Mheshimiwa Rais mkono wa CHADEMA umenyooshwa kwa maridhiano, mpira uko kwako

Hebu toa elimu kidogo.
Rais akiukataa mwito huu wa maridhiano atafanywa nn? Au serikali yake itaathirika vipi? Mbona amewadhulumu wapinzani ktk uchaguzi wa serikali za mitaa mchana kweupe na hakuna chochote kilichotokea?

Nchi nyingine vyama vya upinzani huwa vinajivunia mwamko wa wananchi. Kwamba upinzani ukilalamika tu wananchi wanaliamsha dude. Hapa kwetu wananchi ni maiti, upinzani unajivunia nn?

Hebu tuambie Rais akigomea maridhiano kuna madhara gani kwenye taifa hili la wananchi maiti na mbumbumbu?
Sasa kwa nini mnataka kuwaongoza maiti/mambumbumbu? Muwaibie sio. JPM endelea kubana hadi pesa zote walizo tuibia wazitoe kwenye matundu yao.
 
Mbowe angeonba msamaha angeeleweka zaidi kuliko Hilo neno lake Koko la kuomba maridhiano!!!! Mtu ukimkosea usiende kwake na maneno ya mafumbo ohh maridhiano bull shit go straight repent your sins to him ask for forgiveness

Akusamehe kwanza ndio ukinyooshe kimkono Chako kuwa muanze ukurasa mpya
Shida yenu wapambe huwa hamna muda wa kusoma maandishi ya wenzenu na kuyatafakari. Hapo mwishoni mwa andiko hili nimeomba usichochee kuni maana tuko chini ya paa moja. Jengo likiungua tunateketea sote. Au mwenzetu utakimbilia kwa mabeberu!!!?
 
maridhiano ndio Nini? Chadema walimkosea Sana na kumpuuza Sana Magufuli Leo unakuja ohhh nataka maridhiano!!! Omba msamaha kwanza usanehewe ndipo hizo porojo zako Koko zifuate.Hata Afrika kusini na Rwanda watu walianza kuungama dhambi zao kwanza ndipo yakaja maswala ya maridhiano

Mbowe anaibuka tu anataka maridhiano what about your sins that you committed against Magufuli ? Repent first
Pointi ya kuomba msamaha naiunga mkono. Walikataa kumtambua alipoapishwa. Wakazira kuhudhuria sherehe za nyuma za kitaifa licha ya kualikwa. Wakamwita Rais majina mabaya. Wakamkejeli. Leo eti mardhiano. Mbowe alitakiwa apige magoti aombe msamaha!
 
Wamenyimwa na nani mkuu? Kama chama chao ndio kimewanyima hiyo fursa si wauondoe uongozi?
Ndugu usijifanye mbuni kuficha kichwa kwenye mchanga kupisha tufani!!! Au wewe ni mgeni katika Yerusalemu usjue yaliyotendeka humo siku za karibuni!!!? Jinsi mkuu alivyoshirikiana na wakuu wa wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, watendaji wa Kata, vijiji na mitaa, kuwanyongelea mbali wagombea wa upinzani na kuwapitisha wale wa "Viti Maalum bila kupigiwa kura.!!!?"
 
Ndugu usijifanye mbuni kuficha jichwa kwenye mchanga kupisha tufani!!! Au wewe ni mgeni ni katika Yerusalemu usjue yaliyotendeka humo siku za karibuni!!!? Jinsi mkuu alivyoshirikiana na wakuu wa wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, watendaji wa Kata, vijiji na mitaa, kuwanyongelea mbali wagombea wa upinzani na kuwapitisha wale wa "Viti Maalum bila kupigiwa kura.!!!?"
Kama hawakukidhi vigezo ulitarajia nini? Mimi ni site participant. Sio wa mtandaoni.
 
Kama hawakukidhi vigezo ulitarajia nini? Mimi ni site participant. Sio wa mtandaoni.
Mkuu tuwe wakweli kwa nafsi zetu, Kama kweli Wewe Ni wa site, badala ya kuwa Tomaso na kuja na argument mfu humu, fanya utafiti mdogo tu. Mtafute Mtendaji yeyote wa mtaa au Kijiji umuulize chini ya kiapo cha kutotoa siri, utaelewa nisemacho Wala hutaakisi mapambio ya akina Chakubanga Polepole!!!
 
