Elections 2010 Mheshimiwa John Pombe Magufuli awe Rais wetu

Magufuli alitakiwa sasa awe gerezani Ukonga kwa uhujumu uchumi!Aliwapa nyumba za serikali ndugu zake zilizojengwa na Nyerere kwa mikono yake(Kuna picha maktaba zinaonyesha Nyerere akibeba mchanga kwenye karai kuwapa mafundi akijenga nyumba za Oysterbay)Magufuli ndiye waziri anaye ongoza kwa kuitia hasara serikali((Rejea uamuzi wake alipogoma kutii amri ya mahakama na kubomoa kituo cha mafuta-Mwanza)

Kwa mawazo haya, ni kweli kabisa kuwa sisi watanzania ni watu waajabu sana!
 
Nilisema hapa mchana jk ataweka historia ya kuifanya hccm kuwa historia...nikasema kama team lowassa wakifanya mambo yao tunayoyajua...membe akatizi top 3 ...kuna mtu kasema 100% membe raisi wa tz...nasema tena kama team lowassa wakifanya mambo yao ninayoyafahamu...mgombea wa uraisi kwa ticket ya ccm mwaka huu ni mwanamke...nasema tena pona ya ccm mwaka huu ni huruma ya team lowassa...lowassa anaweza asimwage mboga lakini wananchi watamwaga mboga na upinzani kama wakijipanga vzuri wanaingia magogoni...tusubiri tuone...
Wakina msoga wamemwaga mboga, na wazee matumaini wakamwaga ugali
 
Hafai, hajui kuanalyaise mambo,ana kalili tu,takwimu zake nyingi ni uongo! wabongo mfatilieni kwa ukaribu mtagundua ana mapungufu mengi tu.

Kiujumla Waafrika wote wana uwezo mdogo kiakili.Licha ya mapungufu yake,Magufuli ni afadhali mara mia zaidi ya Lowasa na Membe.Km si udenzi wa Wabongo,nadhani Muhongo ndo alikuwa anaweza jukumu hilo.
 
Endelea kuamini kupitia hii hapa:

1436642319519.jpg
 
Kwa mawazo haya, ni kweli kabisa kuwa sisi watanzania ni watu waajabu sana!

Watu wengine wanadhani mtendaji akıchukua hatua na watendewa wakachalenji hatua yake mahakamani basi yeye ndiye anachunguza na kwenda mahakani.Maswala hayo mengne yanakuwa ya DPP,POLICE NA AG.Idara zetu za kiuchunguzi na kimashtaka zina uwezo mdogo.Wamekuwa wakifail mambo mengi na sıo ıshu za magufuli tu.
 
Kwanza nadini ya CCM hawezi kukubarika kwa sababu wanajua kuwa atawasumgua kwa kutaka kwake sifa anaweza kufanya kitu cha ajabu bila hata ya kufikiria. Wanaojua vizuri mwanza watakumbuka vituko alivyofanya wakati wa uvunjaji wa kituo cha mafuta cha MOIL, alilazimisha kuvunja matokeo yake serikali iliwalipa pesa nyingi sana wale wahindi wa CCM! Kwa kupenda kujipendekeza JP alipongeza safari za raisi JK pamoja na kujua fika zinaliingiza taifa kwenye ghalama zisizo za lazima hii yote ni kwa sababu huyu mheshiwa anapenda sifa sana so alijipendekeza kwa JK kwa kumpa sifa zisizo na tija kwa watanzania of which watanzania sidhani kama tunahitaji raisi wa style hii. Kwa visasi ndo mwenyewe kumbukeni issue ya fast ferry za Azam alozileta lake Victoria, JP alitaka kumkomoa Mwandosya kwa vile alikuwa amekula karamu ya ujio wa meli hizo hivyo JP akajua kumkomoa ni kugoma kusaini boti hizo kupitishwa kwenye barabara zake kwa kisingizio ni nzito wakati kuna mitambo ya migodini ni mizito mara mbili ya boti hizo kila siku inapitishwa kwenye barabara zake na sisi watz tukishuhudia. Kwa kifupi JP hafai hata kidogo kuwa raisi, ikumbukwe tena aliwahi kupigiwa kelele na wananchi wa Buziku kwenye moja ya mikutano yake jimboni chato,alichokifanya ni kuwaambia kwa kisukuma " Buta baba gete mtalaibona ilami maisha ging'we pyee!" kilichotokea ni kuipindisha barabara ya lami ilotakiwa kupita Buziku akalazimisha ipite Chato ili kuwakomoa wananchi hao....sasa jamani tunamjadiri kuwa raisi wa nchi mtu wa aina hii? Labda kwa vile ni demokrasia acha tumuweke tena raisi wa majaribio kama tulivyofanya 2005 & 2010.

