Mhe Waziri hujafunga zipu!

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,395
208
Hapa mapaparazzi wameniacha hoi kabisa. Wameshindwa nini kumwambia mheshimiwa kwamba kasahau kufunga zipu yake? Mheshimiwa katoka kwenye loo, karudi haraka kupiga picha na hawa wakurugenzi baada ya kuwafungulia kongamano lao. Kumbe huko alisahau ku-zip suruali yake. Mapaparazzi wala hawamwambii, wao wanachangamkia kupiga picha tu! Hebu oneni hapa jamani, sawa hii?

mramba7654retgdfjk0.png


Waziri B. Mramba akiwa kwenye Press Conference
 

Attachments

  • zipu ya mheshimiwa.bmp
    895.1 KB · Views: 138
hahaha hahahahha may b ndio uzee si wapumzike jamani watu kama hao??
 
Atakumbuka kweli maswala ya wananchi wakati yeye mwenyewe hoi?
 
Sasa hao maaskari kanzu wake wanafanya kazi gani, kwani wameshindwa hata kumshtua mzee wa watu ajisitiri zaidi?.
 
Jamani,
Anatia huruma lakini.. Labda mheshimiwa waziri alikuwa anawaza sana jinsi ndege ya raisi itakavo patikana hata tukila nyasi.. hadi akajisahau kurekebisha!
 
Jamani mambo ya kawaida haya! Kila mtu hapa ameshawahi kupitiwa in his/her life! Sasa tusiifanye kitu cha ajabu.
What I do find interesting is the captions that one can put as a bubble kwamba anawaza nini - Rwabugiri your comment was great!
 
Duh! Hiyo noma... kama kakurupushwa vile! Kama alitoka msalani spidi kuwahi picha basi si ajabu na mikono hakunawa!
 
Hii ni bahati mbaya tu, tuache kumkosea adabu huyu mzee. Kwa kuwa huyu wengine ni kama mzazi wetu na kwa kudumisha integrity ya JF natoa ombi hii picha itolewe. Haijalishi kama kwenye vyombo vingine vya habari wamemtoa hivyo.
 
...hakuna kitu hapo ni mambo ya Adobe tuu na i remember hii picha iliwahi kuwa all over the net some days ago
 
Hii ni bahati mbaya tu, tuache kumkosea adabu huyu mzee. Kwa kuwa huyu wengine ni kama mzazi wetu na kwa kudumisha integrity ya JF natoa ombi hii picha itolewe. Haijalishi kama kwenye vyombo vingine vya habari wamemtoa hivyo.

Green,
Siyo bahati mbaya,
Mh waziri alikuwa bize sana kufanikisha mipango ya ndege ya raisi hata watanzania tukila nyasi!!

Kwa mtaji huo hiyo kazi alo kuwa akiifanya kwa vile imesababisha watanzaia tusote, sioni kwanini ahifadhiwe, tena kama kuna mwenye anuani pepe yake tafadhali tumtumie (lol!)
 
Green,
Siyo bahati mbaya,
Mh waziri alikuwa bize sana kufanikisha mipango ya ndege ya raisi hata watanzania tukila nyasi!!

Kwa mtaji huo hiyo kazi alo kuwa akiifanya kwa vile imesababisha watanzaia tusote, sioni kwanini ahifadhiwe, tena kama kuna mwenye anuani pepe yake tafadhali tumtumie (lol!)

Binafsi ninapinga mambo yote yahusianayo na ufisadi na ukandamizaji. Na nina imani kuwa kwa hoja zenye akili tutaleta ukombozi kwa Taifa letu.

Lakini siungi mkono kuwashambulia hawa viongozi wa serikali kwa kuwadhalilisha. Si jambo la busara kumtoa huyo mzee zipu ikiwa wazi. Najua tuna uweza kuwashinda bila kuwadhalilisha wao wala familia zao. Na pia ni kuwaonyesha kuwa tunaopambana si wahuni bali ni watu wenye fikra sahihi.
 
No hiyo ni aibu kabisa kwani kwa kiongozi kama yeye anamsaidizi wake ambaye pamoja na mambo mengi, anatakiwa kuwa pia mshauri wake wa karibu wa mavazi.
 
That’s hilarious! This shows how careless our politicians are… Leadership and good grooming go together MR.!
 
Press conference wapi & lini?

Mtu kusahau kufunga zipu si jambo la ajabu sana na jambo hili halina uhusiano wowote na uwezo wa mhusika.

Hatahivyo, ukiangalia picha vizuri sehemu za shingo pameunganishwa... definetely sio picha ya Mramba.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom