''MHESHIMIWA DOCTOR rais''......!vp wazee inaendana na alikoifikisha nchi sasa?

Mbona hata Mkapa anayo ya heshima na mkewe pia, lakini hatujawahi kusikia anaitwa Dk.... Ni aibu kujipendekeza kiasi hicho
 
The Prezidaa wasn't sure of being called DR even in jokes situations, so when this happened was like rain in the desert....He knows the truth that Upstairs he doesnt worth the name
 
SAWA MIMI SIO MWANASIASA ,.Vyuo vikuu vina Mathamanisho yake,..ya kiheshima either unaufuata MTAALA na unatunukiwa heshima baada ya kuumaliza, au Uthamanisho wa heshima unakufuata kutokana na mchango wako katika jamii,.ile vita ya kenya kwenye na baada ya Uchaguzi iliuwa si Ndogo,.wenyewe wanaelewa,..
publications mzee ni muhimu zinaweza kukugusa indirectly kutokana na uliyoyafanya ambayo yanaweza kutumika kama hadidu sehemu nyingine .,hiyo pia ni publication,.na inakubalika,.
mimi sio mwanasiasa ..
SUALA LA MAPROFESA hebu tuliangalie.,.ningependa tuzungumzie wa TANZANIA upande wa tiba[madaktari] NI VIPI WAMEWEZA KUWA MAPROFESA BILA KUWA NA PhD,..kwa walio wengi ninaowajua hawana Phd,.. Hawajawahi kuwa maasosiate PROF,..Lakini wanatambulika hivyo wakati ki mtaala haiko hivyo,.neno kubwa ni kupablish kupablish,.ameshapablish.,.. teaching staff,..teaching hours amefikisha point,.ni nani mwenye kuwahakiki?
Kwa huku tulipo ili upate masters DEGREE lazima upablish angalau pepa moja yenye mahusiano na tafiti yako ,.lasivyo humalizi shule,.na kama una uwezo basi zaidi ya hapo[motisha pia hutolewa kwa kila pepa inayotoka],
KWA watu wa PhD pepa moja yenye mahusiano na tafiti yako tena lazima itoke SIC journal ,la sivyo humalizi shule,..je baada ya kufanya hivyo nikirudi bongo nitaitwa prof,.
lakini mbona wale wa BONGO wanaitwa maprofesa???
Basi ujue lazima kuna system ya vyuo vikuu ambayo imekubaliana na hali hiyo.,.ingawa wakija maprofesa toka nje majamaa huona noma na kujiita madockta.,lakini heshima ni heshima tu mzee ni kama tuzo ya NOBELI.,WANAKUBALIKA,.Ndio System ya dunia WAMEPEWA HAO TUZO YA KIDAKTARI,huna budi kukubali

Ndugu Bawa kama umefuatilia thread hii ( kitu ambacho nina uhakika maana umetoa mchango mzuri tu) hakuna anayepinga JK kupewa hiyo heshima ila tatizo ni ule ulimbukeni wake wa kuitumia kana kwamba aliisomea! kuhusu sentensi zilizo katika wino mwekundu, napenda tu nami kuchangia mawazo yangu. Una ushahidi gani kuwa ma Profesa wa tiba ya afya hapa TZ hawana PhD? ni kweli kuwa ili uwe Prof ni lazima uwe na PhD na hiyo ipo hata kwa Medical Doctors, na ni kweli kuwa lazima wawe na publication, kuhusu la ulazima wa kuwa na teaching point hilo sio lazima sana kwa non- teaching institutions, ingawa kwa hapa TZ ma Prof hawa wa tiba wanatoka katika taasisi ambazo pia zina vyuo vya kufundisha, so wanapata pia teaching point, na point hizi uhakikiwa na mabaraza ya vyuo vyao na ndio yenye majukumu ya kuwapandisha daraja, na kwa taarifa zaidi vyuo hivi huwa vina utaratibu wa kupanda haya madaraja na utaratibu huu uko kwenye documents zinaitwa " UP THE LADDER". Kuhus kupata masters degree sio tu huko mlipo, mtu hupata shahada hiyo baada ya kutoa publish paper, hata hapa TZ huwezi pata masters degree bila ya kutoa andiko la mradi wako au utafiti wako, na andiko hilo ni either liwe Thesis ( sijui kiswahili chake) au iwe ni Dissetation, ni ki ukweli hata undergraduate degree mtu huipati hata TZ hadi umeandika special project! na kwa PhD ni hivyo hivyo kama Masters japo kwa PhD andiko ni lazima liwe detailed! kuhusu wewe kuandika paper huko ulipo na eti ukirudi huku utaitwa Prof, sahau sio rahisi kiasi hicho, kuna point zinatakiwa ziwe accumulatated ili uwezo kufikia kiwango cha kuitwa Prof. na mwisho madai yako eti ma prof huku huwa wanabadilika na kujiita madaktari pindi wajapo ma prof kutoka nje! ni meshangaa sana, una ushahidi na hili, nikueleze tu ndugu " once you are a Professor always a Professor go East, go West, go North go South"!
 
