Ichwampaka
Senior Member
- Nov 19, 2018
- 134
- 109
Mheshimiwa Rais,
Ninaomba kazi ya ukurugenzi wa halmashauri hasa katika maeneo ya kilimo au wafugaji kwasababu ninataka kutumia uzoefu na elimu yangu katika kuimarisha ushirika wa uzalishaji mali katika kilimo au ufugaji. Nina uzoefu wa muda mrefu katika kujenga uwezo wa taasisi ndogo ndogo za kifedha na kwa uzoefu niliojifunza nchi jirani, ninaona kabisa naweza kuwa sehemu ya mabadiliko katika kuhakikisha wakulima na wafugaji wa nchi hii wanajiimarisha katika ushirika au vikundi vya ushirika vya uzalishaji mali. Lengo hasa ni kuwalenga vijana ambao wana nguvu kazi, maarifa na mitaji lakini wanakosa mtu wa kuwapa maarifa ya kuwaunganisha.
Nimejipima mara nyingi nimegundua falsafa yako ya uongozi na mtazamo wako wa mambo, mimi ni mwanafunzi wako bora kabisa. Mimi nataka kutumia ujuzi wangu kuleta mabadiliko. Sitaki na sipendi business as usual nataka kuona mabadiliko hai kwa wananchi utakaonipa ridhaa ya kuwatumikia. Nitataka kuanzisha vikundi katika wilaya au halmashauri ambavyo vitakuwa vinalenga shughuli za kiuchumi. Kununua pembejeo pamoja, kuzalisha pamoja, kuhifadhi mazao pamoja, kutafuta bei pamoja na hatimaye kuuza pamoja. Fedha zitakazo patikana wanavikundi watajenga/kuboresha nyumba zao, kulipia bima za afya, kusomesha watoto wao na pia kulipa kodi kwa nchi.
Ukitazama ardhi iliyolala katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Rukwa, Katavi na Iringa, unajiuliza wako wapi viongozi kuwakusanya wananchi wafanye shughuli za uzalishaji mali badala ya kushinda kutwa kufanya siasa na kubeti? . Vijana wanaweza kuanzisha miradi ya ufugaji kuku wa kienyeji, ufugaji wa samaki, kilimo cha mbogamboga nk. Mashirika na taasisi zinatoa sapoti kwa shughuli hizi zipo tele zimejaa kinachokosekana ni uongozi wa kuwaleta pamoja wananchi.
Mimi naipenda nchi yangu na natamani kuwa sehemu ya Rais JPM ambaye anataka kuibadilisha hii nchi, na anahitaji watu kama sisi tunaoilewa falsafa yake ya uongozi.
tunatekeleza@gmail.com