Mhe. Zitto, hongera kwa uzalendo, sema ukweli usipotoshe, hakuna mkataba uliosainiwa, kilichopo ni draft tuu na kuwa initialed sio kusainiwa!

Mimi sijali kuitwa muongo. Ninachojua sijasema uongo wowote. Nimeusaidia umma kufafanua hiyo FRAMEWORK agreement ambayo Serikali yetu imesaini ( kwa lugha ya mkataba INITIAL ). Sasa kama hiyo agreement haipo nitakuwa mwongo. Kama ipo Paskali ajifunze tu.
Zitto we si mwongo pia mpotoshaji
 
Naamini, I might not be right, Zitto is much more ahead of you in such matters leave alone your capacity as a reporter and not an investigative reporter! aspects!
Ndugu Pascal unatumia nguvu nyingi mno bana ! Kwani wewe hujui unafiki wa ZZK ? lakini vizuri kuweka these kinds of details ili watu wengi waelewe ! Zitto niliwahi sema ni DISTORTER IN CHIEF ! I MENT IT SQUARELY!
 
Mimi sijali kuitwa muongo. Ninachojua sijasema uongo wowote. Nimeusaidia umma kufafanua hiyo FRAMEWORK agreement ambayo Serikali yetu imesaini ( kwa lugha ya mkataba INITIAL ). Sasa kama hiyo agreement haipo nitakuwa mwongo. Kama ipo Paskali ajifunze tu.
YOU ARE A DISTORTER IN CHIEF ! PERIOD ! Tulia serikali ifanye kazi na matokeo utayaona ! Shame on you ! Dont think you are the best brain in this country and everyone else is stupid. Hata hao walio tuingiza mikataba ya hovyo they were equally intelligent only that they focused on personal gains ! AND YOU KNOW IT PRETTY WELL IN YOUR HEART.
 
Kuna maeneo maalumu ya kusign sio kila page, then una initial page zote ili wasije zibadirisha.

Inawezekana alichokiona Zitto ni intialed pages

Maana ake we already have one of the most unlawful and stupid agreement between the government and those you are calling imperialists

..hata mimi nilitaka kusema kitu kama hicho.

..katika mikataba ziko sehemu / vipengele ambavyo una-initial. Halafu kuna sehemu unaanguka saini.

..kwa hiyo, nadhani Pascal Mayalla alitakiwa aweke angalizo kuhusu masuala ya "initials" vs "signature". Hakutakiwa moja kwa moja amtuhumu Zitto kuwa amepotosha.

..lakini ukiangalia MAUDHUI ya makubaliano aliyoyaleta Mh.Zitto unaona kabisa kuwa hakuna win-win situation, bali kuna win-loss situation.

..Na katika hili inawezekana Prof.Kabudi hastahili lawama kiasi hicho. Inawezekana kuwa tulikuwa hatuna madai ya uhakika au ya msingi zaidi ya kilio kwamba hatufaidiki na uchimbaji madini.
 
..hata mimi nilitaka kusema kitu kama hicho.

..katika mikataba ziko sehemu / vipengele ambavyo una-initial. Halafu kuna sehemu unaanguka saini.

..kwa hiyo, nadhani Pascal Mayalla alitakiwa aweke angalizo kuhusu masuala ya "initials" vs "signature". Hakutakiwa moja kwa moja amtuhumu Zitto kuwa amepotosha.

..lakini ukiangalia MAUDHUI ya makubaliano aliyoyaleta Mh.Zitto unaona kabisa kuwa hakuna win-win situation, bali kuna win-loss situation.

..Na katika hili inawezekana Prof.Kabudi hastahili lawama kiasi hicho. Inawezekana kuwa tulikuwa hatuna madai ya uhakika au ya msingi zaidi ya kilio kwamba hatufaidiki na uchimbaji madini.
Mimi najua kilichotokea, mabeberu walipogundua jamaa ni mpenda sifa, anataka aonekane yeye ndio the almighty, the know all one,wamempatia.

Masikini utakuta hawajampa hata shilingi wamempigia magoti tu then wakampeleka kwenye hoja kitu asichokiweza and this is what we have today.NOTHING.
 
