Mheshimiwa Rais Magufuli, Tanzania Itamsubiri Mtu Huyu Hadi Lini?

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Mwanzoni tulidhani atakuwa Nyerere, lakini wapi !!
Halafu tukajua ni Mwinyi tu, hapo ndipo mambo yakaharibika kabisa!
Alipokuja Ben na mapishi ya ubinafsishaji katika ndoto usiku, kumbe kulipokucha, ni njaa ya hatari.
Kwa nasibu akatokea JK wa maisha bora kwa kila mtanzania!
Jamani nani ambaye hakumshangilia mtu huyu?

Kiukweli jamaa yetu alikuwa mwerevu mno, maana alipogundua kuwa hicho alichoahidi hakitekelezeki alibadili gia angani bila ruhusa ya chama chake!

Mayowe yakawa katiba mpya, katiba mpya.
Kwa kweli kiongozi wetu huyu tukiacha makando-kando yake mengine; hapa alikuwa sahihi kuliko watangulizi wake!

Na iwapo JK asingekwamishwa na baadhi ya wabinafsi wachache; leo angelikuwa ndiye yule mtu ambaye watanzania walikuwa wanamsubiri kwa hamu kubwa!

Maskini watanzania nani atawapa katiba ya maoni yao kama yalivyopendekezwa katika rasimu ya Warioba?

Huyo atakayefanya hivyo; bila shaka yeye ndiye atakuwa shujaa wetu katika kizazi cha sasa!
Na kamwe haitotokea watanzania wakamsahau maishani mwao, majira nenda majira rudi.

Mhe JPM binafsi ninaukubali utendaji wako wenye kusukumwa na dhamira ya kweli.

Hata hivyo msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Kila binadamu anayo mapungufu yake, ndiyo maana kiongozi bora yafaa asaidiwe na sheria au muongozo bora.
Kwa bahati mbaya watawala wengi wa kiafrika hujifanya hawalioni hili.
Kwamba hivi viwili hutegemeana mithiri ya kuku na yai.
Bila kuku yai hakuna na bila yai kuku hakuna.
Pasipo kiongozi bora hakuna sheria bora na bila sheria bora hakuna kiongozi bora!

Ndiyo maana bado tunaendelea kumsubiri mtu huyo muhimu. Iwe ni asubuhi au ni jioni, iwe ni mchana au ni usiku.
Lakini ukiamuwa kutoangalia uso wa mtu; wewe JPM waweza kuwa ndiye yule taifa linayemngojea!
Mwenyezi Mungu amekupa nafasi na uwezo wa kufanya hivyo kuliko mtu yeyote katika taifa hili kwa sasa.

Nakutakia tafakuri njema mchana huu.
 
Back
Top Bottom