Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 59
Mheshimwa Kikwete,
Kwa mujibu wa habari zinazodondoka hapa JF kuwa unakuja tena US kwa safari zako za kawaida. Kwa mikono miwili na heshima nyingi, wana JF wa USA tunakukaribisha tena kuja kula mbwa wa moto (hot dogs) na kucheza mpira wa kurushwa na kupigwa na gongo lenye umbo la kuchukiza (baseball).
Hongera pia kwa ziara ya Mama Kikwete hapa kwa mwaliko wa Mama Kichaka juu ya (on top of) mengine yooote. Pamoja na kuwa watu wa UK hawajui kwa nini umewatosa na kukwepa kuhudhuria mkutano wao ambao ulikosa maelezo thabiti hapa JF, mimi binafsi natoa shukurani kwa uamuzi wako wa kuja tena USA.
Nakushukuru kwa vile najua kabisa kuwa una taarifa zote kuwa yule mtu anayetuhumiwa kufanikisha wizi mkubwa kabisa wa BoT alikuwa anajificha hapa kwa muda fulani ili mafisadi wasimdito. Nakushukuru kwa vile najua kabisa kuwa una nia kabisa ya kujua nini kilitokea kwenye mapesa yote pale BoT ambayo kwa bahati mbaya au nzuri yalifanikisha kukuweka madarakani.
Kwa kujua hili na kwa vile naamini kuwa umebadili moyo na una nia ya kuomba msamaha kwa watanzania na kuhakikisha kuwa wezi wote wanakamatwa na kuwekwa lupango wanakostahili, nakupa juu (I holla you) kuwa ninajua kilichotokea kwa Balali na yale yote ambayo mafisadi wanajitahidi kwa kila njia kuyafunika huku ili watanzania wasiyajue kabisa.
Kwa haya yote, karibu tena USA ili tusaidiane kujua kwa undani zaidi kilichotokea kwenye mapesa yetu pale BoT. Karibu tena ili tusaidiane namna ya kudeal na huyo mwizi na mkoloni mwenye uraia wa utata ambaye ametokea kuwa swahiba wako - Rostam Azizi.
Karibu tena USA President Kikwete ili tukusaidie kujua yale yote yaliyotokea kwa Balali na mapesa ya walalahoi wa kitanzania na wale wakina mama na watoto wanaokufa kila siku kwa kukosa dawa na chakula bora huku mabilioni yakitumika kumlipa richmonduli!
Asante!