Mkuu Whitesmith
  1. Yes ni draft ya kweli
  2. Imeandaliwa na Barrick na kuridhiwa na GOT
  3. Yes huu ndio ulikuwa mwelekeo kabla serikali haijagoma kusaini mpaka Acacia aondoke.
  4. True
  5. Kwa sababu huo ndio uwezo wetu, mimi nilidhani watu watahoji ilikuwa tusamehe dola bilioni 190 kwa ajili ya kishika uchumba cha dola milioni 300?.
P
Mkuu Pascal
Kwanza hiyo dola billion 190 ambayo TRA ilitengeneza na hapakuwa na uhalisia yaani wao wamechukua ripoti Prof. Kabudi wakakokotoa yaani tuseme dhahabu ukienda migodini inaokotwa with no operational costs. Pili tunajua TRA nje nakuwa mamlaka yaukusanyaji kodi pia ni fimbo ya serikali dhidi ya yoyote ambaye yuko against system. Tokana na sababu ya pili TRA ikakosa uwaledi ikaja na wrong figure ambayo siyo tu halipiki bali haijadiliki. Technically akazaliwa mdogo wake na dola billion 190 ambaye anaitwa dola million 300. Hivyo mkuu tuhoji nini wakati ni obvious.
Ni aibu kubwa sana kwa serikali ya JPM kuja na agreement ya hovyo kiasi hicho ile hali imesheni ma Dr na Prof…Hiki ndo tunachohoji mkuu kwasababu Dolla billion 190 ilikuwa fimbo tu yakumchapa mwekezaji nakumlazimisha aje meza ya majidiliano. Sasa tulikuwa tunamshauri mkuu haya mambo yawekwe wazi tuyajadili ili tutoe mawazo yetu tuende mbele kama one nation, one team badala take wakajifungia chumbani. Nakuhakishia mkuu P jambo LA faragha ambalo Mungu amelibariki na linaleta matokeo mazuri ni “tendo la ndoa” nje na hapo mambo ya umma yapelekwe kwa umma.
Thanks
 
Napata tabu kumpinga zitto bila kuona kilichoandikwa kwenye makubaliano, na kama kweli barrick wamelitupa kabrasha barabarani likaokotwa lazima liende na mtu,
 
Wanabodi,
Tangu baada ya Barrick kutangaza kuninunua Acacia, kumeibuka mijadala mingi kuhusu suala hili, haku wanasiasa waki capitalize kwa kutafuta political score na political capitalization kuhusu jambo hili, kwa kutumia hoja za uongo au upotoshaji wa makusudi for political gain au upotoshaji wa bahati mbaya kutokana na kutokujua vizuri lugha ya Malikia.

Sijitapi kuwa mimi ndie mtu wa kwanza kuleta hii braking news ya Acacia kununuliwa, na ni miongoni mwa wana jf tulioandika sana kuhusu hili, to be on a safe side, kunapotokea mambo yahusuyo lugha za watu, huwa ninaweka source ili ukajisomee mwenyewe, hivyo hili ni bandika la kukosoa Mhe. Zitto kwa uongo na upotoshaji huku nikimuomba asikasirike kama lugha ya malikia haipandi kivile, kwa vile tuko wengi tuu lugha hii inatupiga chenga, kuanzia ile 1st Class ya LL.B ya Sheria ya UDSM yenye GPA ya 4.9 na Ph.D ya Sheria, hadi Ph.D ya Kemia, hii lugha ya malikia kwenye hili imesumbua, watu waliambiwa 50/50 ya Economic Benefits, wakatueleza ni 50/50 ya net profits!. Mhe. Zitto naye kaona Draft Agreement ikaelezwa imekuwa initialed, kaibuka kuwa ni mkataba umesainiwa!, kakwe draft agreement ni mkataba, na kuwa initialed kwake ni kusainiwa!, hizi lugha za watu jamani, zisitufanye kuwa waongo na wapotoshaji, tuwe wakweli daima, tell the truth and the truth will set you free!.
Naomba tuanzie kwenye bandiko langu kuhusu jambo hili

Kwenye bandiko hili, niliweka links za Barrick na Acacia.

Ndipo Mhe. Zitto naya akaibuka na bandiko lake, japo hoja zake kwa asilimia kubwa ni za kweli, lakini pia kuna asilimia ndogo ya uongo na upotoshaji mkubwa kama kupotosha kuwa makubaliano yamesainiwa!, hakuna makubaliano yaliyosainiwa!.

