Mheshimiwa Rais, kabla ya watoto kurudi shule, wewe toka kwanza nyumbani kwako Chato rudi ofisini Ikulu

Nimeona Clip ila cha kushangaza hajasimamishwa na watu barabarani aongee nao :D :D :D :D :D amewapita kama hawaoni ,sasa ile safari mbona nasikia ni ya Dodoma Chamwino? ila safi maana Dodoma na Dar kwasasa zinafukuzana kwa "FUTA".
Hahaha...washenzi sana nyie, ungeanalia TBC au angalia Ikulu YouTube, kasimama tena kahutubia muda mrefu tu mkuu na akawasifia vile hawana hofu na kazungumzia pia mazungumzo yake na Kenyatta jana na leo kuhusu mambo ya mpakani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok mkuu sina access na TV huku nilipo ila pia nina allergy na TBC1 whether online or via TV,kama amesimamishwa ngoja nipate updates za kigogo kwanza kama kweli alisimama.
 
Ok mkuu sina access na TV huku nilipo ila pia nina allergy na TBC1 whether online or via TV,kama amesimamishwa ngoja nipate updates za kigogo kwanza kama kweli alisimama.
Waambie hao (kigogo) waache uoga, mambo ya kutublock ni utoto na ni ukiukwaji wa haki ya kikatiba ya kutoa maoni yetu (freedom of speech and expression), wao wanataka watukanaji tu wanaowapinga basi kufuli, huo ni udikteta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waambie hao (kigogo) waache uoga, mambo ya kutublock ni utoto na ni ukiukwaji wa haki ya kikatiba ya kutoa maoni yetu (freedom of speech and expression), wao wanataka watukanaji tu wanaowapinga basi kufuli, huo ni udikteta.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukimpinga anakublock
Hii mijamaa ni ya kuiignore
Bora hap jf ambapo tunapashana misuli mnyamwezi akishindwa anaenda kujificha kwa muda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mujibu wa sheria za nchi ofisi rasmi ya raisi ni Ikulu, Ikulu zozote zilizo ndani ya nchi na wala siyo nyumbani kwake.

Kwa sasa zaidi ya siku 50 Rais anafanyia kazi za nchi ndani ya nyumba yake huko Chato, sijajua yale mafaili confidential ya nchi anayaweka sebuleni kwake au dining room, hili hakuna anayelijua.

Hata hivyo raisi juzi kwenye hotuba ya kisiasa aliyoitoa akiwa madhabahuni alisikika akisema kuwa anakusudia kufungua vyuo maana anaamini nchini mambo ni shwari korona siyo tishio sana.

Mimi ningependa kumwambia ndugu rais kwamba, kabla ya kufungua vyuo rudi kwanza ofisini. Wakati akiwataka maelfu ya watumishi ambao ni waalimu warudi mashuleni kuchapa kazi basi ni muhimu naye akarudi katika ofisi ambayo kisheria ndiyo anayopaswa kufanyia shughuli za kiofisi.

Nyumba ya rais huko Chato siyo ya kwake peke yake, ni yake na mkewe. Mkewe ana haki ya kuchagua mtu gani aingie ndani ya nyumba hiyo, hata hivyo Ikulu siyo yake na mkewe kwa hiyo hawana haki ya kumkatalia mtu yeyote kwenda kupata huduma ya raisi au taasisi ya uraisi yenye ofisi zake Ikulu.

Kitendo cha raisi kufanyia kazi za nchi kwenye nyumba yake binafsi kinawanyima haki ya kupata huduma za kiofisi wananchi wengi wenye kutaka kupata huduma za kiofisi za raisi.

Kitu kingine ni kwamba nyumba ya raisi huko Chato haikujengwa makhsusi kuwa na hadhi ya Uraisi, haikuwekewa vifaa vyote vya ulinzi stahiki wa mtu anayekalia kiti cha rais, kwa hiyo ni security risk kwa rais kuendelea kukaa kwenye nyumba hiyo binafsi.

Kama rais anadhani Korona ipo under control atoke huko Chato kwenye nyumba ya mama yetu mama Janet aje kwenye nyumba ambayo wananchi wamemuweka afanye kazi zetu.

Ndugu rais uko nje ya ofisi kwa muda mrefu sasa, rudi ofisini!
Amekusikia karudi leo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waambie hao (kigogo) waache uoga, mambo ya kutublock ni utoto na ni ukiukwaji wa haki ya kikatiba ya kutoa maoni yetu (freedom of speech and expression), wao wanataka watukanaji tu wanaowapinga basi kufuli, huo ni udikteta.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unataka kuniuzia mimi msala :D :D :D :D huo ujumbe wako kashaupata maana anapitia pia JF.
 
Back
Top Bottom