December 9, 2019
Mwanza, Tanzania

Magufuli alivyowaona vigogo wa CHADEMA alijongea na kuwasalimia

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, amesalimiana na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani katika sherehe za miaka 58 ya uhuru.

Vigogo wa chama cha CHADEMA waliopata nafasi ya kusalimiana na Rais Magufuli ni Mwenyekiti Kanda ya Kati CHADEMA Lazaro Nyarandu, mbunge John Heche, Meya Boniface Jacob, mbunge Joseph Mbilinyi Sugu, mbunge John Mnyika na mbunge Godbless Lema katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Pia Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB) Mh. Freeman Mbowe (MB) aliitwa kusalimia halaiki wa watu uwanjani CCM Kirumba na watanzania kwa jumla waliokuwa wakifuatilia sherehe hizo za uhuru wa Tanganyika majumbani mwao ktk televisheni zao.

Katika sherehe hizo za miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika kulikuwepo pia mabalozi wa nchi za Afrika, Ulaya, Marekani ya Kaskazini, Asia na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kama Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya n.k

Source: Global online TV
 
Very good...

Inaonesha wewe ni msomi wa kweli hasa maana mpangilio wa hoja zako uko perfect kabisa na una reflect usomi wako....

Mimi umenigusa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa....

For sure, CCM na serikali yao ambao ndiyo wenye dhamana na nchi hii kwa uchaguzi huu, walifanya kosa kubwa (grave mistake)

Viongozi wa SM (vijiji & mitaa) kimsingi ndiyo hasa wanaongoza msingi wa maendeleo ya nchi.....

Kama imevurugwa hivi, ni wazi tumevuruga msingi wa maendeleo....

Hivi mwenyekiti wa mtaa au kijiji ambaye hakuchaguliwa kwa ridhaa ya watu wenyewe kwenye kijiji ama mtaa wake, atawezaje kuwaongoza watu hawa??

Je watatumia fimbo ama bunduki kutulazimisha kuwatambua na kuwapa ushirikiano?

Duuh, hali hii ni mbaya sana na kamwe haina mwisho mwema.....
 
Nani anaypendwa kutukanwa?
Kenyatta ana kebehiwa (sio kutukanwa) kila siku na hachukulii mambo hayo personal bali anajua ni siasa. Penye matusi sheria ipo inachukua mkono.
Huwezi kuchukia kundi Fulani, au chama Fulani au eneo fulani kwa sababu mmoja wao au wawili wamekuita mshamba au dikteta! Sio sifa ya uongozi siku hizi.
 
Maridhiano yaende sambamba na kufufua uchunguzi wa washambulizi wa Tundu Lissu pamoja na kuwakamata wale wote waliohusika pamoja na wale waliozing'oa camera za cctv
Kufufua uchunguzi wa wale waliohusika katika kumpoteza Ben Saanane Azory Gwanda na kumuua Alphonce Mawazo ili wafukishwe mbele ya vyombo vya sheria
Wauwaji wa hayati Akwilina wakamatwe mara moja
Mauwaji ya Watanzania huko rufiji uchunguzi ufanyike ili wahusika wafukishwe mahakamani

Kufuta kesi zote za kijinga dhidi ya Wapinzani zilizopo mahakamani

Hapo ndio maridhiano ya kweli yatakapofikiwa.
Hayo ndiyo "maneno" ila uoga utawatinga kuanzia sasa na najua wasiojulikana wako busy kushauri "hakuna cha maridhiano". maisha yetu yana tija bila wao.
Watangoja mpaka waje akile Buthelezi kutuambia. Namhurumia magufuli. Akina bashite watatoka mita siku si nyingi trust me!
 
wakina lema, mnyika, sugu, wameshaona mwakani hawarudi bungeni, wanachofanya ni kumpigia magoti Magufuli awaonee huruma na kuwaachia ubunge wao, chadema wanataka maridhiano kwa maslahi yao binafsi
Na wewe umbulula hawarudi bungeni kwa matakwa ya ccm na serikali au wananchi?
 