Mkuu Mhe. Zitto, kwanza asante kwa bandiko hili na uzalendo wako kwa nchi yako. Kwa vile mimi ni miongoni wa wana jf ambao tumeandika sana kuhusu hili, nitachangia baadhi ya vipengele with reference ya nilisema nini, nilishauri nini na kulinganisha na kilichotokea ni nini, but with due respect, na wasiojua ligha ya Malikia, ni kwa heshima na taadhima, tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tuache urongo na upotoshaji, just tell the truth and the truth will set you free, sii kweli kuwa mkataba huu umeisha sainiwa!, hilo neno (INITIALED) sio kuonyesha kuwa umesainiwa, bali katika mikataba, kunatakiwa signatories watie initials zao kwenye kila page ya draft kuonyesha wameelewa, lakini draft ni draft na mkataba ni mkataba!, ku INITIALED sio kusaini.

Hicho kiambanisho 4 ni draft, na mimi nimekiweka kwenye bandiko langu la tangazo la kifo cha Acacia
na nikasisitiza,

Hatuwezi kusema kila kitu mpaka baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, na nikasisitiza kwenye makinikia kuna lakini sikuiweka hiyo lakini kwa sababu bado hatujaona makubaliano yaliyofikiwa, as of now hayo ni mapendekezo tuu, yaani draft, siku zote drafts zote huwa ni tentative, inaweza kubadilika, hivyo naomba kusisitiza katika hili tuwe wakweli, tutumie ukweli, tuache urongo na upotoshaji!.

Sijamuita Zitto muongo, au mpotoshaji, nimesema kwenye hoja zake kuna uongo na upotoshaji. Kwa vile Zitto namfahamu fika toka enzi zetu za UDSM, hivyo naifahamu intelect ya Zitto, haiwezekani katika kiambatanisho hicho, awe hayajaona maneno haya
"Appendix 4 Summary of the material terms of the current draft documentation under discussion (but not yet finalised) with the GoT The discussions between Barrick and the GoT have advanced to the point where draft documentation was initialled by the GoT on 19 May 2019". Hapa maana yake hii ni draft tuu imekuwa initialled na GOT lakini haijawa finalized, kwa Zitto ninayemjua mimi, haiwezekani Zitto awe hakuyaona maneno haya.

Kwenye document hiyo, kuna maneno ya capital letters na bold
"THERE IS NO CERTAINTY THAT THE TRANSACTION DOCUMENTS WILL BE AGREED WITH THE GOT IF THE SCHEME BECOMES EFFECTIVE AND THE TERMS OF THE FINAL FORM OF TRANSACTION DOCUMENTS, IF AGREED, MAY DIFFER FROM THOSE SUMMARIZED BELOW."
Siamini kuwa Zitto hakuyaona maneno haya, kwa wasio jua lugha ya Malikia ni "hakuna uhakika kama makubaliano haya yatakubaliwa na GOT, na hata yakikubaliwa, yanaweza kuwa ni tofauti na kilichokubaliwa hapa!. Hivyo Zitto kusema ni mkataba umesainiwa, huu ni uongo wa mchana kweupe, na amepotosha kwa makusudi tuu sio kuwa hakuona mistari hiyo!.

Kwenye kipengele cha 11 cha makubaliano hayo kinasema wazi kuwa
"11. The conditions set out in (a) to (g) of paragraph A10 above may be waived by the Acacia parties and the conditions set out in (h) to (i) of paragraph A10 above may be waived by the GoT. "
Hapa wanasema masharti ya mkataba huu yaliyowekwa kwa ibara ya 10, yanaweza kukubaliwa au kukataliwa na Acacia, au na GOT kuthibitisha kuwa makubaliano haya sio final and conclusive, haiwezekani Zitto ninayemjua mimi, hakuliona hili!.

Kipengele cha 12 kinasema
"12. Those provisions which are stated to become effective on signing of the Framework Agreement"
Hapa kwa lugha ya Malkia ni masharti hayo, yatatakiwa kutekelezwa baada ya kusaibiwa kwa makubaliano hayo, bado hakuna makubaliano yoyote yaliyosainiwa!. Siamini kuwa Zitto hakuliona hilo.

Kwenye kiambatisho hicho kuna hii para
"The discussions between Barrick and the GoT have advanced to the point where draft documentation was initialled by the GoT on 19 May 2019, albeit with a number of substantive issues still outstanding which are subject to further discussion. Whilst a basis for settlement has been developed, the terms have not yet been finalised"
Naamini kabisa Zitto anajua maana ya maneno hayo, hawa jamaa wanasema bado kuna issues ni still outstanding na zinahitaji majadiliano zaidi.

Sasa ili kumtendea haki Mhe. Zitto, naomba kuziweka hoja zake zote 5 na kusema hoja zipi ni za kweli na hoja zipi ni za uongo na upotoshaji tuu.

