Mhe. Wassira azungumzia Mauaji yanayotokana na jeshi la polisi live on TBC

isasikitisha kuona mzee kama huyu anakuwa kama hajazaliwa tanzania kana kwamba hajui mauaji yaliofanywa na polisi kule mwembe chai. Pia anakituhumu chama cha democrasia na maendeleo ndo kina sababisha mauaji hayo hajayataja ya mwembe chai kwa sababu ameisahau cuf. Kasahau pia chama chochote cha kisiasa kinachokuwa kinakikaribia chama tawala ndo kinakutana na mikasa ya mauaji ya wafuasi wake kwa umakini tatizo sio chadema bali chama chochote kinacho kikaribia chama tawala kwa maana hiyo tatizo ni chama taw.
wasira ni mnafki, yeye ni miongoni mwa waanzilishi wa chadema, yeye na sitta ni wale wale, wanaangalia maslahi yao kwanza, sio watanzania wameegesha tu

watu kama hawa ukiwafuatilia kwa makini utakuta watoto wao wameshanunua uraia wa marekani, sasa wao wapo shambani wanachuma kama balali, tupa kule
 
Huyu Waziri ni loser mkubwa tena wenzake walishastaafu akina Mungai, Mramba na wenzake umri wake na vitu anavyofanya ni tofauti na ndio maana anabaki kuchemsha tu. Kumsikiliza unaweza kuharibu siku bure tune hata katuni
 
Kama hamjajuwa Wasira ndo chanzo cha mauwaji yanayotekelezwa na polisi, ndo mchakataji wa hila zote za kuhujumu wapinzani na watu binafsi wanaopingana na ccm, anajidai kuongea kwa masikitiko kumbe ni mnafiki mwandamizi. Anavoongea anaonesha kuwa polisi hawana makosa isipokuwa cdm tu. Mzee hovyo kabisa huyu
 
Ni dhahiri sasa maandamano/mikutano bila polisi amani inatawala. Tumeona hivyo kwenye mikutano ya CHADEMA ambayo polisi walikaa kando, lakini pia tumeona hivyo kwenye maandamano ya waislam jijini Dar es Salaam.

Mh Wassira anatakiwa aache kudharau watanzania, na atoe maelezo yanayoheshimu intelligence ya kizazi cha sasa. Aeleze umma ni kwanini kila mara polisi wanapokuwepo kwenye mikutano ya CHADEMA fujo zinatokea na hata watu wanapoteza maisha?

Lakini kubwa, ningetaka nimsikie Wassira anaweka maelezo ya RPC wa Iringa kuhusu haya:

1. Majina ya polisi wote waliokuwa wamemzingira marehemu Daudi Mwangosi

2. Vituo vya kazi wanavyotoka askari hao (no 1). Na kama hawatoki Iringa walikuja Iringa lini na kwa sababu zipi, na kwa amri ya nani?
 
Anasema Registraa wa vyama vya siasa ni wa serikali sio wa CCM na maamuzi yake ya kufuta chama hawawezi kuhijiwa mahakamani.

Swali: serikali inatokana na chama gani?
Raisi = Mwenyekiti wa Chanma
Makamu/ Mwawaziri ndio wajumbe wa kamati/halmashauri za chama
Hapo utatenganishaje chama na serikali?

Na serikali si inaendeshwa kwa ilani ya CCM? hivyo vyombo vyote vya serikali bado vinamkono wa chama tawala, mbona kunapokuwa na mafanikio huwa viongozi wanajifanya kusifia kwa kutaja kabisa "SERIKALI YENU YA CCM INAWAPENDA IMEWALETEA..........." lakini yakitokea mabaya unasikia hizo taasisi ni independent na haziingiliwi
 
He! Leo kapata muda wa kuongea tbc? Nilidhani yuko busy ofisini akipokea wazungu katika kudumisha mahusiano.....maana ni waziri wa uhusiano ati.
 