Una ushahidi gani kuwa ma Profesa wa tiba ya afya hapa TZ hawana PhD?
Kuhus kupata masters degree sio tu huko mlipo, mtu hupata shahada hiyo baada ya kutoa publish paper, hata hapa TZ huwezi pata masters degree bila ya kutoa andiko la mradi wako au utafiti wako,??????

ni kweli kuwa ili uwe Prof ni lazima uwe na PhD na hiyo ipo hata kwa Medical Doctors, na ni kweli kuwa lazima wawe na publication,

MD bongo hIyo?au MD unayomaananisha ipi?Masters degree au Medical doctor Mbb...,DdSSS...,

NILIKUWA daktari MUHIMBILI NA niliwahi kuwa mwalimu pia wewe,.sijui unazungumza nini,..nimemgusa mzee wako nini,.wewe kwa kukusoma hauko kwenye fani ya medicine ,...sijui yaani tulia kabisa.,..Upladeer

Kuhus kupata masters degree sio tu huko mlipo, mtu hupata shahada hiyo baada ya kutoa publish paper, hata hapa TZ huwezi pata masters degree bila ya kutoa andiko la mradi wako au utafiti wako, na andiko hilo ni either liwe Thesis ( sijui kiswahili chake) au iwe ni Dissetation, ni ki ukweli hata undergraduate degree mtu huipati hata TZ hadi umeandika special project! ???????????na kwa PhD ni hivyo hivyo kama .//////?......
We mtoto kaa kimya kabisa,.SIJUI Huko uliko unafanya nini kama upo bongo BASI ndio nchi imeisha kabisa andiko la mradi wako au utafiti wako,
jifunze leo mpaka mwisho wa maisha yako wewe.//ANDIKO LA MRADI HUITWA Proposal na hata benki unavyoomba mkopo wa kibiashara unatakiwa kuandika hiyo ?lol hata hiyo pia hujui ,.unatetea nini.,,,tofautisha photocopy na kupablishi au machapisho ,......

na andiko hilo ni either liwe Thesis ( sijui kiswahili chake) au iwe ni Dissetation
Thesis,..hujui hata maana yake ,..Wellcome to JF..we will change you
 
Kuna katabia ka vyombo vya vya habari "vya umma" nikimaanisha TBC1 na vikaragosi vyake kumtaja kikwete wakianza na Doctor, hiyo PhD jamaa aliipata wapi? ninavyojua Phd za heshima hatuzianzi kama prefix au nimekosea?

Au anataka kubalance na Dr Slaa?
 
Hata TCU walishawahi kutoa press release juu ya hii na kuwakemea wote wanaowaita wale wenye digrii fake pamoja na za heshima kama ma dokta.... kukubali kuitwa dokta wakati siyo dokta ni ujuha!
 
Kwani slaa ni daktari wa nini ? Si ni wa biblia ? Hata degree yake ya mwanzo ni ya biblia !!!! Na phd yake ni ya canon law...yaani sheria za kikatoliki......sasa yupi bora ?
Musichanganye mambo......kikwete ametunukiwa phd kama 4 ...na anastahiki kwani ni mbinifu.....na ccm ni institition kubwa its like goverment within......sio famila ya wana moshi

mnampandisha slaa kwenye net na tanzania daima....lakini ukweli ni kwamba uwezo wake na mkakati wake hauwezi kufikia wa mrema na nccr mageuzi....mrema alikua real tishio ..na timu yake ilikua ni ya watu makini kutoka nchi nzima lakini mwalimu aliwashauri wacahane na urais kwani walikua bado...wakakata..
Chagueni vizuri sio ushabiki....tukumbuke maneno ya nyerere aliposema hawezi kwenda butiama kulala na kuicha nchi yake kwa d...s alitumia neno zito kuonesha namna gani nchi inge sambaratika kama wapinzania hasa mrema angechukua nchi..
 
Kuitwa Daktari bilaa kudefend theses ni sawa na kuvaa tai bila shati. Haina maana yoyote kitaaluma!
 
anastahili kuitwa Dr. kwani ametunukiwa PhD toka Kenyata University na vyuo vingine kama juzi hapa alipoenda Uturuki, na kama Kenyata inatambuliwa na TCU tatizo ni nini??

sababu za Kenyata kumpa wanasema ni "from the role in reuniting and restoring peace in Kenya after the post-election violence - and for the individual achievements and contribution to the welfare of humanity." copied

vyuo vina taratibu tofauti za kutoa PhD inakuwa vibaya kama ni ya kufoji
 
Ni kweli anastaili kuitwa na kuwa docta
1. Amefanikiwa kuwajua mafisadi wa tra na pale bandarini na kuwachukulia hatua kali ambazo hata wewe unazijua
2. Amewafunga watu kibao kutokana na ufisadi wakiwemo lowasa na rostamu
3. Ameweza kurudisha pesa zilizoibwa na mafisadi kiasi cha tsh..........ambazo ziliingizwa kwenye account...............na zimetumika kwa ajili ya .........
4. Ameweza kutumia madaraka yake vyema kabisa kwa kuwasamehe wale wezi wote waliorudisha pesa zetu tajwa hapo juu

----huyu ndiye doctor tunayemuhitaji------
 
Hujawaelewa, ni mganga wa kienyeji na mafunzo kayapata kwa shehe yahaya heseni
kuna katabia ka vyombo vya vya habari "vya umma" nikimaanisha tbc1 na vikaragosi vyake kumtaja kikwete wakianza na doctor, hiyo phd jamaa aliipata wapi? Ninavyojua phd za heshima hatuzianzi kama prefix au nimekosea?