1. Dola Milioni 300 za kumaliza mgogoro KIINI MACHO

Serikali imekubaliana na Barrick kuwa italipwa Dola milioni 300 (wastani wa TZS 700 Bilioni) kama malipo ya kumaliza mgogoro wote (full, final and complete settlement) na SIO kishika uchumba kama Serikali ilivyoeleza umma. Barrick watalipa fedha hizi kwa muda wa MIAKA 7 na zitakuwa ni baada ya kuondoa madai yote ya kodi ambayo Acacia inaidai Tanzania.

Itakumbukwa kuwa Acacia Group ina madai ya marejesho ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT refunds) inayofikia takribani Dola za Marekani milioni 240 (wastani wa 552 Bilioni). Hivyo katika malipo ya Dola za Marekani Milioni 300, zitakazobakia baada ya kutoa madai ya VAT refunds ni Dola Milioni 60 (wastani wa 138 Bilioni) tu. Kama tutakavyoona katika hoja ya pili hapa chini hata hizi Dola za Marekani Milioni 60 kimsingi hazitatolewa.

Kwenye hoja hii Zitto kuna sehemu amesema kweli, hapa tumepigwa. lakini kuna sehemu Zitto sio tuu hakusema kweli bali amesema uongo. Kwa vile Mhe. Zitto ni Mbunge akisema kitu ndipo watu wanakizingatia, hivyo Zitto hili la dola milioni 300 ndio ameliona baada ya kusoma draft ya makubaliano na kulisemea kwa kulipotosha wakati sisi akina kajamba nani, hili tuliliona kitambo na tukalisemea sana humu.

Baada ya Barrick kuinunua Acacia, ni kweli kweli tutalipwa kifuta machozi cha dola milioni 300, sii kweli kuwa malipo haya yatatolewa baada ya kuondoa VAT refund, bali kweli kuwa malipo haya yatalipwa katika kipindi cha miaka 7.
Tukiisha saini mkataba, tutalipa upfront ta dola milioni 100. Hivyo hoja ya Zitto kuwa kwenye dola milioni 300, tutaambulia dola milioni 60 tuu, huu ni uongo wa mchana kweupe. Ile siku Barrick wanakuja kusaini mkataba, ile kuangusha tuu wino kusaini, kitita cha dola milioni 100 kinawekwa mezani as upfront payment kama ilivyoelezwa hapa
"There will be an initial upfront “payment” by way of assignment to the GoT of minerals contained in containers at Dar es Salaam port with a value of US$100 million". Shilingi milioni 200 zilizobakia, ndizo zitalipwa katika mikupuo 6 ya dola milioni 33.33 kwa mwaka katika miaka 6.

Pamoja ya Zitto kutokuwa mkweli, lakini ukweli wa Zitto kuwa tunapigwa uko pale pale. Tunapigwa kwa sababu hizi dola milioni 300, tuliahidiwa as goodwill money, hasikupaswa kuwa conditional wala hazikupaswa kulipwa kido kidogo, zilipaswa kulipwa there and then.

Kitu cha pili kwa vile hiki kilikuwa ni kishika uchumba tuu na kuonyeshea goodwill ya kulipia mahari kamili ya binti yetu ambayo ni dola bilioni 190, lakini serikali yetu imesamehe mahari yote, na kile kishika uchumba sasa ndio kigeuzwa kifuta machozi, hapa sasa ndipo tulipopigwa!. Hapa nilishauri serikali yetu lazima itufafanulie Watanzania the basis ya msamaha huu.

Kwenye hili kiukweli mimi nimelisema sana humu.
Nchi ya kusadikika na kisa cha binti Mfalme aliyebakwa; Baba wa ...
Dola milioni 300, siku 90, sentano kipande haijalipwa! acacia ...
Hatari ya kulizwa? Acacia waanza kufungasha kiana, wauza mgodi ...
Je, wajua kuna uwezekano Barrick wanatuingiza mkenge?!. Hili la ...
Priorities Zetu Nini?. Dola Milioni 300 Zinatosha Kununua Smelter ...
Dola Milioni 300 zetu za kishika uchumba cha Acacia, danadana ...

2. Barrick Gold Wamesamehewa Kodi ya Ongezeko la Mtaji USD 85.6M

Serikali ya Tanzania imetoa misamaha mbalimbali ya Kodi kwa Kampuni ya Barrick Gold katika makubaliano yaliyoingiwa ikiwemo kodi ya ‘Capital Gains’ ambayo inatokana na mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick. Itakumbukwa kuwa mwaka 2012 Bunge lilitunga sheria ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Mtaji kwa mauzo ya mali zilizopo Tanzania ili kudhibiti ukwepaji wa Kodi.

