Mheshimiwa Rais kuongelea mno jinsia yake pengine ni kukosa washauri wa dhati na wa maana

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Mwanzoni nilidhania ni suala la muda tu kwa Rais Samia kuongelea 'uanamke' wake. Nilidhani ni sehemu ya udhaifu wake kuzungumzia wanawake ni kunyanyasika kwao, nikaona ni suala la muda tu atakuja kuachana na udhaifu huu wenye ukakasi masikioni mwa watu haswa wanaume.

Ikaja hotuba ya pili, ikaja ya tatu na ya nne. Ghafla ukawa ni utaratibu wa Rais kuhutubia akiongelea kwanza yanayohusiana na hotuba ya siku hiyo halafu kwa uchungu anakuwa anaongelea kama vile anawasuta au anawapiga vijembe wanaume. Sifa ya wanaume ni uvumilivu na uwezo wa kuweka kila kitu moyoni kama vile hakuna kinachoendelea.

Mama anadai mwanaume ni muweka mbegu tu na kila kitu kinafanywa na mwanamke!. Niliwatazama wanaume pale ukumbini sura zao nikaona baadhi ni zile ambazo kwa kingereza zilikuwa 'uncomfortable' yaani ni kama walikuwa pale kwa kulazimishwa tu.

Nilichokibaini ni kwamba Mama Samia licha ya kuwa ni rais mwanamke wa kwanza wa JMT, bado ni cheo ni kile kile na chenye kuambatana na udhaifu ule ule wa siku zote. Ni Mheshimiwa Rais na anapigiwa mizinga 21 kwa heshima yake. Huyu ni mtu mkubwa sana hata kama anao uwezo wa kujishusha na kuonekana kama vile ni dhalili katika baadhi ya nyakati.

Nahisi kuwa Rais Samia anaogopwa na washauri wakilinda mkate wao wa kila siku, hivyo anakuwa haingiliki wala hasogeleki karibu yake, zaidi ya ule ukaribu walionao wale wapambe kinamama wanaokuwa nae siku zote. Rais kazungukwa na wapambe wenye kumpatia uhuru unaopitiliza. Au pengine wanaogopa ule ule 'uanamke' wake, kwamba wanajiuliza wamshauri au wasimshauri wakiwa na nia ya siri ya kulinda kibarua chako.

Vinginevyo umefika wakati wa Mheshimiwa Rais Samia kuachana na hizi dhana zenye kumuonyesha kama ni mtu mwenye kulalamika muda mwingi akiwakejeli wanaume. Anakuwa anawasuta baadhi ya wanaume wenye ukaribu na ile dhati ya moyo kila wanapojihusisha na masuala ya urais wake. Kila kitokacho kinywaji mwake ni agizo la aina fulani na linawekwa kwenye rekodi za kiofisi au za kijamii.

Nawasalimu kwa jina la JMT.
 
Back
Top Bottom