Hivi nyie ni watu wa aina gani mbona Hamna jema? ?? Kwenu kila mtu hafai jitokezeni basi nyie tuwachague au nyie marais wa nje ya fence? ??
 
Duuuuuuh…!!!! Tatu bora haina mgombea aliye haidi kupambana Dhidi ya ufisadi ulio kithiri na rushwa kubwa kubwa ndani na nje ya chama, #CC .
 
Mwenzenu napata taabu kidogo, sijui jinsi gani Mheshimiwa huyu ashawishiwe na kukubali ombi hili. Natamani sana John Pombe Magufuli awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama sio sasa kwa sababu za taratibu za CCM, basi zamu inayofuata.

Vyovyote iwavyo, naamini huyu bwana anafaa kila kona uwanjani anapocheza siasa. Hata PhD aliyoipata majuzi inaongezea chachandu tu, kwamba hatababaishwa na vyeti vya udaktari wa kupewa zawadi tu, maana anayo real one.

Sina uhusiano naye kabisa huyu mtu na wala sijawahi kukaa naye au kuonana karibu, lakini vitu vyake mwisho bwana. Naamini atachagua timu ya washauri inayofanana naye. Hata kama anayo mapungu yake kama binadamu, the good outways the bad, wakati mwingine analazimika kufanya vitu vingine kwa kuwatii wakubwa zake, lakini akishika rungu mwenyewe nashawishika (sidanganyiki) kwamba ataifaa Tanzania ya sasa.

Leka
Katika vitu nchi hii ilifanya makosa ni vitatu, cha kwanza azimio la arusha pili kumpitisha jpm, tatu wachangiaji kwenye uzi huu, kosa lao halitasahaulika milele
 
Najua JPM ni mchapakazi mzuri zaidi ya mawaziri wengine wengi kama siyo wote, ni mfuatiliaji mzuri wa watu wa chini yake, ana uwezo wa kujieleza, kujenga hoja na kizisimamia hata pale hoja hizo zinapokuwa na upinzani wa dhahiri - mfano ni uuzwaji wa nyumba za serikali.

Tatizo langu na huyu jamaa ni moja tu si msikilizaji mzuri na anaweza kuwa "dictator" mzuri sana hasa pale mitazamo na misimamo yake itakapokuwa kinyume na maslahi ya nchi - refer uuzwaji wa nyumba na ubadilishwaji wa ramani ya barabara kuu kupitia wilayani kwao. Wakati wa uuzwaji wa nyuma za serikali JPM alikuwa na majibu ya kejeli - kama ya bosi wake Mkapa - kwa wale wote waliokuwa wanahoji busara ya zoezi lile. Ni aina ya mtu ambaye anapenda kutumia hoja za nguvu badala ya nguvu ya hoja pale anapokabiliwa na wapinzani makini wanaohoji busara za maamuzi na matamshi yake.

Tatizo letu Tanzania ni la kimfumo zaidi kuliko kiongozi mmoja mmoja. Tuna mfumo ambao hauna vidhibiti mwendo kwa kiongozi mkuu kabisa wa nchi na wateule wake hasa pale wanapoamua kushirikiana kuifilisi nchi. Ninashawishika kuamini kuwa hata kama utamweka JPM kama mfumo ni huu huu wa kuwa na imperial president hakuna jambo la maana atakalofanya zaidi ya kujitwalia chake mapema. JPM katika mfumo wetu wa sasa hana tofauti na Benjamin William Mkapa.

Katika mfumo wa sasa nadhani JPM anaweza kuwa mtendaji mzuri akiwa waziri mkuu na apewe mamlaka kamili ya kuwasimamia na kuwawajibisha mawaziri wote.

Yote uliyosema yametimia
 
Back
Top Bottom