''MHESHIMIWA DOCTOR rais''......!vp wazee inaendana na alikoifikisha nchi sasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

''MHESHIMIWA DOCTOR rais''......!vp wazee inaendana na alikoifikisha nchi sasa?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Teamo, Aug 10, 2009.

 1. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mimi nakwazika kidogo!naona nadharia zimekuwa mingi sana kuliko ''hali-halisi nchini kwetu''

  sina wa kumlaumu,wala kumlilia!Ninaililia nafsi yangu,ninaulilia umaskini wangu.

  Ndani ya miaka mitatu,tayari wapo waliomtunuku tuzo hii ya heshima,ya udaktari,naona vyombo vya habari tayari walishaanza kuandika jina lake kwa staili hiyo ya ''mh dk rais nanihii''.

  tunaolia mtuache tulie tu kasababu bado ahadi nyingi hazijatekelezwa.....!

  tunaomba sana ''mh dk rais '' uushikilie msemo ufuatao,kinyume na hilo ''I AM AFRAID I WON'T MISS YOU''..............''WALK THE TALK-BJ''
   
 2. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Jamani tusaidiane; Dr. ya Kikwete inamaanisha Daktari wa Falsafa yaani PhD (Alisoma wapi na lini?), Daktari wa binadamu au Daktari wa wanyama? Lakini kumbukumbu zangu zinaonyesha alisoma uchumi UDSM? Sasa huu Udokta uliogain popularity kubwa kiasi hiki ni Udokta gani huo? Maana kama ni hizi PhD za heshima, nakumbuka Mkapa pia alikuwa nazo kadhaa, hata Nyerere aliwahi kupewa, cha ajabu hawakuwahi kuitwa hivyo.
  Shida ipo kwa waitaji (wanaomwita Doctor) au ipo kwa muitwaji (anapenda kuitwa Doctor).
   
 3. M

  Mutu JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hahahaaaaaaaaaaaaaaa si alipewa Chuo kikuu cha Kenya umesahau ,ni hizi za heshima na kutambua mchango fulani.Sio za uganga wa viumbea hai wala si msongamano wa degree.
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mmmh, sasa hizo si wanapewa wengi tu, mbona yeye yake inavuma kupita kawaida? Hadi kwenye mbao za ufunguzi wa majengo au shughuli fulani za kitaifa anaandikwa Dr. Sasa hii siitaleta shida baadaye kwa vizazi vijavyo watakapokuwa wanaona document zimeandikwa Dr au mbao za ufunguzi wa majengo zimeandikwa Dr, watajua Tanzania iliwahi kuongozwa na PhD holder. Confusion!!
  Lakini pia PhD za hivyo Mkapa anazo kama tatu hivi na hakuwahi kuitwa Dr. Inasemekena Rais wa India kwa mfano, ni Professor lakini hata siku moja haitwi Prof. nk nk nk. Hii kitu inanipa shida kidogo.....
   
 5. M

  Mutu JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tatizo rais wako si mkwere au hujui inawezekana ana engineer mwenyewe iandikwe hivyo ,maana dr za namna hizo wengi wanazo ila hawaoni hekima kutumia...Nyerere alikuwa nazo ila huoni kutumika .
   
 6. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 362
  Trophy Points: 180
  Huo ni ulimbukeni wake tu! Nyerere alikuwa nazo kama 12 hivi! Siku wakizihitaji sijui tutaanza kufuta hayo majengo yaliyoandikwa Dr. Mgabe wamechukua karibia zote!
   
 7. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Lakini kwa kweli hapa kuna issue ya kuzingatiwa, maana udaktari wa namna hii huweza kuwa revoked. Sasa kama initials zimeenda kwenye mabango yaliyo permanent hapo itakuwa kasheshe.

  Btw, nadhani kuna thread imeshaliongelea hili swala kwa kirefu sana tu, itakuwa vyema kama thread hii inaunganishwa na ile (wazo tu).
   
 8. K

  Kilamia Member

  #8
  Jul 2, 2010
  Joined: Jul 9, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Nami nichangie kuhusu hili. Rais wetu anaonekana kama limbukeni fulani hivi. Haiwezekani kama watu wako wanataka kujikweza kwako kwa kukuita Dr na wewe unakubali tu. Nina hakika akitoa maelekezo kwa wasaidizi wake basi watu hawatamuita tena namna hiyo. Inanitia kichefuchefu kwa sababu Rais wetu anaonekana kilaza kwa kutumia na kuachia wenzake watumie initials za Dr kwenye jina lake kila mara anapotajwa wakati u Dr wenyewe ni wa heshima tu.
   