Barrick inainunua Acacia kwa Hisa ambazo Barrick haikuwa inamiliki ambazo zimepewa thamani ya Dola Milioni 428. Capital Gains Tax ya 20% ilipaswa kulipwa lakini Rais Magufuli na Profesa Kabudi wametoa ‘waiver’ (Msamaha) na kupoteza Mapato halali na ya kisheria kwa nchi yetu ya Dola Milioni 85.6 (wastani wa TZS 200 Bilioni). Tukirejea hoja ya kwanza hapo juu utaona kuwa sio tu Tanzania kiuhalisia haitapata Dola Milioni 300, bali pia tunaipa zawadi Barrick ya Dola Milioni 25.6 (wastani wa TZS 59 Bilioni) za ziada.
Hili ni kweli, hawa na ni kawaida kwa serikali yetu kutoa misamaha ya aina hii kwa kutotoza capital gain tax kwenye acquisitions kibao, au kwenye hostile take overs,
Celtel ilibadilika kuwa Zain, ikabadilika kuwa Airtel, hakuna tulicholipwa!.
Sheraton ilibadilika kuwa Moven Pick, Royal Palm sasa Serena sijui kama tulilipwa kitu!.
Mibitel, iligeuka kuwa Tigo sijui kama tulilipwa kitu!.
Kibo Breweries ilikuwa taken over kwenye hostile take over, sijui kama tulilipwa kitu, hivyo hapa Zitto is right, but its not the first time, kama kule kuingine tumetoa misamaha hiyo, why not now?.

3. Tanzania kupewa Hisa 16% za daraja B lakini Watanzania kunyimwa umiliki wa 30% kupitia Soko la Hisa la DSE

Ni kweli kuwa Serikali itapewa hisa za bure 16% kwenye Kampuni tanzu zote za Acacia hapa nchini kama tulivyoambiwa na Serikali. Lakini hisa hizo ni za Daraja la B ambazo ni hisa dhaifu kulinganisha na zile za Daraja la kwanza. Hisa hizo haziruhusiwi kuuzwa, hazina kura kwa masuala fulani fulani ya Kampuni na huwezi hata kuziweka kama dhamana ya mikopo. Hata mgawo wa gawio hisa hizi hupata baada ya wale wa daraja A kulipwa kwa ukamilifu.

Licha ya makubaliano haya ya hovyo na yasiyo na tija, Serikali yetu imetoa ‘waiver’ (msamaha) kwa Barrick kutoorodhesha hisa kwenye Soko la Hisa la Tanzania. Sheria ya Madini ya mwaka 2010 (Wakati wa Waziri William Ngeleja) na Kanuni zake iliweka sharti kwamba ni lazima makampuni ya madini yauze 30% ya hisa kwa Watanzania kwenye soko la Hisa la Tanzania.

Makubaliano ya Mei 2019 kati ya Barrick na Serikali ya Tanzania yametoa msamaha kwa Barrick kutekeleza sharti hilo la kisheria. Uamuzi huu unavunja sheria za nchi, ni hujuma kwa Watanzania kumiliki maliasili zao na ni ukosefu wa maarifa ya kiuchumi kwa kiwango kisichomithilika wala kuvumilika.

Hili la hisa za daraja B ni kweli lakini sii kweli kuwa Watanzania tumenyimwa umiliki wa 30% kupitia DSE!.
Hizi hisa aslimia 16 za Tanzania, ni free carried shares, tumepewa bure, na kote free carried shares huwa haziuzwi ila sii kweli kuwa hazina voting rights, huu ni uongo!. Pia sii kweli kuwa Watanzania tumenyimwa umiliki wa 30% kupitia DSE!.
Naomba hapa ikumbukwe, shares zinazouzwa ni shares za Acacia zinazo trade kwenye London Stock Exchange tuu, hata yale mambo ya PUSU ni mambo yao, sijasikia lolote kuhusu shares za Acacia zinazo trade kwenye DSE, hivyo business ya hisa za Acacia ndani ya DSE zinaendelea as usual.Hata baada ya sale kukamilika, hivyo kampuni mpya italazimika kuuza 30% ya hisa zake kwenye DSE na Watanzania wenye fedha, watakuwa free kununua hisa hizo kwenye soko.

