Mheshimiwa Chenge, ona aibu, bwawa hili la Ning'wa linakidhi mahitaji yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mheshimiwa Chenge, ona aibu, bwawa hili la Ning'wa linakidhi mahitaji yetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, May 24, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mnyonge mnyongeni lakini haki zake mpeni,maneno haya ya hekima yamekuwa yakitumiwa sana na wahenga angalau kuthibitisha huruma kwa mnyonge hasa anapo dhulumiwa haki yake.Leo hii maneno haya yadhihakiwa na kupotoshwa maana yake kutokana na wanyonge kunyanayaswa na haki zaoza msingi kuhujumiwa na kama si kunyimwa kabisa.

  Kwa wale wakazi wa manispaa ya Shinyanga wanatambua shida kubwa inayowakabili wakazi wa manispaa hii na vitongoji vyake ni maji japokuwa kuna mradi mkubwa wa maji ya ziwa victoria ulio chini ya katibu mkuu wa CCM bwana Wilson Mukama, unavyo tumika vibaya kukwamisha haki za msingi za wananchi wa manispaa hii katika kupata huduma hii.

  Mradi huu ulianzishwa kwa lengo la kuwakwamua wananchi wa mkoa huu uliopo kanda ya ziwa kutokana na dhiki ya maji iliyoikumba maeneo haya takribani miaka zaidi ya uhuru.Mradi umekamilka,lakini hauna tija kwa wananchi ikiwa wananchi wanakwamishwa kwa kukosa huduma hii kwa asilimia kubwa.

  Kulikuwa na haja gani ya kupoteza fedha nyingi kwaajili ya mradi huu wa maji ilihali wananchi wanateseka na adha hii kuliko hata wakati mradi haupo.Kinacho fanyika hapa ni zaidi ya usanii,inawezekana vipi mradi mmoja ukaendeshwa na makampuni mawili kwa kutumia pesa za wanyonge walipa kodi na kampuni hizo kushindwa kufikia malengo kusudiwa kwa wananchi.

  Kuna KASHWASA, yenyewe kazi yake kuzalisha maji na kuuzia SHUWASA ambaye naye ana sambaza maji kwa mlaji.Gharama zote anarundikiwa mlaji ambaye ni mnyonge bila kujali mwenye kuwajibika kwa ustawi wa watu na maendeleo yake ni serikali.Lakini pamoja na gharama hizi kuelekezwa kwa mnyonge lakini hata huduma hii haikidhi mahitaji ya watu.

  Nasema haikidhi si kwamba mradi ni mdogo la hasha,bali unakwamishwa na makampuni haya ya uendeshaji kwa kushindwa kupeleka maji kwa wakati muafaka kwa walengwa ambao ni wananchi.Leo takribani wiki nzima wananchi hawana maji,kisa KASHWASA anamdai SHUWASA,hivyo ameamua kufunga maji ili alipwe pesa anazo dai.Mbaya zaidi wadaiwa sugu ni Jeshi la polisi na Magereza,eti wanadaiwa zaidi ya milioni 500,lakini anaye teswa ni mlalahoi asiye kuwa na deni!

  Kabla ya mradi huu tulikwa na bwawa la Ning'wa ambalo kwa kiasi fulani lilitatua kero za wananchi,na hata mara baada ya mradi huu wa ziwa Victoria kukamilika tulikuwa tunapata huduma hii ya bwawa hili mara mabingwa hawa walipokuwa wanatunishiana vifua jinsi ya kuwaadabisha wanyonge kwa kuwakatia maji.

  Lakini ajabu na kweli bwawa hili nalo lipigwa bei na wajanja kinyemela,bwawa hilililiwahi kutaka kuuzwa kinyemela wananchi walipogundua walitishia kuaandamana na kuwatoa ofisi wale wote walio husika.Mbaya zaidi wadau wa bwawa hili ambao ni wananchi hawakuhusishwa na si ajabu kanuni ya procurement haikuzingatiwa.

  Aliye linunua bwawa hili ni Mtanzania mwenzetu kwa jina la mzee wa vijisenti(Chenge),bila hata kutaka kujua thamani ya utu wa watu wanaotumia bwawa hili.Hali kama hii inatokea serikali ipo, lakini hakuna hatua yeyote inayo chukuliwa ilikuwa kunusuru wananchi kutokana na adha hii.

  Tunataka serikali kupitia wizara ya mali asili na utalii kulifuatilia suala hili kwa kina na kutoa maelezo kwa wananchi wake waliyoiweka serikali hiyo madarakani,hatima ya bwawa hilo liltumika miaka dahari kwa matumizi ya binadamu.Pia mh. Chenge wewe ni kiongozi mwakilishi wa wananchi,kwanini hukufanya uchunguzi kabla ya kulinunua hasa ukizingatia wewe ni kiongozi uliye chaguliwa na watu ili kuwaongoza na si kupora hata kile kilichokuwa kimbilio lao.

  Changamoto kubwa hapa ni kwa waziri mteule wa wizara hii ya mali asili na utalii kulifanyia kazi suala hili kwani hata kama kulikuwa na haja ya kuuliza basi mngepata baraka za wadau wanao tumia huduma hii.

  Tanzania tuitakayo,tutaipata ilihali rasilimali zetu zote zimekwisha porwa na mabwenyenye?Tuanze sasa kupingana na wadokozi wa mali ya umma.  Source ya uuzaji wa bwawa hili toka kwa Diwani viti maalumu(CDM)
   
 2. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,240
  Trophy Points: 280
  Nadhani mbunge wa Ridhiwani ndugu Masele atatatua hiyo kero
   
 3. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,357
  Trophy Points: 280
  lihabari refu ova kojo la mlevi..mtu anisaidie ameeleza nini,especially inamhusu fisadi chenge ndo nimechoka hata kuisoma,hivi we mleta uzi ulimpigia kula huyu fisadi?
   
 4. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  sijaelewa
   
 5. monongo

  monongo JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  kwa kweli hakuna wananchi wanaodharauriwa hapa Tanzania kama Shinyanga.kuna pepo gani? Mbona rasilimali za wananchi zinaporwa ki-hasara hasara? Siri-kali iko wapi? Au mnataka tuchukue mapanga na mashoka, panga na rungu? Shinyanga kuna wakoloni weusi na mabwa nyenye weusi,ipo siku tu!!je, mbunge wa viti maalumu S.Maselle analijua hilo?
   
 6. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kila jambo lina wakati wake,sasa ni wakati wa mabadiliko ya kweli kutoka mfumo dume wa kimangimeza kuelekea mfumo wa haki sawa kwa wote.Shinyanga ya leosi ya jana.Mabadiliko yataendelea siku hadi siku.Uwezo wa kuwaadabisha tunao,sababu tunayo na nia tunayo,kilichobaki siku zao zilizokuwa zinahesabika sasa zimetimilika
   
 7. MANI

  MANI Platinum Member

  #7
  May 25, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Jamani tusiwe wavivu wa kusoma!
   
Loading...