mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Nakukumbusha mh rais, moja ya ahadi zako kubwa ulizotoa wakati wa kampeni ni kutupunguzia bei ya vifaa vya ujenzi ili sisi masikini tunaoishi kama mashetani tuweze kujitengenezea vibanda vyetu vyenye utu kidogo vya kuishi.
Ni muda sasa sijasikia sio waziri wako wala wewe ukizungumzia mikakati ya kutekeleza hilo. Bajeti ya wizara ya ujenzi na pia ile ya viwanda zimepita bila kulizungumzia hili.
Tunaomba Rais utuambie hii ahadi utaitekeleza lini ili na sisi wanyonge tuweze kuishi kama binadamu, kwa kuachana na maisha ya kijima ya kuishi kwenye nyumba za tembe?!
Ni mimi mpiga kura wako ninayekupenda sana na kukufagilia sana kwa utendaji wako!