JembeNaNyundo
JF-Expert Member
- Dec 9, 2016
- 533
- 652
Kwa miaka mingi sana kumekuwa na ukakasi wa madaktari bingwa kupandishwa madaraja yao ya mshahara pindi wanapotoka masomoni. Hawa ni madaktari ambao waliajiriwa kazini wakiwa kama Registrars au Medical Officers (au generalist) na kisha kuruhusiwa na serikali kwenda kujiendeleza katika kiwango cha udaktari bingwa na baada ya kuhitimu wanarudi kazini na kuanza kufanya kazi kama madaktari bingwa.
Kuna madaktari bingwa waliomaliza digrii yao ya pili na ya tatu ya udaktari bingwa toka mwaka 2011, na wamekuwa wakifanya kazi ya kidaktari bingwa lakini bado wanalipwa mishahara ya daktari wa kawaida (generalist). Kwa kweli hii inawavunja sana mioyo hawa madaktari, na baadhi yao wamekuwa wakiacha kazi na kwenda kufanya kazi private sector au nje ya nchi. Kweli inaudhi sana.
Matatizo ya kupandishwa madaraja ya mshahara yapo sana kwa watumishi waliopo chini ya Wizara ya Afya toka enzi na enzi. Sijui shida ni nini? Ukienda kwa RAS watakwambia wewe tutakupandisha daraja kwenye budget ya mwaka ujao. Sasa mimi wakati napelekwa shule hawakujua kwamba baada ya miaka kadhaa tutakuwa na mtu mwenye elimu ya udaktari bingwa. Pamoja na hayo kwa madaktari waliopo TAMISEMI wao angalau wana ahueni kidogo ukilinganisha na wale waliopo wizara ya Afya.
Rais Magufuli, tusaidie kuhamisha maofisa ajira wote walioko Wizara ya Afya waende kwenye hospitali zilizoko chini yake kama Kibong'oto, Mirembe, Mbeya n.k. Uwapo wao kule Wizarani unawafanya wasifanye kazi zao na kutojali. Lakini pia UTUMISHI na HAZINA wamekuwa hawana link nzuri na wizara ya Afya.
Ninashangaa hata pale Waziri wa Wizara ya Afya alipotamka wanataka wachukue hospitali za mikoa ziwe chini ya Wizara ya Afya, wakati kufanya recategorisation tu kwao ni issue zinazotumia at least miaka mitano.
Tusiwakatishe tamaa madaktari hawa. Hata call allowance pia walipwe. Huo uhakiki usiathiri stahili zao.