Mheshimiwa Rais Magufuli huu nao ni ufisadi kupitia Rasilimali watu!

makoye2009

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,638
1,218
Kwako Rais JPM najua unapitia pitia kwenye mitandao ya kijamii na nina uhakika utaisoma hii thread(siyo namba) maana tunaoisoma namba ni sisi Watanzania hasa ambao tulitumia demokrasia yetu kuchagua vyama vya siasa tofauti na CCM.

Swala langu ni kuhusu hizi teuzi zinazoendelea ili kukamilisha safu yako ya kukusaidia katika majukumu mazima ya kuongoza serikali yako. Leo umewaapisha Wakurugenzi wa Halmashauri Miji na Majiji wengi wao wakiwa ni wapya kabisa na wageni katika kazi hizi za kuhudumia umma. Umesema kwamba ajira siyo lazima mtu awe na uzoefu baali cheti ingawa kwenye uhalisia ni kinyume chake.

Ninachokiona katika teuzi hizi ni aina nyingine mpya ya kutengeza Ufisadi wa Raslimali watu. Nitaeleza.

Haiwezekani Rais unaingia madarakani halafu uteua watu wote katika kila idara kana kwamba hawa waliokuwepo awamu uliyoikuta wote hawafai........!!! Hii ni aina nyingine ya Ufisadi kwa vile hawa watumishi wapya inabidi walipwe fedha za kujikimu wao na familia zao, nauli zao na mizigo yao huko wanakoenda na mishahara mipya! Lakini pia wakti huohuo kuna hawa ambao wanaondolewa kwenye nafasi hizo nao wanastahili kulipwa malipo hayohayo pamoja na kiinua mgongo kwa kuwastaafisha kwa lazima.

Ukifanya hesabu ya GHARAMA HIZI utakuta NI MABILIONI YA FEDHA ZA KITANZANIA ambazo zingeweza kupelekwa kwenye shughuli nyingine za maendeleo kama maji,umeme, shule, hospitali na mabarabara.

Mimi siamini kuwa wote uliowakuta maofisini wote ni Mafisadi na wala rushwa. Kuna watu waadilifu tu ambao umewaacha kwa kisingizio cha Ufisadi. Katika uteuzi wa Baraza lako la Mawaziri kuna Mawaziri ambao uliwateua na Watanzania wakahoji kwanini wawepo kwenye Baraza lako wakti waliharibu wakti wa JK?

Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo ni mfano ulio hai. Pamoja na kashfa ya Escrow wewe uliamua kumteua kwa kigezo kuwa ni mchapa kazi! Je, ina maana hawa wote ulio waacha kwenye uteuzi huu na mwingine wote ni Mafisadi wala siyo wachapa kazi kama Waziri Muhongo?

Nina hakika fedha itakayotumika kuwalipa hawa waajiriwa wapya na hawa wanaoondoka ni Mabilioni ya fedha ya walipa kodi. Huu nao ni ufisadi tu kama ufisadi mwingine labda tofauti ni kwamba unafanywa na Rais ambaye yuko juu ya sheria na hawezi kushtakiwa popote akiwa madarakani na hata baada ya kuondoka madarakani.

Mheshimiwa Rais lazima ushukru sana kwa vile CCM mmeamua kujitengenezea Katiba inayowalinda Vigogo wa CCM kabla na baada ya Utawala na ndiyo hasa kisa cha kuikataa Katiba mpya.

Wasalaam.
 
Nilisikia ajira zimesitishwa kwa miezi isiyozidi miwili.

Au hawa malipo yao hayapitii hazina?
 
Jiburudishe kwa picha hii kijana usije ukashindwa kumeza mate....kila mtu anajaribiwa kwa awamu yake...mpe.mkuu muda afanye kazi
 

Attachments

  • us-president-barack-obama-talks-with-staff-along-the-colonnade-of-ctdkya.jpg
    us-president-barack-obama-talks-with-staff-along-the-colonnade-of-ctdkya.jpg
    32.9 KB · Views: 34
Back
Top Bottom