Mheshimiwa Peter Serukamba-uko na wananchi au mafisadi?

Shalom

JF-Expert Member
Jun 17, 2007
1,315
124
Nimesoma humu JF na kwenye magazeti mbalimbali habari ninazo ziona kuwa si njema kuhusiana na Mheshimwa Peter Serukamba. Inaonekana huyu mbuge ambaye kwa kweli ni kijana ameamua kuwa upande wa mafisadi na si upande wa wananchi katika muda huu ambao nchi nzima ina kilio nao (anajiamini sana!).

Hizi habari nilipozisoma sijashangaa sana kwa kuwa namjua kidogo huyu mheshimiwa na kwa kweli huyu ni mtu ambaye yuko tayari kufanya lolote ili mradi roho yake ifurahi au anufaike binafsi. Kwa hili jambo najua wazi ameamua kuwatetea hawa mafisadi kwa manufaa yake binafsi hasa ya kupenda madaraka nje ya uwezo wake. Kwa kiasi Fulani anafanikiwa lakini si vizuri tuwafuge watu wa aina hii tena. Huyu akifika kwenye miaka 50 tayari ni mafia mwingine .

Ombi langu kwa JF ni kuomba tumrekebishe huyu angali bado mbichi la sivyo hili nalo ni bomu la kutegwa na litatugharimu sana kulitengua!!
 
Huyuhana lolote anajikomba ili kujiakikishia uteuzi wa 2010, hawa ndo tunajua kabisa hawana machungu na nchi anachotaka ni kuendelea kuwakumbatia viongozi wezi ili na yeye anukie harufu ya pesa za wizi. Dawa yake ni kumshitaki kwa wanchi wake halafu aone kama wadanganyika bado wamelala kama anavyofikiri.
 
Shalom hili ni wazo zuri sana, hasa kujua datas zake zote na uhusiano wake uliopo katika juhudi zake za kutetea wezi wa vijisenti vyetu! Kijana kama yeye kutetea mawazo mgando kwamba fisadi asiguswe kwa vile anakisaidia chama?? huyu aweza kuja kuwa fisadi wa mafisadi na mbabe wa hali ya juu! Inabidi afungwe speed gavana!
 
HUYU MHESHIMIWA NA WAFUATAO NI HATARI KWA NCHI HII

MATHAYO DAVID MATHAYO
DR. CYRIL CHAMI
NA wengine vijana wenzetu siju kama ni wanachama wa hapa jamvini, wangekuwa wanakuja hapa tunawapa somo
 
Shalom hata mie nilikuwa najifikiria sana; tungejua elimu yake; historia yake; na silka yake kama strategy to be built basing on those; wananchi wake wajue undani wa mijadala yake; waipime waamue; kama anastahili au la; si mtu wa kufuga TZ ya leo; tatizo ana wananchi wako remote; hawapati undani na kelele za kifisadi anazopiga naona hazisikii kabisa, na akipewa hela ( maana ndio anatafuta) za EPA/Richmond/Radar etc anaweza kubadili upepo wa watu wake kwa zawadi; Invisible/MM/Lunyungu Mpo?????
 
nachoshindwa kuelewa, mafisadi huwa wananunua jamaa kama huyu serukamba kwa hela kiasi gani?? maana kuteam up na mafisadi kuna lengo fulani si hivi hivi tu unless na yeye alikuwa ni mfisadi tangu huko nyuma lakini alikuwa amekula jiwe na sasa imetimia muda ibilisi kuonyesha makucha na rangi zake zote
 
Shalom hata mie nilikuwa najifikiria sana; tungejua elimu yake; historia yake; na silka yake kama strategy to be built basing on those; wananchi wake wajue undani wa mijadala yake; waipime waamue; kama anastahili au la; si mtu wa kufuga TZ ya leo; tatizo ana wananchi wako remote; hawapati undani na kelele za kifisadi anazopiga naona hazisikii kabisa, na akipewa hela ( maana ndio anatafuta) za EPA/Richmond/Radar etc anaweza kubadili upepo wa watu wake kwa zawadi; Invisible/MM/Lunyungu Mpo?????

