Mhe Werema ulikua unazungumzia Sheria au uliamua tu kujitoa ufahamu kumpinga Tundu Lissu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe Werema ulikua unazungumzia Sheria au uliamua tu kujitoa ufahamu kumpinga Tundu Lissu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mzalendokweli, Jul 5, 2012.

 1. mzalendokweli

  mzalendokweli JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwanasheria yeyote kabla ya kutamka kitu hiki kiko vipi ni lazima atazame msimamo wa kisheria kwa wakati huo anaozungumza isipokua tu kama anawasilisha maoni yake kuhusu hiyo kitu na awe amesema kabisa kua hayo ni maoni yake (Mh Werema anajua hili labla kama aliamua tu kwenda kinyume na CDM asije wapa credits).

  Mhe Werema anajua kua vyanzo vya sheria tunavyotumia kwa mujibu wa Judicature and Application of Laws Act (JALA R.E 2002 formely JALO Cap 453) ni pamoja na SHERIA ZA KIMATAIFA/INTERNATIONAL LAW na MAAMUZI YA MAHAKAMA ZA JUU/CASE LAW (High crt na Crt appeal). Nimetaja vyanzo hivi tu kwakua ndivyo vinavyoweza kutujibia swali hili.

  Kwa mujibu wa ibara ya 1 ya Montevideo convention; ili kue na nchi ni lazima vigezo vinne vitimie ambavyo ni; a) watu; hii inamaana eneo liwe na watu wanaoishi hapo permanently na isiwe eneo linalotembelewa tu, b) eneo,au ardhi isiyomilikiwa na chombo kingine chochote bali hiyo nchi tu, c)serikali na d)uwezo/mamlaka ya kujiamulia mambo yake yote ya ndani na ya nje, kuanzisha au kuvunja mahusiano na nchi zingine bila kuingiliwa na chombo au nchi nyingine yoyote.

  Zanznibar inao watu; wazanzibar, inayo ardhi; visiwa vya unguja na pemba na visiwa vya jirani vinavyozunguka na maji ya bahari yanayozunguka, inayo serikali ya mapinduzi Zanzibar sasa tatitzo liko kwenye hayo mamlaka ya kujiamulia mahusiano ya kimataifa (sovereignity). Kuna wanaosema inayo kama kina Prof Shivji na wanaosema haina ambamo nami nimo na Tundu Lissu bila shaka, hapa ndipo kwenye mjadala.

  Lakini hebu tuachane na hizo sheria za kimataifa mana kila upande una hoja za msingi kabisa kusema wanavyojisikia.
  Tuje kwenye msimamo wa sheria hapa nchini;

  Kwakua hakuna Sheria ilipitishwa na bunge inayotoa tafsiri ya nchi, tafsiri pekee kwa sasa kwamujibu wa sheria Tanzania, na yeyote atakaetaka kusema msimamo wa sheria Tz ni lazima azingatie; ni maamuzi ya mahakama ya rufaa katika case ya SMZ v Machano Khamis Ally na wenzake 17.

  Kwenye hii case mahakama ya rufaa ilitamka kwamba Zanzibar, kama ilivyo kwa Tanganyika, ilipoteza uhuru wake wa kuingia mahusiano ya kimataifa tangu mwaka 1964, pale ilipoingia kwenye muungano kati yake na Tanganyika na mamlaka hayo iliyakabidhi kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hivyo

  Zanznibar sio nchi na mtu hawezi tenda uhaini dhidi ya Zanzibar.
  Jamani huo ndio msimamo wa sheria hapa Tanzania kwasasa.

  Sasa AG sjui kama kwa kauli yake alimaanisha kua yeye kama mwakilishi wa serikali kwa maswala yote ya kisheria bungeni na nje ya bunge, ana msimamo tofauti na ule wa mahakama, na kwamba serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaichukulia Zanzibar kama nchi na si vinginevyo, au alikua akieleza msimamo wake binafsi.

  Kama ni kama aliisemea serikali basi hapa Tanzania tuna vyombo viwili vya kutafsir sheria; Mahakama, na Mwanasheria mkuu wa serikali, vinginevyo, kwa hali yoyote ile, AG kwa nafasi yake, hata kama anamtazamo tofauti, aliwajibika kufuata msimamo wa mahakama ya rufaa kwani Katiba ya JMT inamtaka kufanya hivyo.

  Kila nikitazama bunge nazidi kuona uhalali wa kauli ya Mhe Peter Msigwa (MB) aliposema;
  ".....tunaruhusu akili ndogo itawale akili kubwa, humu tuna mapofessor lakini wanafanya mambo kama mtu aliemaliza darasa la saba....."
  Nasikitika sana watanzania hua hatuoni u
  muhimu wa elimu (isipokua kwa wale mafisadi wa elimu tu) tulizo nazo na tumekua wepesi sana kujidharaulisha mbele ya umma kwa kuweka taaluma zetu pembeni na kusimamia mawazo ya kishabiki ya vyama au mitandao yetu.
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
 3. Ras Cutty

  Ras Cutty Member

  #3
  Jul 5, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  mzalendo kweli nakushukuru sana kwa darasa. nadhani na werema nae atakuwa ameelewa. Ukweli utasimama Daima, wewe waache waendelee na ushabiki.
   
 4. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
Loading...