Hapa mapaparazzi wameniacha hoi kabisa. Wameshindwa nini kumwambia mheshimiwa kwamba kasahau kufunga zipu yake? Mheshimiwa katoka kwenye loo, karudi haraka kupiga picha na hawa wakurugenzi baada ya kuwafungulia kongamano lao. Kumbe huko alisahau ku-zip suruali yake. Mapaparazzi wala hawamwambii, wao wanachangamkia kupiga picha tu! Hebu oneni hapa jamani, sawa hii?
Waziri B. Mramba akiwa kwenye Press Conference
Waziri B. Mramba akiwa kwenye Press Conference