Zakaria Lang'o
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 2,593
- 2,767
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mkono wa Chama Kikuu cha Upinzani Chadema UMENYOOSHWA kwako kwa ajili ya MARIDHIANO. Je, utaupokea au utausukumia mbali!!?
Alichosema Mwenyekiti wa Chadema kina umuhimu wa pekee. Upinzani kwa ujumla wake una wanachama na wafuasi kwa mamilioni katika nchi. Hivyo ni ukweli ulio wazi kwamba kuwapuuza huku ukiimba wimbo wa umoja wa Watanzania ni kujidanganya.
Nitoe mfano: Katika mtaa ninaoishi wenye wapiga kura 1300, Chadema walifanya sensa na kupata wanachama na wapenzi wapatao 850.Mwenyekiti wa mtaa alikuwa anatokana na Chama hicho, tena mtu mwenye Elimu ya Chuo akiwa amesomea Ujenzi (civil engineering). Ameongoza mtaa kwa ufanisi kwa miaka mitano. Amewashirikisha Wananchi kujiletea maendeleo yao.
Wananchi walikuwa na matumaini ya kumpatia nafasi tena. Sasa matumaini hayo umeyazima kwa kuwateulia "viti maalum" maana ndivyo wanavyojulikana kwa sasa katika mitaa, vitongoji na vijiji. Mwenyekiti mwenye Elimu ya Chuo tena engineering, ameambiwa ameshindwa kujaza fomu kwa sababu hajui kusoma na kuandika!!!
Hali hii inazalisha chuki kwa sababu wengi wanaona kuwa kilichofanyika ni mapinduzi dhidi ya demokrasia yao. Wengi wanatambua kuwa kiongozi wa mapinduzi hayo ni Mhe Rais akiwashirikisha watendaji wa Kata, mitaa na vijiji.
Hebu tutafakari kwa pamoja kwamba Vyama vya upinzani vilivyoweza kuweka wagombea wapatao 600,000, laki sita kwa nchi nzima, Mhe. Rais unawezaje kuwapuuza kwa kutojali haki yao ya msingi ya kuchaguliwa wakati huo huo ukiitaka Tanzania iwe moja!!?
Ni kweli kuwa unahimiza maendeleo. Lakini unasahau kuwa Katiba ya nchi imeweka utaratibu kuwa maendeleo yoyote ni lazima yawe shirikishi. Watu ndio msingi wa maendeleo na kwa hiyo watu walio huru katika maamuzi ya nani awe kiongozi wao ndio chachu kuu ya maendeleo. Katiba ya Jamhuri Ibara ya 3(1) na 146(2)(c) iko wazi juu ya haya niliyoeleza.
Katika uchaguzi huu uliopita majeraha ni makubwa, hivyo ni busara tiba ikapatikana kupitia mkono ulionyooshwa wa Ndugu Mbowe.
Napenda nikukumbushe juu ya kile anachofanya Rais Uhuru Kenyatta kwa rafiki yako Raila Odinga. Rais Uhuru anajenga daraja akimshirikisha rafiki yako huku Wewe ukibomoa madaraja yanayotuunganisha Watanzania katika amani, udugu, haki na Uhuru!!!
Juzi tu Profesa Kabudi alikuwa akiwazodoa Wakenya kwa kutazama kibanzi kwenye macho yao juu ya Ukabila, huku sisi tukiwa na boriti ya ubaguzi wa vyama iliyokomaa!!!
Wakati ni sasa Mhe Rais, usizitazame kijani kwenye mikutano yako ikipiga vigelegele ukadhani Tanzania ni shwari. La, hasha. Hao wengi wao ni wanafiki wanaotumia fursa kwa sababu wanajua mkononi mwako kuna mkate. Ukidondoka kesho hutawaona karibu na wewe hata kidogo.
Mwisho ni imani yangu kuwa Watanzania wenzangu mtakaosoma maoni haya mtasaidia kumhimiza Mhe.
Rais wetu kujenga daraja la maelewano badala ya kumsaidia kuchochea kuni ili kuteketeza jengo la umoja wetu.