Tukija kwenye voting rights, sii kweli kuwa Tanzania hatuna voting rights, bali ni kawaida kwa free shares zote hazina voting rights ya pro rata ya share to shares bali tuna voting rights za block shares. Sisi Tanzania wenye free carried shares za 16%, serikali yetu iteteua mjumbe mmoja wa bodi ambaye ni Mtanzania, ataingia na kuwa mjumbe wa bodi ya hiyo kampuni mpya, kwa zile asilimia 16% za shares zetu na ndani ya kikao cha bodi, atakuwa na voting righs za kupiga kura 1 as a block vote kuwakilisha zile shares 14, wakati wajumbe wengine wengine wa bodi, watakaowakilisha zile subscribed shares za asilimia 84%, wanatakuwa na voting rights ya votes 84 kwa uwiano wa share to shares votes pro rata according to shares subscription. Hivyo ndani ya bodi ya hiyo kampuni Mtanzania atakayeingia humo, atakuwa anapiga kura moja kuwakilisha the block ya zile shaes zetu 16 za bure, na katika mgao wa faida, sii kweli kuwa tutapata mgao baada ya wale wengine, huu ni uongo!, Tanzania tunagaiwa mgao sawa kabisa wa faida kwa mujibu wa shares hizo.

Kwa wasio jua kuhusu shares za group A na group B shares za group A ni shares za watu walio invest kwa kutoa fedha zao kununua shares, yaani subscribed shares, na shares group B ni shares za heshima, shares za hisani zinazotolewa bure, shares hizi za hisani haziruhusiwi kuuzwa, wala kuwa disposed or transferred na zina block votes rights. Hili hufanyika kwa makampuni kuwapa hisa za heshima land owners, mfano UAE, hakuna foreigner anayeruhusiwa kumiliki ardhi, ardhi yote ni ya wazawa, hivyo investor akija lazima aingie ubia na wazawa mzawa anatoa land, investo ana jenga, kama alivyofanya Rugemalila kwenye IPTL alitoa ardhi yake na kupewa 30 m% ya shares, IPTL ikaikwa kwa PAP, Ruhemalila akalipwa shares zake, akagawa fedha zake, sasa anateswa bure bila kosa lolote!.

4. Bunge lafungwa mikono kubadili sheria yeyote
Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Barrick wamekubaliana kuwa baada ya mkataba wao kukamilika Bunge la Tanzania haliwezi kutunga sheria yeyote ambayo itabadili makubaliano hayo na kodi zote zilizokuwa zinafanya kazi wakati wa kuingia makubaliano hazitaweza kubadilishwa kipindi chote ambacho Barrick watakuwa wanafanya kazi Tanzania (fiscal stabilisation).

Makubaliano ya namna hii ndiyo kitu kilicholeta Buzwagi mwaka 2007 ambapo Serikali za Rais Mkapa na Rais Kikwete ziliingia mikataba ya kulifunga Bunge kutimiza majukumu yake ya kikatiba kama Dola (sovereign). Sheria ya Madini yam waka 2010 iliondoa sharti hili kufuatia mapendekezo ya Kamati ya Bomani. Rais Magufuli na Waziri Kabudi wameturudisha kwenye unyonyaji wa kihayawani kabisa.

Kwenye hili pia Zitto hajasema kweli, kwenye document hii yenye kurasa 91, hakuna popote Bunge la JMT limetajwa!. Makubaliano haya yatatawaliwa na sheria za Tanzania. Hakuna popote Bunge limetajwa, bali kilisemwa ni maadam sheria iliyotungwa ninaelekeza free carried shares ni asilimia 16%, baada ya kusainiwa kwa makubaliano haya, serikali haiwezi kuongeza kile kiwango cha shares zaidi ya asilimia 16% za kisheria unilateral, kama ilivyofanya kwa sheria mpya ya madini "the GoT will not unilaterally seek to increase its share ownership or economic participation rights in the TMC", hii maana yake, serikali haiwezi kujiamua yenyewe pekee bila kuishirikisha Barrick.

Hili mimi nililizungumzia kitambo ile tuu tunabadili sheria, kuwa kisheria, sheria yoyote ambayo ni sheria nzuri, inaanza kufanya kazi tangu pale inapotungwa. Sheria yoyote inayotungwa halafu ina act retrorespect is a bad law. Hivyo tulipopitisha sheria mpya, nikasema tuwashukuru sana Barrick wamekubali kuanza upya kwa sheria mpya, Hakuna mwingine yoyote mwenye mkataba wa zamani amakubali kubadili na kutumia sheria mpya.