This is amazing!!!!

Jamaa anatetea Mafisi maji wakati wananchi anaowawakilisha hapo mjengoni hawajui hata lami ni rangi gani??

Is he representing people au anawawakilisha Mafisi maji huko bungeni?? Na kwamanufaa ya nani??

Tishio la kumripoti Mama kwa spika la nini?? Lazima aelewe kwamba, msema kweli ni mpenzi wa Mungu, mashetani humkimbia. Hivyo lazima ajue kama yeye amepotea kwa vile Chama cha majambazi kilimuingiza kwa Ufisadi kwenye hiyo position iko siku itamtoka, probably 2010. Na ataingia mtu ambae anawakilisha jammii na siyo muwakilishi wa mafisadi.
 
Kila Mtu Ana Haki Ya Kusimamia Anachoamini Ni Kweli,hata Kama Wewe Unaona Si Kweli.namjua Mh Serukamba,ni Kijana Anaesema Kweli Na Haogopi Kusimamia Ukweli Anaohamini,ni Mpiganaji Hasiechoka,ndio Maana Alimwangusha Kaburu Kigoma....unajua Zamani Inasekana Kuna Mwanafalsafa Mmoja Alidai Kuwa Dunia Ni Duara Na Sio Bapa,alibishana Na Watu Wote Mpaka Wakamuua.lakini Leo Historia Imeona Nani Ni Kweli,leo Hii Mnaweza Kuona Serukamba Hayuko Sawa Lakini Ni Kwa Mtazamo Wa Masafa Mafupi,historia Itamuona Tofauti Na Hayo Mnayowaza.
 
Namfahamu kidogo tu Selukamba,Anapenda sana sifa,anapenda sana kuonekana bab kubwa yaani kujitutumua kupita kiasi na kubwa zaidi ni rafiki wa karibu na kibaraka wa mtoto wa EL yule Fred.Na ubunge wake ameupata kupitia kulekule.........................
 
Ubunge ameupata kupitia kwa Fred? mambo unataka uanze kutusadikisha vitu ambavyo siyo kweli. Mh. Peter Serukamba kamba alivyo Zito Kabwe ni kijana mwenye uchungu na nchi lakini pia na chama chake alichokizungumza Peter huko kwenye NEC ni kitu kizuri kwa chama japo ukiwa unaangalia macho juu juu huwezi kulielewa hilo.Walikuwa kwenye forum ya chama chao na walikuwa wanajaribu kuangalia namna bora ya kukisafisha chama huku wakiwa hawaachi shimo watakalojitumbukiza wenyewe kama ambavyo akina ole sendeka na wengineo wanavyoelekea bila kujijua kukiangamiza chama chao.
 
Please, mtu mwenye uchungu na nchi hawezi ku side na Mafisadi kamwe .Huyo jamaa ni MZANDIKI, KIBARAKA aneyetumiwa na watu kwa uroho wa madaraka tu , ila JF itamuweka wazi na wananchi wa jimboni kwake wataamua 2010
 
Selukamba ni kibaraka mkubwa wa mafisadi na anapenda sana kuwa karibu na familia ya EL,ninahakika ametumwa na mafisadi kuongea hizo pumba zake.
 
Ubunge ameupata kupitia kwa Fred? mambo unataka uanze kutusadikisha vitu ambavyo siyo kweli. Mh. Peter Serukamba kamba alivyo Zito Kabwe ni kijana mwenye uchungu na nchi lakini pia na chama chake alichokizungumza Peter huko kwenye NEC ni kitu kizuri kwa chama japo ukiwa unaangalia macho juu juu huwezi kulielewa hilo.Walikuwa kwenye forum ya chama chao na walikuwa wanajaribu kuangalia namna bora ya kukisafisha chama huku wakiwa hawaachi shimo watakalojitumbukiza wenyewe kama ambavyo akina ole sendeka na wengineo wanavyoelekea bila kujijua kukiangamiza chama chao.

Kuwa kwake karibu nao ndio kumemfikisha hapo alipo hata yeye anakiri hivyo.Kwa hiyo analipa fadhila kuwatetea bila kuangalia alama za nyakati
 
Kila Mtu Ana Haki Ya Kusimamia Anachoamini Ni Kweli,hata Kama Wewe Unaona Si Kweli.namjua Mh Serukamba,ni Kijana Anaesema Kweli Na Haogopi Kusimamia Ukweli Anaohamini,ni Mpiganaji Hasiechoka,ndio Maana Alimwangusha Kaburu Kigoma....unajua Zamani Inasekana Kuna Mwanafalsafa Mmoja Alidai Kuwa Dunia Ni Duara Na Sio Bapa,alibishana Na Watu Wote Mpaka Wakamuua.lakini Leo Historia Imeona Nani Ni Kweli,leo Hii Mnaweza Kuona Serukamba Hayuko Sawa Lakini Ni Kwa Mtazamo Wa Masafa Mafupi,historia Itamuona Tofauti Na Hayo Mnayowaza.
Another Shy? ooh sorry,kusimamia anayoyasema hatumkatazi ila ya mantiki yoyote kwa maslahi ya taifa?...Mkuu tuambie mtazamo wa masafa marefu kwa mheshimiwa huyu?
 
Ubunge ameupata kupitia kwa Fred? mambo unataka uanze kutusadikisha vitu ambavyo siyo kweli. Mh. Peter Serukamba kamba alivyo Zito Kabwe ni kijana mwenye uchungu na nchi lakini pia na chama chake alichokizungumza Peter huko kwenye NEC ni kitu kizuri kwa chama japo ukiwa unaangalia macho juu juu huwezi kulielewa hilo.Walikuwa kwenye forum ya chama chao na walikuwa wanajaribu kuangalia namna bora ya kukisafisha chama huku wakiwa hawaachi shimo watakalojitumbukiza wenyewe kama ambavyo akina ole sendeka na wengineo wanavyoelekea bila kujijua kukiangamiza chama chao.

Duu Kimyamana, Kwa mtazamo wako ni Chama mbele Taifa nyuma?

Yaani unaona sawa kuwatetea mafisadi ili kukinusuru chama kwa vile kimeshikwa na mafisadi?? vipi kuhusu mama yako Tanzania?

Hivi ni kweli Mafisadi ndo wametufikisha hapa? Comeon guys let's be serious! Huyu Serukamba has to come to his sense! Otherwise 'the dot com' generation will chase him out! Siyo habari za zidumu fikra za m/kiti na kidumu chama cha ..
 
Huyu ana kila dalili za UFISADI inawezekana tu hajapata nafasi. FISADI ni FISADI tu hata unamjua kwa matamshi yake.
 
another Shy? Ooh Sorry,kusimamia Anayoyasema Hatumkatazi Ila Ya Mantiki Yoyote Kwa Maslahi Ya Taifa?...mkuu Tuambie Mtazamo Wa Masafa Marefu Kwa Mheshimiwa Huyu?
Amechunguza Hakuona Mahali Ktk Uchunguzi Wa Mwakyembe Wakisema Kuwa Lowasa Alishauri Au Kushinikiza Kuwa Richmond Wapewe Hio Tenda,zaidi Ni Preamble Ambayo Haina Ushahidi Zaidi Ya Kudai Kwamba Wapo Walioongea Nje Ya Kiapo Kitu Ambacho Hakina Mantiki Ktk Tume Ya Uchunguzi.mtazamo Wa Msafa Marefu Ni Kuwa ,watu Watakaa Siku Moja Wakati Hawana Jazba Wala Chuki Binafsi Na Kuuchambua Mustakabari Mzima Wa Tukio Hili.watakuwa Objective And Not Subjective.hapo Ndipo Haki Itatendeka.
 
Hilo tunalijua nipale EL na kundi lake lote watakapopanada kwa pilato
 
Back
Top Bottom