Mhere Mwita awapatia msaada wakina mama wodi ya wazazi hospitali ya Geita alipozaliwa

ccm makinikia

New Member
Aug 19, 2017
1
0
d431a4862099468da46c4bc38085855e.jpg
MHERE MWITA AWAFURAHISHA WAKINA MAMA WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA GEITA.

Mwenyekiti wa Bavicha Wilaya ya Geita Kamanda Mhere Mwita Leo amesherekea siku Yake ya kuzaliwa kwa kutembelea wodi ya wazazi Katika Hospitali ya Mkoa wa Geita na kuwapatia mahitaji watoto ambao wamezaliwa na yeye Tarehe Moja 18 mwezi wa 8.

Mwenyekiti huyo wa vijana amewapatia kina mama nepi na pini zake, Ndizi mbivu, Pampas za watoto, soksi za watoto, na Kofia za watoto zenye thamani ya shillingi 250000/= kama hongera ya kuvumilia uchungu na wengine kujifungua wakiwa salama.

Zaidi ya kina mama 15 walio jifungua na 20 wenye ujauzito wamefurahia Msaada waliopatiwa na kiongozi huyo wa vijana wilaya ya Geita, akieleza Mama Mmoja aliojulikana kwa jina la Mama Esther ambae alikuja kumuona ndugu yake amejifungua.

Amesema "Nimefurahi sana kumuona kiongozi huyu wa Chadema kuja kututembelea na kutuletea mahitaji ya watoto, kwa kweli ameonyesha kutujali sana sisi wazazi Mwenyezi Mungu ambariki sana kijana wetu kwa kweli".

Vile vile kama Mhere Mwita wamewashukuru makamanda ambao walioshirikiana nae Katika kufanikisha jambo hili kwa nafasi ya kipekee anapenda kuwashukuru Kamanda Rose Mayemba mpambanaji kutoka Njombe Julius Manyonga na Jenifer Diwani wa Bukoba Vijijini

Alipotoka hapo wameenda kumpumzisha Mzee Msumeno Mapesa Baba mzazi wa waliekuwa Katibu wa chadema jimbo la Geita mjini na aliekuwa Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa mtaa wa Uwanja Geita Mjini. Kamanda Ezekiel Mapesa.

Imetolewa na;~
Katibu wa Bavicha(w) Geita,
Nguru Bright.
 
nice! viva chadema! mijitu kama pole pole sijui hata km imewah toa shukran hata kwa yatima !
 
`Kwa nini anafanya hivyo, serikali inafanya kazi gani? anatafuta kiki hospitali....' hizi ni baadhi tu ya comments za bavicha kama aliyefanya hayo angekuwa ni kiongozi wa ccm.
Mimi nampongeza mwita kwa moyo wake wa kujitoa.
 
Huyu jamaa ana moyo wa huruma sana au ana kihere here cha siasa, juzi tu alikuwa anaomba msaada wa hata 3m Tsh kwa ajili ya matibabu yake, ni vyema kabla ya hizi kiki akate hata premium service za bima ya afya.
Apambane na hali yake kwanza kabla ya hizi stunt.
 
Back
Top Bottom