 9. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huyo iliyobaki kwake ni "MIX WITH YOURS"
   
 10. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  MWALIMU NYERERE BAADA YA UHURU ALIKUWA ANAJULIKANA KAMA Dr.Nyerere kote duniani,..mpaka baadaye,..sijui ilikuwaje akaanza kuitwa mwalimu,..au mwenyekiti .,.na Watanzania wote tukawa tunaitwa ndugu,.kulikuwa hakuna mtu anayeitwa mheshimiwa au mtukufu sio waziri hata mbunge.,..
  kwa urusi wakati wa Ukomunisti raia wote walikuwa wanajulikana kama [matavarishi],kama ulikuwa na ushiriki kwenye chama pamoja na nafasi bosi wewe ni COMREDI,.
  system duniani imebadilika ,..sasa ni MTUKUFU ,.mheshimiwa,..Hamana COMRADE wala NDUGU,..
  ndio dunia hiyo,..KAPEWA heshima ya kuwa DK.,.na akainama KAMBA ya KOFIA ikabadilishiwa upande ,.ina maana alikubali hiyo heshima ,.sasa tatizo ni nini?
  MIMI ni muumini WA NYERERE Mpaka MWISHO,...YOU DONT LOOK FOR Respect but you earn it.//na ukiipata basi ikubali.,.na huna budi kuitunza hiyo heshima mpaka mwisho.,..
   
 11. b

  blackpepper JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 382
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Dr.Kikwete mmmmmmh
   
 12. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hizi ni PHD za public and economic administration. Ughaibuni nimeziona hata digrii za primary education. shule za msingi. Sijui kama kwetu tunazo au labda ni ulimbukeni wangu.
   
 13. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Kuna heshima na heshima. Wakati nchi nyingi za Kiafrika zinapata uhuru miaka ya 1960 Waingereza waliwapachika viongozi wengi waliokuwa wanawaachia madaraka UDOKTA. Kulikuwa na Dr. Nyerere, Dr. Obote, Dr. Kaunda, n.k. Hii ilikuwa ni fix ya kuwalainisha kwa kuwavika vilemba vya ukoka ili waendelee kuwa watiifu kwao. Baada ya muda viongozi wenyewe walibaini hilo na kuacha kutumia hizo heshima bandia. Kwa Mwalimu Nyerere alikwenda mbali zaidi na kuzuia kuitwa mheshimiwa au mtukufu na badala yake akapendekeza NDUGU. Mwalimu ilikuwa profession yake. Hizi DOKTA zinazosakwa na wanasiasa wetu sasa ni ulimbukeni tu. Hata ambao hawakuwahi kukaa darasani zaidi ya miaka 8 nao sasa ni madokta. Inashusha heshima ya madokata wakweli kwa sababu haitakuwa rahisi kubaini wa kweli na feki. Angalao mtu angekuwa anaonyesha dalili za u-intellectual kidogo labda tungemezea lakini wengine mmmhhhh! Hivi nani aliwahi kuona andiko lolote la Kikwete, iwe makala gazetini, mchango katika jarida au kitabu? Nani amewahi kuona andiko lolote la Karume? Lakini sasa ni madaktari!!!!!!! Kuna na wale ambao wameshtumiwa kughushi shahada na wao hawakukanusha tuhuma hizo lakini bado watu (hata waandishi wa habari na vyombo vyao) wanaendelea kuwaita MaDOKTA. Hivi kunyamaza si ushahidi tosha kuwa mtu amekubali tutuhuma? Tunapokuwa na marais au viongozi wa sampuli za kina Dr au Professor Maji Marefu kwa kweli ni tatizo kubwa. Labda itatusaidia katika Soko la Pamoja la Afrika Mashariki. Na sisi tutaonekana tumo ingawa hatuvumi.
   
 14. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwakweli hapo kwenye nyekundu ni changamoto. Nimeshangaa hata kwenye press release ya wahadhiri wa chuo kikuu na wenyewe wamemtaja kama Dr. Kikwete. Kuna haja ya kureview matumizi ya hili neno ili ijulikana linatumikaje na kwa maana gani. Kama vipi vyuo vikuu viache kutoa degree za aina hiii, bali zije na kitu kingine cha tofauti kitakachoonyesha kwamba ni heshima aliyopewa mtu na si kumwita Doctor ilihali hata hajui hiyo Dr. inasotewaje? Wafanye kama Malkia ambaye huwa anatoa "Sir". Sasa hivi layman hawezi jua tofauti ya Udokta wa Kikwete na wa Magufuli. Wakati in reality ni za mbali kama mbingu na nchi.
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Jul 2, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mtaani huwa twaziita sifa za kijinga,personally anajua yeye kilaza PHD ya darasani hawezi kuifikia kwa nini asijikweze?
  Tena inawezekana yeye mwenyewe ametaka aitwe ivyo wakwere kwa kupenda sifa ...............ila ni jadi yao
   
 16. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,992
  Likes Received: 3,741
  Trophy Points: 280
  Dr Kikwete = Dr Remmy Ongala = Dr Ricky Abdallah = Dr (no prof) Maji Marefu = Dr M-mbabe (namiye wamo!!)
   
 17. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Yaani Kikwete anapenda mno kuitwa Dk!!! anaona kawa mtu wa maana mno!
  Wewe mwangalie usoni siku akitambulishwa kama kama dokta, ndevu zoote zinahamia kwenye shavu kwa tabasamu!!
   
