Mhe. Waziri wa Afya na Waziri wa Nishati, gharama za oxygen hospitalini kwanini ni kubwa hivi na hakuna tamko lolote?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Ninafuatilia maisha ya mama mmoja huko Arusha aliyekaa kwenye oxygeni kwa miezi miwili na familia kutakuwa kulipa zaidi ya milioni thelesini. Katika kipindi ambacho covid ni agenda ya Dunia napata fundisho kwamba ni watu wachache Sana wenye uchumi wakuweza kulipia oxygen.

Naomba wenye utaalam na secta ya afya watueleza gharama za gesi za mahospitali zipoje? Kwa lisaa limoja binadamu anaweza kutumia gharama kiasi gani akiwa anatumia oxygen machine?

Lakini pia kwa mahesabu mepesi Ni kwamba Kama mgonjwa atatumia zaidi ya milioni 30 kwa miezi miwili maana yake ghrama ya Hospitali Ni zaidi ya laki tano kwa siku, hii Ni oxygen gani inayonunuliwa kwa laki tano ndani ya masaa 24?

Je, gesi hii ni sawa na tuliyonayo huko mtwara? Kama ndiyo kwanini isitolewe bure kwa gharama ya serikali?

Wazir wa Afya katika eneo hili tunaomba ujiridhishe na gharama lakini pia utuweke wazi maana sisi sote niwaanga wa covid na tunaweza kuwekewa oxygen. Wananchi wakipata taarifa rasmi ya serikali itatusaidia kujipanga kwa kuchangishana au kuuza Mali tulizonazo kuokoa uhai wa ndugu zetu

Hili Jambo ni zito na linahitaji elimu, lakini pia Kama Hospitali zinatumia hii huduma kama mtaji wa kibiashara Ni muda wakiwaadhibu wote waliotumia covid kuchangia umaskini kwa wananchi.

Poleni wafiwa na Mwenyenzi Mungu awatie nguvu wote mnaopitia kipindi kigumu Cha kuhudumia ndugu zenu waliopo ICU
 
Dr. Mpango alikuwa anatembea na mitungi yake. Hataki ujinga.

Kule Kenya wanamuita "coughing minister", alilazimishwa atoke hospitali autangazie umma kuwa Corona ni kaugonjwa kadogo huku anakohoa balaa!
 
Mgonjwa huyo alikuwa hospitali gani, private au ya serikali?

Alilazwa ICU au wodi za kawaida?

Je, hiyo gharama ya milioni 30 ilikuwa ni bili ya huduma ya oxygen pekee au na huduma zingine zote alizopata mfano: dawa, gharama za kulazwa, vipimo n.k?

Kama Mgonjwa amepona ni jambo jema la kushukuru kwani hakuna gharama ya pesa inayolingana na uhai.

NB: Oxygen inayotolewa hospitali ni tofauti na hiyo ya mtwara ndugu.
 
Back
Top Bottom