- Anasema kuwa Watanzania wengi wasomi wanashidwa kutumia elimu yao kwa manufaa ya nchi.
- Anasema Watanzania wengi wana "PhDs" wanashindwa kutengeneza au kutoa mazawo ktk suara la kuwa na viwanda
- Anasema wasomi wengi Wamebobea katika elimu wanashindwa kuisaidi nchi.
Makosa
Mheshimiwa Raisi huna wasomi unaowafikiria wewe. Kuwa mbunifu sio lazima uwe na PhDs au umebobea katika elimu. Kwani watu wengi waliosoma sana elimu ya darasani (theory) wanakuwa sio wabunifu na wengi wao wanaishia kufa masikini, wanapenda kukimbilia siasa kwani ndio njia nyepesi ya kupata pesa za wizi. nk. Angalia watu kama Zuckerberg, Billgate, Steven Job (RIP), Brendon na wengine. Hawana PhDs leo hii ndio wanabadilisha maisha ya watu duniani
Tanzania kuna watu kama Ally Mufuruki, Bakhressa, Mengi, na wengine wadogo wadogo sana kama Erick Shigongo, Kusaga, Zadoki hawana hata diploma wametengeneza kazi zaidi ya watu 70 kila mmoja, wamebadilisha maisha ya watu na familia zao. Na wanalipa kodi kuendeleza nchi hii masikini.
Asilimia 78 ya kazi Marekani zinatengenezwa na makampuni binafsi madogo madogo na yanachangia karibu asilimia 46 ya kodi. Ndio maana kila siku wanafundisha watoto wao elimu bora (theory +vitendo +life skills) hili wajasiriamali wazidi kuwa wengi hili wa isaidie Marekani kwenda mbele. Angalia China, Japani, Ujerumani wana system hii pia ya kuongeza na kuboresha viwanda vidogo
SOLUTION
- Tuache siasa za kizamani (wapinzani si maadui).
- Wapinzani wasipinge kushinda hoja tusaidiane nchi ni yetu wote
- Elimu yetu mbovu, imepitwa na wakati (acha kuamini PhDs kama unavyofikilia) amini vitendo kuliko midomo.
- Katiba Mbovu (unafanya kazi vizuri(nakupongeza) una ujasiri zaidi ya Nyerere. Lakini ukiondoka watarudia ya nyuma kwani katiba itawaruhusu kufanya maovu. Tubadilishie
- Viwanda vinaitaji elimu ya kitendo (hatuna), umeme (hatuna). Miundo mbinu (hatuna) mitaji (hatuna) Ali Mufuruki na wafanya biashara ambao wanajua wanafanya nini sio wanasiasa na wapiga domo wameshauri hili.
- Tunahitaji life skills (tuingize kwenye elimu yetu kuanzia vidudu mpaka vyuo vikuu na lazima kila mtu kusoma) ndio maana hatujui tunatoka wapi , tupo wapi tunakwenda wapi.. Mikelele tu