5. Barrick wameruhusiwa kufungua kesi ughaibuni kinyume na Sheria

Kwa mujibu wa sheria mpya za madini za mwaka 2017 makampuni yamezuiliwa kufungua mashauri yake nje ya Tanzania. Migogoro yote inapaswa kushughulikiwa na mahakama za ndani ya nchi. Serikali ya Tanzania imekubaliana na Barrick kuwa migogoro itafanyika kwa mujibu wa kanuni za UNICITRAL na Rais wa Kituo cha usuluhishi wa migogoro cha Singapore ndio atateua wasuluhishi ambao hapatakuwa na Mtanzania.

Kwenye hili, Zitto yuko right 100% kipengele kwenye sheria yetu mpya kinachokataza usuluhisi nje ya Tanzania ni hiki
View attachment 1158849

Ile siku sheria hii inapitishwa Bungeni, mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa sheria, Tundu Lissu, alionya kuhusu hili kuwa hatuwezi kupitisha sheria ambayo hatuwezi kuitekeleza and soon tutakuja kuifanyia marekebisho. Hivyo hapa Zitto yuko right, makubaliona haya ni kinyume cha sheria, hivyo ni illegal.

Neno kwa wapenzi wa Zitto.
Kwa wapenzi wa Zitto, naomba kuwahakikishia, lengo la bandiko hili sio kumtweza au kumbagaza Mhe. Zitto, bali ni kumuelimisha tuu na kumtaka awe mkweli kwa kuacha upotoshaji, ila kiukweli kabisa Zitto ni kati ya wanasiasa makini na mahiri kabisa ninaowakubali, na hata nikashauri, kama Tanzania tunataka ushindani katika uchaguzi wa rais 2020, Zitto ndio the one and only anayeweza kuleta ushindani kwa mgombea wa CCM 2020.

Zitto is and has been my hero na hapa nilimchambua vizuri
Nawatakia Jumapili Njema.
Asante.
P
Kumhusu Zitto, nimeisha wahi kusema haya

Zitto ni Mzalendo wa kweli, Baada ya kumsikiliza leo, nimebaini ...
Kiukweli, Kama Sio Nguvu ya Soda, Then ACT ni Tishio. Hawa ni The ...
Face to Face with Zitto Kabwe: Kuhusu Kupika Data, "Namheshimu ...
Zitto Zuberi Kabwe Ni Mchochezi, Akamatwe, Ashitakiwe Kwa ...
Wafuasi wa Zitto na Manazi wa CHADEMA: Tunajenga Nyumba Moja ...
Kichaa Mmoja, Anaweweseka Sana Juu ya Zitto, Kamtungia Uongo ...
Kama Tuhuma Hii ni Kweli!, Then This is "The End Of Zitto ...
Wapinzani msione aibu kushirikiana na CCM kwenye hoja zenye ...
Kilichomkuta Zitto: Kuna mkono wa Mtu! Yajue makundi 10 ya ...
La Zitto Kuvuliwa Nyadhifa CHADEMA: Mhe. Zitto, Please! Play It ...
Opinion: Kung'atuka Kwa Zitto, CHADEMA, Msishangilie, Mkajisahau ...
Unapenda sana kurejea vitu viiiiiiiingi ulivyokwishaeleza nyuma ili kujenga hoja zako japo ungeweza kujieleza kwa ufupi na ukaeleweka

Pamoja na kufanya rejea ya hoja zote hizo maelezo yako marefu yanalenga kumkosoa Zitto anaposhindwa kutofautisha INITIALED na SIGNED. Hiyo ndo hoja yako kuu niliyoiona

Sasa na wewe umeshindwa kutetea unachokitetea vizuri. Nina maswali kadhaa yatakapojibiwa huenda nikaelewa vizuri:-

1. Kilichomo ndani ya document ambayo iko INITIALED ndicho serikali ilitueleza!? Kama sio chenyewe, huoni bado Accacia na serikali hawaongei lugha moja kama tulivyoambiwa kwamba"wamekubali kulipa kiasi tulichotajiwa!?"

Sasa kama mambo yaliyomo kwenye document ya 19May 2019 hayaendani na tuliyoambiwa wamefikia makubaliaono 2017, hapo uongo wa Zitto uko wapi!?


2. Je hiyo draft ina vitu vile vile alivyotueleza Kabudi kwamba Accacia/Barick wamekubali kutekeleza? Yale madolali tuliyotajiwa hata kwenye hiyo draft ya May 2019 wamekili kuyalipa?

