending story watanzania wote watakuwa wakilijadili hili so watu wataogopa.

2. Waamuru TCRA wafungie site zote za ngono xnxx, xvideos etc maana watoto wakigusa tu smartphone wanapelekwa huko jamii inaharibika mapema.

3. Marufuku traffic kuomba rushwa na madereva kuwapa rushwa. Ukitangaza hili mara tatu au nne Basi itakuwa trending story hatimaye Watu hawataogopa kuwapa onyo madereva kuhusu kutoa rushwa. Tabia itakoma

4. Wenyeviti wote wa mitaa andikeni majina ya wauza madawa ya kulevya mtaani kimya kimya ili polisi na wanajeshi wayafanyie uchunguzi. Vijana hawa mapusha wa bangi na cocaine wataogopa sana hi kauli; wataacha wenyewe hii biashara.
 
Back
Top Bottom