 18. b

  bob giza JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mandela anazo hizo za kumwaga..nyiingi balaa lakini no way hata siku moja kajiita dr. Mandela au hata vyombo vya habari kumwita hivyo..
  Hapa bongo both mkwere na vyombo vyake vya habari wana problem.kwamba mkwere anapenda kuitwa hivyo na ndo maana kauchuna tuu, kwasababu angekuwa hataki kuitwa hivyo si angekataa tuu, mkapa alishawaambia waandishi waache kumwita mtukufu alipoingia tu madarakani na wakauchunaa..lakini pia vyombo vya habari hasa itv na tbc utaona kwenye subtitles zao wanaandika, raisi wa sijui nini nini, dr. Jakaya kikwete,.. Wanajikombeleza kwake....unafiki na kujikomba komba ndo tabia yetu..utatuua bongo...
  Sasa wote mkwere na vyombo vya habari hawawezi kuona mifano ya watu wa maana wenye hizo degree za heshima ambao hawajazitumia, wangejifunza kwa hilo kwa kujiuliza mbona nyerere, mandela n.k hawajawahi kujiita hivyo,..then wangepata jibu... Na naamini kuna viongozi wengi tu wa kenya uganda, rwanda n.k wanazo hizo..nadhani hata mu7 anayo hiyo si ndiyo?? Au?? Au!!
  Mkwere bwanaaa!!lakini jamani mkwere vitu vya kujidaia ni vichache so ndo maana hata kitu kama u-dr wa heshima kwake ni dili..mtu kama nyerere kujiita dr. Kwa degree ya heshima kwake nadhani ulikuwa kama mzaha fulani ivi..mbayuwayu bwana!!
   
 19. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sifa za kijinga zinanikera sana mimi zinanibore sana mimi sifa za kijinga! si anataka aonekana kama msomi na yeye wakati aliondoka na gentleman degree pale UDSM miaka ya 1970! angalia watu kama Barrack Obama, huyu jamaa ni PhD holder infact in Professor, lakini aaaah wapi husikii hata mara moja akitwa Dr au Prof Obama! kwa sababu anajua title hiyo sio kipimo cha credibility yake. Lakini kwa imberciles, especially wanapokuwa viongozi hudhani title hizo ndio kipimo cha uelewa wao, kwa ufanyaji kazi wa JK na Uongozi wake, ana aibisha hata hiyo title yenyewe, na kama sio UNAFIKI tu hata WAKENYA waliompa hiyo heshima ya udaktari wanafikiri mara mbili kama walikuwa sahihi au la!
   
 20. B

  Bawa mwamba JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 351
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  SAWA MIMI SIO MWANASIASA ,.Vyuo vikuu vina Mathamanisho yake,..ya kiheshima either unaufuata MTAALA na unatunukiwa heshima baada ya kuumaliza, au Uthamanisho wa heshima unakufuata kutokana na mchango wako katika jamii,.ile vita ya kenya kwenye na baada ya Uchaguzi iliuwa si Ndogo,.wenyewe wanaelewa,..
  publications mzee ni muhimu zinaweza kukugusa indirectly kutokana na uliyoyafanya ambayo yanaweza kutumika kama hadidu sehemu nyingine .,hiyo pia ni publication,.na inakubalika,.
  mimi sio mwanasiasa ..
  SUALA LA MAPROFESA hebu tuliangalie.,.ningependa tuzungumzie wa TANZANIA upande wa tiba[madaktari] NI VIPI WAMEWEZA KUWA MAPROFESA BILA KUWA NA PhD,..kwa walio wengi ninaowajua hawana Phd,.. Hawajawahi kuwa maasosiate PROF,..Lakini wanatambulika hivyo wakati ki mtaala haiko hivyo,.neno kubwa ni kupablish kupablish,.ameshapablish.,.. teaching staff,..teaching hours amefikisha point,.ni nani mwenye kuwahakiki?
  Kwa huku tulipo ili upate masters DEGREE lazima upablish angalau pepa moja yenye mahusiano na tafiti yako ,.lasivyo humalizi shule,.na kama una uwezo basi zaidi ya hapo[motisha pia hutolewa kwa kila pepa inayotoka], KWA watu wa PhD pepa moja yenye mahusiano na tafiti yako tena lazima itoke SIC journal ,la sivyo humalizi shule,..je baada ya kufanya hivyo nikirudi bongo nitaitwa prof,.
  lakini mbona wale wa BONGO wanaitwa maprofesa???
  Basi ujue lazima kuna system ya vyuo vikuu ambayo imekubaliana na hali hiyo.,.ingawa wakija maprofesa toka nje majamaa huona noma na kujiita madockta.,lakini heshima ni heshima tu mzee ni kama tuzo ya NOBELI.,WANAKUBALIKA,.Ndio System ya dunia WAMEPEWA HAO TUZO YA KIDAKTARI,huna budi kukubali
   
Loading...