Kama yako vile vile kama tulivyotajiwa basi Zitto ni muongo na hafai kuaminiwa

NB: Mimi ni msomaji tu wa issue zinazoendelea nchini kwa juu juu hivyo nikiri tu nafaidika na uchambuzi wenu hivyo hata hili swala nalo nalielewa juu juu tu ila nimeshindwa kukuelewa unaposema Zitto ni muongo wakati huo huo hatuambiwi kama Accacia wamekubali kulipa bila masharti yoyote
 
Do you mean the draft carries Zitto recommendations? what Zito did, is to inform us what is in the draft, he has nothing to do with the draft. whether the final binding document will change or not, that is another case, but as how it stands the draft is it is as Zito informed us. So your common sense lead you to believe negotiations of about two years now should come up with this kind of a draft!? Get out of the box so that you can be able to see reality.
I see...!!
 
Mkuu Beem, draft ni draft na mkataba ni mkataba.
P
Kwa hiyo uncle@Pascal Mayalla kwenye draft ndio kuna initial sign, halafu kwenye mkataba kuna final sign? Je inawezekana kutumia draft kiofisi ? Na ndio je draft ikikataliwa wakati wa final sign ya mkataba hali itakuwaje?ilikuwaje serikali isaini initial pages za draftwakati zinatuumiza?
 
[MQUOTE="MAHORO, post: 32229558, member: 168268"]
Sasa ndo umeongea nn na wewe ?? Hoja yako iko wapi ?? Nàona ngojera nyingi tu humu ,

Nikuulize tu ka swali kadogo .... Nionyeshe wapi zitto alipopoposha
[/QUOTE]
Mahoro jibu lipo wazi wafuasi wa zito mnajitoa akili..daft na mkataba ni vitu viwili tofauti..zito kwa maelezo yake kasema mkataba umesainiwa wakati pascal kamueleza kinagaubaga kua hio ni draft na akaeleza mistari inayoeleza wazi kuwa Got inaweza kukubali au kukataa...akili za kijinga kujifanya hamuoni maelezo ya p
 
Mimi najua kilichotokea, mabeberu walipogundua jamaa ni mpenda sifa, anataka aonekane yeye ndio the almighty, the know all one,wamempatia.

Masikini utakuta hawajampa hata shilingi wamempigia magoti tu then wakampeleka kwenye hoja kitu asichokiweza and this is what we have today.NOTHING.

Hip draft imeandaliwa na Barrick na Got ndio wanaishughulikia na ndio sbb draft yenyewe inasema wazi kua Got inaweza kuyakubali au kukataa....Mbona hamuoni hilo...
 
Hip draft imeandaliwa na Barrick na Got ndio wanaishughulikia na ndio sbb draft yenyewe inasema wazi kua Got inaweza kuyakubali au kukataa....Mbona hamuoni hilo...
Why did they reach to such stupid terms even if it is a draft level document.

Why did they think we can accept this shit? What makes them start thinking like that while they are well aware about magufuri's stance on his economic war?

Why do they think he will accept such an insult?

Why?

Why?
 
... Apart from a mere simple fact that he honorably blindsided you on the differences between a Draft version and a Final version of the doc, He went on to skillfully misinterpret the content itself.

My biggest concern is that most folks usually don't like to read anything longer than half a pager. To make matters worse, this particular one is not just an ordinary doc, it is a legal framework written in a foreign language!!

Now this is a perfect opportunity for our honourable brother ZK to score cheap political shots through deliberate distortions.

With all due respect, I will rather wait for competent learned brother or sister to raise up and give us a proper review of the Draft in question.
Do you mean the draft carries Zitto recommendations? what Zito did, is to inform us what is in the draft, he has nothing to do with the draft. whether the final binding document will change or not, that is another case, but as how it stands the draft is it is as Zito informed us. So your common sense lead you to believe negotiations of about two years now should come up with this kind of a draft!? Get out of the box so that you can be able to see reality.
 
... Apart from a mere simple fact that he honorably blindsided you on the differences between a Draft version and a Final version of the doc, He went on to skillfully misinterpret the content itself.

My biggest concern is that most folks usually don't like to read anything longer than half a pager. To make matters worse, this particular one is not just an ordinary doc, it is a legal framework written in a foreign language!!

Now this is a perfect opportunity for our honourable brother ZK to score cheap political shots through deliberate distortions.

With all due respect, I will rather wait for competent learned brother or sister to raise up and give us a proper review of the Draft in question.

Where will you get a proper review of the draft? Everything in our government is confidential. Think you are waiting for Prof. Kabudi, keep on waiting and enjoy yourself.
 
Back
Top Bottom