Very good...

Inaonesha wewe ni msomi wa kweli hasa maana mpangilio wa hoja zako uko perfect kabisa na una reflect usomi wako....

Mimi umenigusa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa....

For sure, CCM na serikali yao ambao ndiyo wenye dhamana na nchi hii kwa uchaguzi huu, walifanya kosa kubwa (grave mistake)

Viongozi wa SM (vijiji & mitaa) kimsingi ndiyo hasa wanaongoza msingi wa maendeleo ya nchi.....

Kama imevurugwa hivi, ni wazi tumevuruga msingi wa maendeleo....

Hivi mwenyekiti wa mtaa au kijiji ambaye hakuchaguliwa kwa ridhaa ya watu wenyewe kwenye kijiji ama mtaa wake, atawezaje kuwaongoza watu hawa??

Je watatumia fimbo ama bunduki kutulazimisha kuwatambua na kuwapa ushirikiano?

Duuh, hali hii ni mbaya sana na kamwe haina mwisho mwema.....
Mkuu "Kitaturu" hili la serikali za mitaa ni kizungumkuti halisi. Ni jana tu nikiwa nimesimama na madada fulani, akapita Mwenyekiti wa mtaa. Mmoja wa wale madada akamsalimia: "shikamoo Mwenyekiti wa Viti maalum." Yule Mwenyekiti badala ya kuitika akamtaka afute kauli jambo ambalo yule dada hakuliafiki. Kukatokea mzozo lakini yule dada alishikilia msimamo wake akimuuliza Mwenyekiti atoe ushahidi ni akina nani walimpigia kura na Kituo kilikuwa wapi. Kwa unyong'onyevu mkubwa Mwenyekiti aliendelea na Safari yake.
Kibaya zaidi ni kuwa CCM wanataka kutumia dola kuwalinda watu hawa katika kutawala badala ya kuongoza. Na hapo ndipo kutakapotokea sintofahamu na hivyo kuzua tafrani ya Wananchi dhidi yao.
 
Nchi nyingine vyama vya upinzani huwa vinajivunia mwamko wa wananchi. Kwamba upinzani ukilalamika tu wananchi wanaliamsha dude. Hapa kwetu wananchi ni maiti, upinzani unajivunia nn?
Nafikiri hata huo upinzani wa hizo nchi zingine ni tofauti sana na huu wa kwetu uliojiapiza kupinga kila linalofanywa na serikali.

Wananchi waliamshe dude kwa mfano, kwakuwa tu wapinzani wanasema miradi inayotekelezwa na serikali, ujenzi wa reli ya kisasa, bwawa kubwa la kuzalisha umeme kuondokana kabisa na tatizo la umeme nk si kipaumbele cha wananchi?! Hao wananchi watakuwa zaidi ya maiti.
 
Mkuu "Kitaturu" hili la serikali za mitaa ni kizungumkuti halisi. Ni jana tu nikiwa nimesima na madada fulani, akapita Mwenyekiti wa mtaa. Mmoja wa wale madada akamsalimia: "shikamoo Mwenyekiti wa Viti maalum." Yule Mwenyekiti badala ya kuitika akamtaka afute kauli jambo ambalo yule dada hakuliafiki. Kukatokea mzozo lakini yule dada alishikilia msimamo wake alimuuliza Mwenyekiti atoe ushahidi Ni akina nani walimpigia kura na Kituo kilikuwa wapi. Kwa unyong'onyevu mkubwa Mwenyekiti aliendelea na Safari yake.
Kibaya zaidi ni kuwa CCM wanataka kutumia dola kuwalinda watu hawa katika kutawala badala ya kuongoza. Na hapo ndipo kutakapotokea sintofahamu na hivyo kuzua tafrani ya Wananchi dhidi yao.

That's true na ndiyo hali halisi popote....

Subiri wakati wa mikutano ya kuhamasishana maendeleo ufike utaona matokeo yake....

For sure, maeneo mengi ya vijiji na mitaa kutazuka migogoro tu kati ya viongozi na waongozwa....

