Mheshimiwa Rais, kabla ya watoto kurudi shule, wewe toka kwanza nyumbani kwako Chato rudi ofisini Ikulu

Nchi haina pesa, inabidi tu watu wadanganye kuwa Coronavirus wamekufa kutokana na hotuba za mkuu, zenye nguvu za kuua kimelea yoyote.
Uzalishaji umeshuka Sana, serikali imefilisika....... Hamna mapato yatokanayo na utalii na sekta nyingine kumedorora.
Hali mbaya utalii umeshuka sana mapato ya utalii ni zero ,kama watalii hawaji na hotel zimefungwa zote,ndege haziingia na kutoka,wafanyakazi wa hotel wote wapo likizo,shule binafsi hali mbaya walimu hawalipwi ukiona hiyo chain ilivyo ni balaa,mapato ya PAYE yameshuka,Utalii mapato sifuri inabidi tu waje kutudanganya tu kwamba tutaishi navyo kama ilivyo ukimwi,wanachoshindwa kutuambia ukweli kwamba ukimwi sio issue tena ila FUTA likikukamata(kama ukiwa na nyemelezi) within 24hrs unaenda kumlaki bwana yesu mawinguni aka unapendwa zaidi aka unakata moto.
 
Nchi haina pesa, inabidi tu watu wadanganye kuwa Coronavirus wamekufa kutokana na hotuba za mkuu, zenye nguvu za kuua kimelea yoyote.
Uzalishaji umeshuka Sana, serikali imefilisika....... Hamna mapato yatokanayo na utalii na sekta nyingine kumedorora.

Well said na ndo maana tunataka atoke huko arudi ofisini.

Waliojenga ofisi si wajinga, wanajua ukifanyia kazi nyumbani kuna mambo mengi ya social kwa hiyo huwezi kuperform to a maximum

Lakini pia kitendo cha yeye kuigeuza nyumba yake ofisi kunawanyima wakazi wa nyumba yake hiyo wakiwemo watoto wake na wajukuu zake haki ya kusocialize na wananchi hapo sababu ya maulinzi ulinzi ya watu wa usalama.

Rais atoke huko arudi ofisini ili wakazi wa nyumba hiyo waendelee kuombana chumvi na wananchi wenzao, kutembeleana na wananchi wenzao, watoto waweze kucheza na wenzao kwa uhuru, wapita njia waendelee kupita bila kuangaliwa angaliwa na mashushushu wa TISS.

Kiufupi arudi tu ofisini achape kazi kikamilifu
 
Rais Magufuli ni nahodha bora ametuvusha salama kwenye corona

Vibaraka wa mabeberu wanaenda kuaibika vibaya

Sawa, Nahodha haongozi meli kutokea seating room, bed room au varanda,
huongoza meli kutokea kwente cabin maalum, cabin maalum ya rais ni Ikulu ya wananchi. Arudi tu Ikulu aongoze nchi yetu vizuri
 
Tusubiri tamko j pili la kufungua vyuo.si unajua Jiwe ka miss headlines za kimataifa

Dark Side
 
Kuna wadau humu waliobobea kwenye masuala ya kisiasa na kiintelijensia kama Pascal Mayalla, walitoa ufafanuzi wa kina ya kwamba Rais anaweza akafanya shughuli zake za kiofisi huku akiwa mahali popote pale ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Hivyo mkuu mtoa mada, usiwe na hofu yoyote ile juu ya hilo. Mwezi ujao (wa sita) tunamtegemea aende Dodoma kulihutubia na pia kulivunja Bunge letu. Baada ya hapo, nina imani atarejea Ikulu ya Dar au atabaki kwenye ile Ikulu ya Chamwino.
Kwahiyo wewe kipimo chako cha ukweli wa taarifa ni Mayalla

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom