Mheshimiwa Mwigulu Nchemba: Kuhusu Matrafiki Hawa, Toa Ufafanuzi Please...!

Shagiguku

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
406
225
Mheshimiwa mwigulu Lameck Nchemba, naomba unipe darasa kuhusu matrafiki hawa wa jeshi la polisi Mwanza. Matrafiki hawa wana kawaida ya kukaa ndani ya gari (Suzuki escudo au Toyota Collona). Na wanapokuwa ndani ya hizo gari huwa wana TOCHI ambayo huitumia kuvizia magari yanayoingia jijini Mwanza hasa nyakati za asubuhi wakati watanzania wanakwenda kwenye shughuli za ujenzi wa Taifa.

Trafiki hawa hubana kati ya eneo la daraja la mwananchi na eneo la kokoto kama mtu unatokea mataa ya Buzuruga kuingia mjini jijini Mwanza. Na kama wakikubahatisha wakakumulika na hiyo TOCHI yao na wakakukuta una SPIDI KILOMITA 51 KWA SAAA, basi ujue siku hiyo "watazaa' na weyeee! Maaaana watawataaarifu trafiki wenzao waliopo mbele eneo la polisi mabatini ili wakukamate kwenye eneo la pundamilia jilani kabisa na geti la kuingilia polisi line mabatini. Na kwa kawaida hawana cha mswalia mtume, hata kama utawaeleza kuwa hiyo spidi 1 iliyozidi ni bahati mbaya, utawaona mara moja hiyo asubuhi asubuhi wanakuandikia faini 30, 000/=

Kitu cha ajabu muda huo wa asubuhi kama unatoka katikati ya jiji kuelekea maeneo ya buzuruga, hata uwe na spidi ya 120kph wala hawatashughulika na weye.

Ikumbukwe kwamba barabara ya kutoka katikati ya jiji la Mwanza kuelekea Kisesa ilitanuliwa na kuwa njia tatu; ambapo wakati wa asubuhi watumiaji barabara hii wenye magari huruhusiwa kutumia njia 2 kuingia mjini, na jioni kuanzia saa 9 alasiri watumiaji wanaotoka katikati ya jiji huruhusiwa kutumia njia 2 zinazotoka. Pamoja na barabara hiyo kutanuliwa na kuwa HIGH WAY, bado rais JPM wakati huo akiwa waziri wa ujenzi alitujengea daraja la kuvuka barabara katika eneo la Mabatini Center.

Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, ishu yangu hapa siyo kukamatwa na trafiki (maana na wao wapo kazini). Ishu yangu mimi ni KUFUATA NA KUZINGATIA SHERIA ZA KUNIKAMATA.

Napenda nikuulize na unifahamishe mambo yafuatayo:

1. Kuanzia eneo la Nyakato-National hadi Mabatini jijini Mwanza, HAKUNA alama YOYOTE ya barabarani inayoelekeza uendeshe gari kwa spidi YOYOTE. Na utaratibu unatutaka wakati tunaendesha gari tuzingatie alama za barabarani. Hawa matrafiki wako ndugu Mwigulu, wakikukamata saaasaaa! na weye ukawaeleza kwamba hujaona alama yoyote inayokuzuia kwenda spidi yoyote, majibu yao huwa ni haya;- "KWANI WEYE CHUONI HUKUAMBIWA KWAMBA ENEO LA MAKAZI YA WATU UENDESHE SPIDI CHINI YA 50KPH.....?????"""

Ebooo! chuoni wanafundisha KUZINGATIA alama za barabarani, ambazo ki-msingi zinapaswa kuwepo barabarani. Na kama hazipo mimi hiyo hainihusu, hivo nitapaswa kuendesha kwa KUZINGATIA alama ninazoziona.

2. Kwa uelewa wangu [NA HAPA NDIPO HASA NINAPOKUOMBA UNIPE HILO DARASA WEYE UKIWA KAMA KIONGOZI WA HAWA MATRAFIKI WA MWANZA]. Kwa uelewa wangu ni kwamba, barabara YOYOTE inapoitwa HIGHWAY huwaga inamtaka dereva aendeshe gari lakwe kwa spidi isiyopungua 100KpH. Nenda kokote duniani, ingia pale Nairobi ndugu yangu Mwigulu barabara ya JOMO KENYATTA HIGH WAY, nenda pale Ghana barabara ya W. BUSH HIGH WAY, pitia pale South Africa Johannesburg barabara ya WALTER SISULU HIGH WAY (na barabara zote hizo kuu zina vivuko vya waenda kwa miguu "madaraja").

Sasa inakuwaje barabara ya NYERERE ROAD "highway" Mwanza, dereva akamatwe kwa kuendesha spidi tena isiyozidi hata 80 KpH....!!!????????? Tena pasipokuwa na alama YOYOTE inayomuelekeza aendeshe kwa spidi fulani....!!!???? kwa kweli Mheshimiwa Mwigulu nchemba (waziri) hiii siyo fair hata kidogo....!!!!

3. Hiyo asubuhi asubuhi wanapotuvizia na kutukamata kwa "makosa hewa" ya kuendesha spidi zaidi ya 50 kwenye ""HIGH WAY YA NYERERE" yenye daraja la wavuka kwa miguuu na isiyo na alama za kumzuia mtu kuendesha spidi yoyote, wanafikiria sisi tukatoe wapi pesa ya kuwapa kirahisi rahisi namna hiyo!!?? Ikizingatiwa kwamba ile BATANI aliyoikandamiza mheshimiwa NGOSHA bado hajairegeza hata kidogo, mambo yanazidi kuwa magumu kiuchumi, na hasa kwenye mwezi "DUME" wa Januari....!


OMBI: Mheshimiwa waziri wa mambo ya ndani (Mb), Ndugu Mwigulu Nchemba, nafahamu muda huuu unausoma huu uzi hapa JF huku ukikunja uso na sehemu zingine ukiachia ka-tabasamu kadogo. Tafadhari saaaana pamoja na mambo yoooote uliyonayo, pamoja na ubize wooooote ulionao katika kutimiza na kutekeleza shughuli zako ulizokabidhiwa na wanaNzengo wa Tanzania kuzifanya kwa niaba yao. Nakuomba upate muda uongeee na mkuu wa usalama barabarani mkoa wa Mwanza, ama uje weye kimya kimya jijini Mwanza kisha mimi ntakupakiza kwenye ka-starlet kangu asubuhi moja halafu NINYOOOOKE NA zaidi ya spidi 50kph kuanzia kwenye mataaaa ya Buzuruga hadi eneo la geti la police line Mabatini kwenye kivuko cha waenda kwa miguuu (pundamilia) kisha ushuhudie watakachotufanya hao vijana wako wa usalaaaama barabarani; weee njoooo tu kimya kimya Mwanza kama unavokujaga siku zingine ujioneee kwa macho yako!

Ahsante saaana.....!!!!!!!!!!!
MwanaNzengo Miye, Napenda kuwasilisha kwako Mheshimiwa waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba (Mb) kama ilivo hapo juuuu....!

Duuuuuh! ila kauzi karefupoo...!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar threads

Top Bottom