Huwezi ukaoa au kuolewa na mke ama mume aliyeletwa na baba au mama halafu ndoa hiyo ikawa stable na kudumu....

Hakuna, ndoa ya namna hii sharti iishie njiani tu

Hii ndiyo NDOA ya wananchi na wenyeviti wa SM (vijiji & mitaa) iliyofungwa tarehe 28/11/2019....

Ndoa ya kulazimishana siku zote haijengwi juu ya msingi wa UPENDO na MARIDHIANO.....

Kwa kuwa iko hivi, itatawaliwa na migogoro na palipo na migogoro hakuna shughuli za maendeleo....!!

Hapa ndipo tulipofikishwa na Rais Magufuli na CCM yake!!
 
Shida yenu wapambe huwa hamna muda wa kusoma maandishi ya wenzenu na kuyatafakari. Hapo mwishoni mwa andiko hili nimeomba usichochee kuni maana tuko chini ya paa moja. Jengo likiungua tunateketea sote. Au mwenzetu utakimbilia kwa mabeberu!!!?
Ukikorofishana na mtu usipomwpmba msamaha Moto uko pale pale huwezi uzima kwa kuja na porojo zaidi ya kuja na neno moja to nisamehe nimekosa moja mbili tatu.
Kama unataka Moto uzimike
 
That's true na ndiyo hali halisi popote....

Subiri wakati wa mikutano ya kuhamasishana maendeleo ufike utaona matokeo yake....

For sure, maeneo mengi ya vijiji na mitaa kutazuka migogoro tu kati ya viongozi na waongozwa....

Huwezi ukaoa au kuolewa na mke ama mume aliyeletwa na baba au mama halafu ndoa hiyo ikawa stable na kudumu....

Hakuna, ndoa ya namna hii sharti iishie njiani tu

Hii ndiyo NDOA ya wananchi na wenyeviti wa SM (vijiji & mitaa) iliyofungwa tarehe 28/11/2019....

Ndoa ya kulazimishana siku zote haijengwi juu ya msingi wa UPENDO na MARIDHIANO.....

Kwa kuwa iko hivi, itatawaliwa na migogoro na palipo na migogoro hakuna shughuli za maendeleo....!!

Hapa ndipo tulipofikishwa na Rais Magufuli na CCM yake!!
Zamani zile za ujinga ndoa hizo zililazimika kudumu kwa sababu baba au mama alitishia kumtolea mtoto laana. Lakini leo, kwenye mwangaza huu nani atakubali kuozwa bila ridhaa yake. Thubutu!!!
 
Ukikorofishana na mtu usipomwpmba msamaha Moto uko pale pale huwezi uzima kwa kuja na porojo zaidi ya kuja na neno moja to nisamehe nimekosa moja mbili tatu.
Kama unataka Moto uzimike
"Yehodaya" ni wapi Chadema wamewahi kumkosea Rais Magufuli zaidi ya kumkosoa!!? Chadema mapema kabisa walilalamikia elements za maamuzi ya kidikteta ya Rais. Kama Chama cha siasa cha upinzani ni haki yao kukosoa hata kukemea hali isiyowaridhisha. Tabia hiyo ya maamuzi ya kibabe ya Rais ndiyo imeifikisha nchi katika sintofahamu ya kuwateulia Wananchi viongozi wao.
Sasa kwa kuwa wapinzani wanaonyesha tabia ya kistaarabu ya kutaka MARIDHIANO dhidi ya umwamba, wewe unataka wapige magoti kwanza. Kweli!!!?
 
Nani anaypendwa kutukanwa?
Hakuna ndio maana kuna adhabu ya kisheria ukitukana. Huna sababu ya wewe kuleta ugomvi na kutumia ofisi kupambana na anayekutukana zaidi ya kumkabidhi kunakohusika ajibu tuhuma.
Kutumia ofisi au maguvu kumshambulia aliyekutukana ni kosa kubwa zaidi ya tusi na kisheria nawe ushughulikiwe.
Hata yeye anavyotukana watu nao hawapendi kutukanwa
 
Back
Top Bottom