chitambikwa
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,941
- 900
plan c in not yet born
maana yake tunahoji uhalali wa mamlaka? Kwani hatujui?
Voiceofreason,
Nashukuru kwa maoni yako na ya wachangiaji wengine. Suala hili nitalitolea tamko rasmi. Hoja yako ilikuwa mwezi Agosti, wakati mpango wa dharura ndio ulikuwa kwenye hatua za awali za utekelezaji. Serikali ilihodhi usimamizi wa utekelezaji wa mpango husika na kiwango kikubwa iliachiwa Wizara ya Nishati na Madini. Nilitahadharisha kwamba kwa mfumo huo malengo yaliyotajwa bungeni hayatatimia kwa wakati. Sasa tuko mwezi Oktoba na malengo ya mwezi Septemba ya mpango wa dharura sehemu kubwa hayajafikiwa; tunapoelekea sio kuzuri kama hatutakuwa na Plan C kuanzia mwezi wa Oktoba/Novemba. Tuendelee kujadili na kuchukua hatua za haraka
JJ
Nimefurahi ulivyo jibu mheshimiwa lakini hali hii imekithiri na watu wanumia, shughuli za kiuchumi zinakwama kama hali itaendelea maana yake ni kwamba tutarudi nyuma kimaendeleo baada ya kusonga mbele. Mheshimiwa Mnyika serikali imeruhusu sekta binafsi kuinvest kwenye umeme, ombi langu kwakua ninyi mko mstari wa mbele kutetea maslahi yetu sisi wananchi huoni kua sasa ipo haja ya nyinyi wabunge kumua kutafta wawekezaji binafsi kuzalisha umeme?