Mheshimiwa Godwin Gondwe unakaba kivuli hadi penati?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,548
108,858
Kaka si tayari umeshateuliwa kuwa Mheshimiwa huko Handeni na sasa umeshafikia kilele cha Mafanikio yako ya Kimaisha sasa mbona Kaka bado unaendelea tu kuwatangazia AIRTEL " matangazo " yao ya Redio?

Unaonaje labda na sasa ungewaachia na wengine nao " waokoteze okoteze " vijisenti huko AIRTEL kwa kufanya nao matangazo yao huku Wewe sasa ukipambana tu na Wana Handeni katika kuwaletea Maendeleo huku ukipambana kwa hali na mali kuwapunguzia Wachawi waliokithiri huko?

Kuna tangazo jipya limeanza kuruka leo leo la AIRTEL na Kaka naona bado umekomaa tu utadhani Beki anayekaba " kivuli " na " penati ".

Kaka acha hizo bhana ujue hata Mungu anakuona hivoooo.......!
 
Tangazo lilitengenezwa kabla hajawa mheshimiwa

Si kweli kwani nina uhakika wa kutosha kuwa alilifanya wikiendi hii iliyoisha. Kama ni Ndugu yako mwambie basi awaachie na " wanaochipukia " ili na Wao watoke kwani kiukweli " anawabania ". Kwa maadili ya Uongozi hili analolifanya Mheshimiwa Godwin Gondwe haliruhusiwi na halivumiliki pia.
 
Mshahara wa milioni tatu hauwezi kumtosha mtu watu wanayemuona Mungu mtu,kaulize wakurugenzi wanavyonuna wasipoandikwa kwenye madokezo
 
Kumbe tangazo tu

Nadhani huelewi impact ya hii kitu ethically. Katika nchi zinazojitambua na kuendelea nadhani hii ingekuwa ni " kashfa " ya aina yake na hapa nadhani inabidi tuombe msaada na Watu waliobobea katika Uongozi na Utawala ili watusaidie kujua imekaaje.
 
Mshahara wa milioni tatu hauwezi kumtosha mtu watu wanayemuona Mungu mtu,kaulize wakurugenzi wanavyonuna wasipoandikwa kwenye madokezo

Hivi kuna " mshahara " unaomtosha Mwanadamu? Jamani hebu tujaribu basi kujibu hoja kama Great Thinkers kweli.
 
Wivu wa kike huo. Muache apate hela, kwani Airtel hawakulijua hilo. Kama wamemfuata wafanya nae tangazo na wakaclose deal awaambie kuwa yeye ni mheshimiwa kwa hiyo hataki hela???

Tuache wivu bhnaaaa
 
Kaka si tayari umeshateuliwa kuwa Mheshimiwa huko Handeni na sasa umeshafikia kilele cha Mafanikio yako ya Kimaisha sasa mbona Kaka bado unaendelea tu kuwatangazia AIRTEL " matangazo " yao ya Redio?

Unaonaje labda na sasa ungewaachia na wengine nao " waokoteze okoteze " vijisenti huko AIRTEL kwa kufanya nao matangazo yao huku Wewe sasa ukipambana tu na Wana Handeni katika kuwaletea Maendeleo huku ukipambana kwa hali na mali kuwapunguzia Wachawi waliokithiri huko?

Kuna tangazo jipya limeanza kuruka leo leo la AIRTEL na Kaka naona bado umekomaa tu utadhani Beki anayekaba " kivuli " na " penati ".

Kaka acha hizo bhana ujue hata Mungu anakuona hivoooo.......!
Inawezekana lilitengenezwa kabla hajateuliwa
Inawezekana alishalamba mpunga kabla hajateuliwa
Ni vizuri pia akipata kazi kama hizi ili asitamani rushwa kwa kua kipato kitamtosha
 
Nadhani huelewi impact ya hii kitu ethically. Katika nchi zinazojitambua na kuendelea nadhani hii ingekuwa ni " kashfa " ya aina yake na hapa nadhani inabidi tuombe msaada na Watu waliobobea katika Uongozi na Utawala ili watusaidie kujua imekaaje.
Wewe unayeelewa, kachukue nafasi yake
 
Tena ukuu wa wilaya hauna vyanzo vya ndani,ukizingatia hela za matumizi ni za kusuasua.Lazima ofisini yake itakuwa imekauka sana acha akipige kazi zingine kuongeza kipato.
 
Back
Top Bottom