Mheshimiwa Rais Magufuli huu nao ni ufisadi kupitia Rasilimali watu!


makoye2009

makoye2009

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2009
Messages
2,644
Likes
499
Points
280
makoye2009

makoye2009

JF-Expert Member
Joined Jun 12, 2009
2,644 499 280
Kwako Rais JPM najua unapitia pitia kwenye mitandao ya kijamii na nina uhakika utaisoma hii thread(siyo namba) maana tunaoisoma namba ni sisi Watanzania hasa ambao tulitumia demokrasia yetu kuchagua vyama vya siasa tofauti na CCM.

Swala langu ni kuhusu hizi teuzi zinazoendelea ili kukamilisha safu yako ya kukusaidia katika majukumu mazima ya kuongoza serikali yako. Leo umewaapisha Wakurugenzi wa Halmashauri Miji na Majiji wengi wao wakiwa ni wapya kabisa na wageni katika kazi hizi za kuhudumia umma. Umesema kwamba ajira siyo lazima mtu awe na uzoefu baali cheti ingawa kwenye uhalisia ni kinyume chake.

Ninachokiona katika teuzi hizi ni aina nyingine mpya ya kutengeza Ufisadi wa Raslimali watu. Nitaeleza.

Haiwezekani Rais unaingia madarakani halafu uteua watu wote katika kila idara kana kwamba hawa waliokuwepo awamu uliyoikuta wote hawafai........!!! Hii ni aina nyingine ya Ufisadi kwa vile hawa watumishi wapya inabidi walipwe fedha za kujikimu wao na familia zao, nauli zao na mizigo yao huko wanakoenda na mishahara mipya! Lakini pia wakti huohuo kuna hawa ambao wanaondolewa kwenye nafasi hizo nao wanastahili kulipwa malipo hayohayo pamoja na kiinua mgongo kwa kuwastaafisha kwa lazima.

Ukifanya hesabu ya GHARAMA HIZI utakuta NI MABILIONI YA FEDHA ZA KITANZANIA ambazo zingeweza kupelekwa kwenye shughuli nyingine za maendeleo kama maji,umeme, shule, hospitali na mabarabara.

Mimi siamini kuwa wote uliowakuta maofisini wote ni Mafisadi na wala rushwa. Kuna watu waadilifu tu ambao umewaacha kwa kisingizio cha Ufisadi. Katika uteuzi wa Baraza lako la Mawaziri kuna Mawaziri ambao uliwateua na Watanzania wakahoji kwanini wawepo kwenye Baraza lako wakti waliharibu wakti wa JK?

Waziri wa Nishati na Madini Sospeter Muhongo ni mfano ulio hai. Pamoja na kashfa ya Escrow wewe uliamua kumteua kwa kigezo kuwa ni mchapa kazi! Je, ina maana hawa wote ulio waacha kwenye uteuzi huu na mwingine wote ni Mafisadi wala siyo wachapa kazi kama Waziri Muhongo?

Nina hakika fedha itakayotumika kuwalipa hawa waajiriwa wapya na hawa wanaoondoka ni Mabilioni ya fedha ya walipa kodi. Huu nao ni ufisadi tu kama ufisadi mwingine labda tofauti ni kwamba unafanywa na Rais ambaye yuko juu ya sheria na hawezi kushtakiwa popote akiwa madarakani na hata baada ya kuondoka madarakani.

Mheshimiwa Rais lazima ushukru sana kwa vile CCM mmeamua kujitengenezea Katiba inayowalinda Vigogo wa CCM kabla na baada ya Utawala na ndiyo hasa kisa cha kuikataa Katiba mpya.

Wasalaam.
 
L

laki si pesa.

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Messages
10,048
Likes
8,746
Points
280
L

laki si pesa.

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2015
10,048 8,746 280
Umeshaambiwa wenye experience ni wezi na mafisadi bora wateuliwe wapya wazalendo wakasafishe halmashauri
 
SUPER PREDATOR

SUPER PREDATOR

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Messages
2,089
Likes
289
Points
180
Age
58
SUPER PREDATOR

SUPER PREDATOR

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2014
2,089 289 180
Sasa mkuu Profesa muhongo ameingiaje hapa maana mimi sioni tatizo la muhongo
 
M

Mtimbo

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2012
Messages
1,335
Likes
526
Points
280
M

Mtimbo

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2012
1,335 526 280
prof Muhongo ni mtuhumiwa tu kama mulivyomtuhumu Edwad lowassa
 
Amoxlin

Amoxlin

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Messages
3,617
Likes
3,675
Points
280
Amoxlin

Amoxlin

JF-Expert Member
Joined May 30, 2016
3,617 3,675 280
Nilisikia ajira zimesitishwa kwa miezi isiyozidi miwili.

Au hawa malipo yao hayapitii hazina?
 
M

magafumukama

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2016
Messages
742
Likes
196
Points
60
Age
68
M

magafumukama

JF-Expert Member
Joined May 31, 2016
742 196 60
Wewe kijana umeshaoa? Una mke na watoto? Kweli? Shauri yako
 
brokergeneral

brokergeneral

Senior Member
Joined
Jun 21, 2016
Messages
132
Likes
38
Points
45
Age
50
brokergeneral

brokergeneral

Senior Member
Joined Jun 21, 2016
132 38 45
Umeongea ukwel ila nashaka huenda Leo ukakamatwa kwa ajili ya mahojiano
 
G

Ghost Worker

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Messages
814
Likes
992
Points
180
G

Ghost Worker

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2016
814 992 180
Bora tu ionekane kuwa ufisadi kuliko kuwa na DED form 4, wasomi wote hawa.
 

Forum statistics

Threads 1,235,082
Members 474,351
Posts 29,211,571