Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Enzi zile za utotoni ilikuwa ni jambo gumu sana kukutana na kijana amedhoofu, akiwa anatokwa udenda mtaani kwa sababu ya madawa ya kulevya.
Ilipofika miaka ya 90 mwanzoni nakumbuka kukatiza pale pembeni ya mahakama ya kisutu na kukuta kundi kubwa la vijana waliokamatwa nje ya nchi wakifanya biashara ya madawa ya kulevya.
Siku ile wapita njia tulikubali kupoteza zaidi ya saa nzima kuangalia jinsi vijana wale walivyokuwa wakipandishwa kwenye karandinga.
Hapo ndipo jamii ya Tanzania ilipopata mwanga mpana juu ya namna ambavyo vijana wengi wa nchi hii wanavyohangaika huko nje kutafuta fedha kwa udi na uvumba.
Miaka imesogea kwa kasi na tatizo limekuwa kubwa kulinganisha na jinsi lilivyochukuliwa miaka ile ya 90 mwanzoni.
Madhara ya madawa ya kulevya yanaoonekana wazi kabisa. Haihitajiki kazi ya ziada kuweza kuwaona mateja. Ni wadogo zetu, rafiki zetu pia. Mfano katika wanafunzi tuliomaliza wote shule ya msingi, wapo takriban saba ambao walifariki kwa sababu ya dawa hizo.
Anapojitokeza mkuu wa mkoa na kuamua kuvalia njuga suala hilo sio wa kukejeliwa. Tunapokejeli kifanyikacho kwa kuongelea masuala eti ya taratibu za watu kuitwa kitu cha polisi. Ni kama tunabariki uwepo wa janga hili, kwa kutumia vigezo vye kisomi.
Tunapoteza nguvu kazi kubwa, kwani vijana wanaotumia madawa haya wengi wao, wanafariki dunia kabla hata hawajafikisha miaka 30.
Huu ubinafsi wa kutazama personalities za watu na tukaziona ni muhimu kuliko madhara ya jamii kuwa na watumiaji wengi wa madawa ya kulevya, ni aina fulani ya laana ambayo haiwezi kutuacha salama.
Mheshimiwa Paul Makonda umeshayavulia maji nguo na huna budi kuyaoga. Kejeli ni nyingi na vijembe ni vingi, ndio hulka ya kitanzania kung'ang'ania katika vitu shallow na kuachana na mambo yenye maana maishani mwetu.
Mheshimiwa pambana uwezavyo, hii ni nafasi ya kuacha legacy.