Au anataka kubalance na dr slaa?
 
anastahili kuitwa Dr. kwani ametunukiwa PhD toka Kenyata University na vyuo vingine kama juzi hapa alipoenda Uturuki, na kama Kenyata inatambuliwa na TCU tatizo ni nini??

sababu za Kenyata kumpa wanasema ni "from the role in reuniting and restoring peace in Kenya after the post-election violence - and for the individual achievements and contribution to the welfare of humanity." copied

vyuo vina taratibu tofauti za kutoa PhD inakuwa vibaya kama ni ya kufoji

DEGREE YA HESHIMA INATAMBULIKA HALI KADHALIKA PhD YA HESHIMA....NI MTU MWENYEWE AKATAE KUITWA HIVYO KAMA ALIVYOKATAA Dr. B W MKAPA KUITWA MTUKUFU RAIS
 
Dk Manyaunyau, Dk Mtimkavu Dk Maji Marefu Dk JK Dk L. Abdalah mchambuzi wa soka..................nk.
 
Ndugu zangu najiuliza, hivi kweli kikwete ni mwanauchumi? kweli mikataba kama ile ya reli aliisoma kwa kisomo chake au ndo nini?

Muhuni huyu jamaa? hana uwezo wa kufikiria au ni uzalendo umetoweka? najiuliza ni mtu gani asiyeona jinsi tunateseka? asome kitabnu cha

Nyerere cha our leadership and the destiny of Tanzania. The fake president ''Mr Kikwete''
 

DEGREE YA HESHIMA INATAMBULIKA HALI KADHALIKA PhD YA HESHIMA....NI MTU MWENYEWE AKATAE KUITWA HIVYO KAMA ALIVYOKATAA Dr. B W MKAPA KUITWA MTUKUFU RAIS

Ni kweli Jk daktari tena bingwa. Nimesoma kwenye kampeni zake ame prescribe wajawazito wapewe bajaji kwenye barabara zenye makorongo
 
Kwani slaa ni daktari wa nini ? Si ni wa biblia ? Hata degree yake ya mwanzo ni ya biblia !!!! Na phd yake ni ya canon law...yaani sheria za kikatoliki......sasa yupi bora ?
Musichanganye mambo......kikwete ametunukiwa phd kama 4 ...na anastahiki kwani ni mbinifu.....na ccm ni institition kubwa its like goverment within......sio famila ya wana moshi

mnampandisha slaa kwenye net na tanzania daima....lakini ukweli ni kwamba uwezo wake na mkakati wake hauwezi kufikia wa mrema na nccr mageuzi....mrema alikua real tishio ..na timu yake ilikua ni ya watu makini kutoka nchi nzima lakini mwalimu aliwashauri wacahane na urais kwani walikua bado...wakakata..
Chagueni vizuri sio ushabiki....tukumbuke maneno ya nyerere aliposema hawezi kwenda butiama kulala na kuicha nchi yake kwa d...s alitumia neno zito kuonesha namna gani nchi inge sambaratika kama wapinzania hasa mrema angechukua nchi..


Bah! Sasa Mrema anaingiaje hapa? Tujadili hoja bila jazba na chuki binafsi. Hoja ni kwamba hizi PhD za heshima zinaweza kumfanya mtu aitwe dokta fulani? Nakumbuka akina Nyerere, Mkapa na hata Mama Mkapa walitunukiwa hizi na vyuo mbalimbali, lakini kwa kutambua kuwa wao sio wasomi wa level ya PhD kamwe hawakujiita Dr Nyerere au Dr Mkapa. Sasa huyu Mkwere kaona hiyo ni dili na ninaambiwa kawatuma wapambe wake wahakikishe kuwa jina lake linatanguliwa na Dr... hasa kwenye vyombo vya habari vya kifisadi kama TBC. Huu ni uchovu! Halafu huwezi kumlinganisha Dr Slaa na huyo mchovu wenu kwani anamuacha kwa mbali sana! Kwani hujui kwa nini anaogopa mdahalo?
 
Wakuu nahitaji msaada maana nimechoka kutapika kila ninaposikia Kikwete anatajwa kama Dokta.

Ninavyojua mimi kama ni honorary hata Marais waliotangulia walikuwa nazo na hakuna hata mmoja alijiita dokta.

Kwa wagombea urais wa sasa tunajua kabisa kuwa Profesa Lipumba wa CUF ni Phd Holder na Dr. Slaa wa CHADEMA naye ni Phd holder. Huyu JK sasa huu udokta wake ni wa kitu gani????

Amebobea kwenye taaluma gani???
 
Back
Top Bottom