Mheshimiwa Kawambwa alikuwa anamaanisha kweli alichokuwa anakemea....!? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa Kawambwa alikuwa anamaanisha kweli alichokuwa anakemea....!?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by TUJITEGEMEE, Apr 11, 2011.

 1. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  Habel Chidawali,Dodoma= Gazeti la Mwananchi la 10/04/2011


  NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe, ameuomba uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), umpe vipindi ili aweze kutoa mchango wake katika kuboresha taaluma katika chuo hicho.

  Dk Mwakyembe alifanya hivyo juzi kufuatia ombi lililotolewa na Profesa Mark Mwandosya, la kuwataka wabunge na mawaziri wenye uwezo na nafasi ya kufundisha, wafanye hivyo.

  Mwandosya alimtaka Makamu Mkuu wa Udom, Profesa Idrisa Kikula kutumia nafasi ya wabunge wanapokuwa Dodoma kwa ajili ya vikao vyao, kuwaomba waende kufundisha, ili kupunguza pengo la wahadhiri.

  Waziri huyo alisema kwa upande wake, yuko tayari kufundisha katika chuo hicho.Kwa upande wake, Mwakyembe alisema na yeye yuko tayari na kuutaka uongozi wa chuo hicho umpangie vipindi na kwamba ataanza kufundisha Juni mwaka huu wakati Bunge la bajeti, ambapo alisema atakuwa Dodoma kwa muda mrefu.

  Dk Mwakyembe ambaye amekuwa akialikwa katika vyuo vikuu kadhaa duaniani kwa ajili ya kutoa mihadhara, ni mtalaamu aliyebobea katika sheria.

  Kulingana na maelezo yake, somo hilo ndilo atakalokuwa anafundisha Udom.Makamu Mkuu wa Udom Profesa Kikula, alimwagiza Mkuuu wa Idara ya Mafunzo katika Kitivo cha Sheria kuwasiliana mara moja na Dk Mwakyembe, ili kumpatia ratiba ya namna atakayofundisha.

  Kabla ya uteuzi wa nafasi ya Makamu wa rais mwaka jana, Dk Mohamed Bilali alikuwa akifundisha katika chuo hicho.Alikuwa anafundisha Fizikia na wanafunzi walikuwa wanamsifu kwa mbinu za ufundishaji.

  Kwa upande wake, Waziri wa Elimu na Mafunzoya Ufundi Dk Shukuru Kawambwa alikemea tabia ya wahadhiri wa vyuo mbalimbali nchini, kuhubiri mambo ya siasa vyuoni badala ya kufundisha.

  DkKawambwa alisema tabi hiyo imekuwa ikiota mizizi siku hadi siku baadhi ya wahadhili wamekuwa wakidiriki kufundisha hata kwa kutumia mifano ya EPA,Richmond na Dowans.


  Chanzo cha habari>>>>>Mwakyembe aomba akafundishe


  Binafsi, namshauri Mh. Kawambwa akanushe usemi wake vinginevyo nitaamini kuwa naye ni "KUPE"(mnyonyaji ) ambaye anataka watanzania waendelee kuwa wajinga.
   
 2. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Kwani kuna dhambi gani kutumia mifano inayoeleweka kwa urahisi na wengi wakati wa kufudisha? Kawambwa asilete upuuzi wa kuwapangia wahadhili namna ya kufundisha. Ndo maana wakati wa kampeni alikuwa anaomba kura kwa kupiga magoti mbele ya umati wa watu na picha kubwa ya bosi wake.
   
 3. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kama kweli Shukuru Kawambwa alisema hivyo basi haelewi maana ya mwalimu bora ambae akitaka kutoa mfano wa jinsi viongozi wa nchi walivyokosa maadili, kwanini asitumie mifani ya DOWANS,EPA NA RICHMOND pamoja na contract ya barabara ya MSATA -BAGAMOYO? Yote mifano hiyo inaonyesha [ grand corruption] jinsi viongozi wanavyoweka mbele maslahi binafsi na si uzalendo. Hakuna mifano mizuri current ambayo wanafunzi wanaweza kuelewa somo kama hiyo iliyotolewa hapo juu!!
   
 4. L

  Leliro Member

  #4
  Apr 11, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asingekuwa ccm ningeshangaaaaaaaaaaaaaaaaa lakini kwa sasa...
   
Loading...