Mheshimiwa Rais, kabla ya watoto kurudi shule, wewe toka kwanza nyumbani kwako Chato rudi ofisini Ikulu

Rais Magufuli ni nahodha bora ametuvusha salama kwenye corona

Vibaraka wa mabeberu wanaenda kuaibika vibaya
ila we jamaa wagaunanifurahisha mnooo 😁😁😁 popote ulipo agazi bia na kitimoto utalipa mwenyewe 👍👍

CCM CHAMA CHA BABA NA MAMA
 
Ww unapungukiwa na nini akiwa chato na inazidi kitu gani kwako akiwa dodoma
Kwa mujibu wa sheria za nchi ofisi rasmi ya raisi ni Ikulu, Ikulu zozote zilizo ndani ya nchi na wala siyo nyumbani kwake.

Kwa sasa zaidi ya siku 50 Rais anafanyia kazi za nchi ndani ya nyumba yake huko Chato, sijajua yale mafaili confidential ya nchi anayaweka sebuleni kwake au dining room, hili hakuna anayelijua.

Hata hivyo raisi juzi kwenye hotuba ya kisiasa aliyoitoa akiwa madhabahuni alisikika akisema kuwa anakusudia kufungua vyuo maana anaamini nchini mambo ni shwari korona siyo tishio sana.

Mimi ningependa kumwambia ndugu rais kwamba, kabla ya kufungua vyuo rudi kwanza ofisini. Wakati akiwataka maelfu ya watumishi ambao ni waalimu warudi mashuleni kuchapa kazi basi ni muhimu naye akarudi katika ofisi ambayo kisheria ndiyo anayopaswa kufanyia shughuli za kiofisi.

Nyumba ya rais huko Chato siyo ya kwake peke yake, ni yake na mkewe. Mkewe ana haki ya kuchagua mtu gani aingie ndani ya nyumba hiyo, hata hivyo Ikulu siyo yake na mkewe kwa hiyo hawana haki ya kumkatalia mtu yeyote kwenda kupata huduma ya raisi au taasisi ya uraisi yenye ofisi zake Ikulu.

Kitendo cha raisi kufanyia kazi za nchi kwenye nyumba yake binafsi kinawanyima haki ya kupata huduma za kiofisi wananchi wengi wenye kutaka kupata huduma za kiofisi za raisi.

Kitu kingine ni kwamba nyumba ya raisi huko Chato haikujengwa makhsusi kuwa na hadhi ya Uraisi, haikuwekewa vifaa vyote vya ulinzi stahiki wa mtu anayekalia kiti cha rais, kwa hiyo ni security risk kwa rais kuendelea kukaa kwenye nyumba hiyo binafsi.

Kama rais anadhani Korona ipo under control atoke huko Chato kwenye nyumba ya mama yetu mama Janet aje kwenye nyumba ambayo wananchi wamemuweka afanye kazi zetu.

Ndugu rais uko nje ya ofisi kwa muda mrefu sasa, rudi ofisini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais ni taasisi bwashee!
 
Kuna wadau humu waliobobea kwenye masuala ya kisiasa na kiintelijensia kama Pascal Mayalla, walitoa ufafanuzi wa kina ya kwamba Rais anaweza akafanya shughuli zake za kiofisi huku akiwa mahali popote pale ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Hivyo mkuu mtoa mada, usiwe na hofu yoyote ile juu ya hilo. Mwezi ujao (wa sita) tunamtegemea aende Dodoma kulihutubia na pia kulivunja Bunge letu. Baada ya hapo, nina imani atarejea Ikulu ya Dar au atabaki kwenye ile Ikulu ya Chamwino.
Mwalimu anaweza ita wanafunzi wake bar akaanza kuwapigisha pindi ni kweli kabisa ulichokisema
 
Ewaaaaaaa heko mleta mada

2396740_IMG_20200511_213146.jpeg
 
Rais Magufuli ni nahodha bora ametuvusha salama kwenye corona

Vibaraka wa mabeberu wanaenda kuaibika vibaya
Endelea kudhihaki hili janga kwa kuwa halijakupata. Likikupata utagundua tu tutakapona hatuzioni posts za robot anayeitwa Bia yetu
 
Back
Top Bottom