Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,371
Mh. Kesho ikiwa ni Alhamisi, tunaomba kupitia kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, ulize serikali kama mwezi huu serikali itato nyongeza ya mishahara kwa watumishi kama ilivyoahidi maana teyari kuna mkanganyiko kuhusu swala hilo.
Ikibidi pia beba na gazeti la HabariLeo lililomnukuu kigogo mmoja wa serikali aliedaiwa kusema utaratibu wa kupanda mishahara sasa hautategemea tena sheria ya kupanda madaraja kila baada ya miaka 3 bali itategemea utendaji kazi wa mtumishi.
Pia uitaka serikali ifafanua kama nyongeza hiyo itahusu watumishi wote au ni wale zaidi ya 59,000 tu na usisahau kuhoji kama watalipa malimbikizo.
Swali la nyongeza:
Kwakuwa mpaka sasa kuna taarifa zisizo rasimi mitandaoni na ambazo hazijakanushwa kuwa waliokuwa wamesitishiwa promotion ili kupisha zoezi la uhakiki, barua zao sasa zinatakiwa zionyeshe kuwa watakuwa promoted kuanzia tarehe mosi November mwaka huu na si vinginevyo,je mh.Waziri Mkuu hii ni kweli?
Wabunge wengine wa upinzani muulize nini kinaendelea kuhusu Bombadier maana Mwanasheria wa serikali tulieambiwa katuma Canada kushughulikia swala hilo hivi saaa yuko Bungeni na mumtake waziri mkuu athibitishe kuhusu majibu ya barua ya Waziri Mkuu wa Canada kwa Raisi.
Naamini haya yatakuwa maswali ya kisera na yatajibiwa.
Waheshimiwa mimi kama mwananchi nimewakumbusha tu ila ni namna gani maswali hayo mtayauliza nawaachia wenyewe.
Tunaomba mtuwakilishe vema hiyo kesho.