Mheshimiwa JK hii ndiyo inaleta uvunjivu wa amani Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa JK hii ndiyo inaleta uvunjivu wa amani Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dopas, Mar 6, 2011.

 1. D

  Dopas JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wapendwa wanaJF tunakumbuka mojawapo ya jambo alilozungumzia mheshimiwa JKikwete katika hotuba yake ya mwisho wa Februari 2011 ni kuwa maandamano ya Chadema yanaleta uvunjivu wa amani Tanzania.

  Kwa waliosoma gazeti la mwananchi la jana moja ya taarifa ilikuwa "Wanafunzi wa darasa la pili na tatu wa shule ya Msingi Magwalasi katika Kata ya Rujewa, wilayani Mbarali, mkoani Mbeya wakiwa darasani wakiendelea na masomo kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa shule hapo imewalazimu chumba kimoja kutumiwa na wanafunzi wa madarasa mawili kwa kila darasa kugeukia upande wake" .

  Kwa walioona gazeti hilo, nadhani kuona picha ya wanafunzi hao kwanza utacheka, lakini pili lazima utawahurumia. Inakuwaje? Wataelewaje wanachofundishwa ukizingatia kuwa kila mwalimu katika chumba hicho kimoja anafundisha. Na wanafunzi wa madarasa hayo mawili katika chumba hicho kimoja lazima wamsikilize mwalimu husika na sio mwingine?

  Kwakweli ni masikitiko ya hali ya juu. Hivi mashangingi waliyopewa waheshimiwa wabunge, na mawaziri hivi karibuni: kila moja mil 90. Isingiwezekana kuwapunguzia adha hawa watoto wetu walau kila darasa ikawa na chumba chake?

  Naamini darasa 1 halizidi mil 15. Shangingi moja si lingejenga madarasa 6 au zaidi? Mbona nchi inakosa vipaumbele? Mbona hela za mashangingi zilipatikana haraka x idadi ya wabunge? Kwa nini hela ya kujenga vyumba vya madarasa ili walau wanafunzi wa kila darasa waingie chumba chao(kwa wakati moja bila kuchangia na darasa nyingine) haipatikani, isipokuwa mapambio ya hakuna hela? Hiyo ni kuwaelimisha au kuwachanganya watoto akili? Hivi hata hao walimu si watachanganyikiwa baada ya muda kwa fujo ya aina hiyo?

  Ningepata nafasi na Mheshimiwa Waziri mkuu Pinda ningekuwa na swali kwake.
  Juzi alipokuwa akihutubia Bukoba alisema kuwa Rais amekuwa mvumilivu, ila uvumilivu karibu utamshinda dhidi ya Chadema. Swali la kwanza kwa Pinda ni vipi kuhusu wimbo wa uhaba madarasa unaoimbwa kila mwaka haumkoseshi uvumilivu mheshimiwa Rais, hadi inafikia hatua ya watoto kugeuziana migongo? Je, ni lini mheshimiwa raisi uvumilivu kuhusu hilo utamshinda? Na mengine mengi ambayo yangepaswa kuwa vipaumbele lakini tunaamini hata hayafikiriwi?

  Ni kweli matatizo yalikuwepo tangu enzi za mababu, lakini nadhani ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu chumba kimoja cha darasa tumiwa na madarasa mawawili kwa wakati moja, kila mwalimu akifundishwa somo lake. Nadhani ni afadhali hata chini ya mti kwani watoto wanaweza kujifunza kwa utulivu.

  Ndiyo maana namwambia Mheshimiwa Jakaya Kikwete kuwa hii ndiyo italeta uvunjivu wa amani Tanzania muda sio mrefu ujao na wala sio maandamano ya Chadema.
   
 2. malkiory

  malkiory JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Priority kwa watawala wetu ni kufikiria anasa. Wanafikiria ujenzi wa jiji la Kigomboni wakati wafunzi hawana madawati. Ni mambo ya kusikitisha kwa kweli, bila hata kukosa aibu wanamwita Slaa Savimbi.
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  kingine wananchi wanataka mh uwe unajibu hoja sio ulalamike, then wanataka kuona uthubutu wako, fukuza mafisadi ktk chama cha babu, jaribu kuwa na meno, lasivyo utaishia kulalamika, kulaumu na kuhaha haha!
   
 4. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  japo kwa muda uliobaki jenga falsafa ya uongoz wako!
   
 5. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  kweli kabisa hizi ndo hoja za kushinda uvumilivu na siyo cdm tena kumeanza kujitokeza agenda mpya hapa baada ya kuona ile ya udini watu wameishtukia sasa ni chadema wanavuruga amani hivi tujiulize tanzania tuna amani au tuna utulivu amani ipi katika utitiri wa matatizo kila kukicha siku utulivu utakapoisha patachimbika!
   
Loading...