Hajui wakati yeye ndie kinara wa kuagiza polisi waidhibiti cdm? Ukweli utajulikana soon. Hawezi kutoa roho za watu kwa kuilinda ccm
 
Ameruhusu matusi

Yeah kakaririshwa kumtukana ruksa, lakini huwezi kutukana nyara za serikali kule Gombe na Mahale utakuwa wewe ndo umepungukiwa na ufahamu. Aendelee kuimba kama kasuku maana wajuzi tunajua kuwa yeye ni CD au VCD iliyowekwa katika kisemeo. CCM wamerekodi katika CD hiyo
 
Nadhani anajaribu kufuta yale yaliyotoke kwenye Kipima Joto ITV jana...lakini ile picha ya wale polisi nane wakimpiga Mwangosi haiwezi kufutwa na propaganda yeyote ya CCM.
 
Anasema Registraa wa vyama vya siasa ni wa serikali sio wa CCM na maamuzi yake ya kufuta chama hawawezi kuhijiwa mahakamani.

Swali: serikali inatokana na chama gani?
Raisi = Mwenyekiti wa Chanma
Makamu/ Mwawaziri ndio wajumbe wa kamati/halmashauri za chama
Hapo utatenganishaje chama na serikali?

Ndo maana nitaendelea kusema yeye ni kisemeo tu (amerekodiwa) maana akisema serikali ana maana gani? Mbona mara zote wanasema wao chama twawala wamepewa ridhaa na wananchi wa TZ kuunda serikali sasa anasemaje serikali si wao? Wakarekodi upya single hii wamekosea.
 
Kwa nini jimboni kwake hatakiwi ? Mbona haulizwi hili swali ?Kiini cha vurugu ni Nchimbi na Wassira kwa wasi wasi wa madaraka
 
sikuwa home nikaambiwa eti mtoto alikuwa analia sana. Sikujua tatizo ni nini kwa wakati ule, sasa najua.
 
Jaman,wasira anapaswa kuogopwa kama ukimwi,nawataka watz wamuone kama janga la ukimwi nchin!najiuliza hv janga kama hili ndo linamshauri rais wa nchi?ama kwel tanzania ni ya kuombea walahi!
 
Hana jipya huyo anataka kuisafisha tu ccm

nimemwona nakumsikiliza, kimsingi anajaribu kuitetea sheria ya vyama vingi kuwa pingamizi harali la polisi linatakiwa kuheshimiwa mara vyma vinapokataliwa kufanya mikutanoau maandamano.na pia akaenda mbali zaidi kuwa iwapo chama kitatumia nguvu na kusababisha uvunjifu wa amani chama hicho kifutwe.na pia sheria hiyo inasema ,"chama kikishafutwa, hakiruhusiwi kukata rufaa au kupinga kufutwa huko mahakamani.nachelea kusema huyu mzee enzi zile namwona pale falcon wakati aliposhindwa mahakamani na warioba alivyokuwa mpole anasinzia flacon restaurant, sikutegemea leo awe mwanasiasa asiyejali haki na maslahi ya umma.na akumbuke kuwa madaraka na vyeo ni vyakupita, na pia ajue kuwa vizazi vinatakiwa kukumbuka mema yake.Kimsingi kusukuma lawama kuwa mauaji ya watanzania yanayofanywa na polisi cdm ndo chanzo ni kukosa busara, na upotoshwaji wa kimsingi, na pia kuishiwa kisiasa.ni nani asiyejua kuwa huo ndo mpango wa ccm kisiasa kudhoofisha cdm?na sheria kandamizi, nani asiyejua kuwa pia zinatugwa na kuungwa mkono,hivyo kupitishwa na wabunge wa ccm walio wengi kwa kusema," ndiyo", hata kama mbovu.Mfano jana waislam wamevunja sheria mbona hawajapiga mabomuaau kutumia silaha za moto?mbona hawajawakamata viongozi wao kwakuvunja sheria?Pia msajiri wa vyama vya siasa akifuta chama kimakosa, kwanini sheria imruhusu asipingwe hata kama ni kinyume na katiba.wasira ni mgonjwa wa akili kwa huu upuzi hakusitahili kuusema mbele ya vyombo vya habari.watanzania wa sasa si hao wa ghiriba na hadaa
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom