Mhe. Wassira azungumzia Mauaji yanayotokana na jeshi la polisi live on TBC

Isasikitisha kuona mzee kama huyu anakuwa kama hajazaliwa tanzania kana kwamba hajui mauaji yaliofanywa na polisi kule mwembe chai. Pia anakituhumu chama cha democrasia na maendeleo ndo kina sababisha mauaji hayo hajayataja ya mwembe chai kwa sababu ameisahau CUF. Kasahau pia chama chochote cha kisiasa kinachokuwa kinakikaribia chama tawala ndo kinakutana na mikasa ya mauaji ya wafuasi wake kwa umakini tatizo sio chadema bali chama chochote kinacho kikaribia chama tawala kwa maana hiyo tatizo ni chama taw.
 
Wadau mlio karibu na TV zenu Naona Waziri ma mahusiano na uratibu ofisi ya Raisi Mheshimiwa Steven Wasira yuko TBC anazungumzia vifo vya mara kwa mara vinavyotokana na jeshi la polisi kuzuia maandamano na mikutano ya Chadema. Naomba tuangalie tuone mitizamo na misimamo yake.
 
Tusipojiangalia na kujitambua...
Wanasiasa wasipoamua kuwa na ziada ya busara...
Polisi wataendelea kuuwa na wananchi wataendelea kuuawa KISA SIASA...
SIASA ZENYEWE ZA NCHI HII .. SIASA MATAKATAKA!!

LAZIMA TUJITAMBUE.. NA SANDUKU LA KURA PEKEE NDIO MKOMBOZI WA NCHI HII! (kwanini nasema hivyo? sitarajii katiba iwe tayari kabla ya uchaguzi ujao!)
 
huyu babu anazeeka vibaya,anasema eti wale washabiki wa cdm na wandishi wa habari waliomtukana aliposema kuwa cdm itafutwa waendelee tu kumtukana kwa kuwa matusi hayaui.ANA LAANA SANA HUYU MZEE
 
Anasema Registraa wa vyama vya siasa ni wa serikali sio wa CCM na maamuzi yake ya kufuta chama hawawezi kuhijiwa mahakamani.

Swali: serikali inatokana na chama gani?
Raisi = Mwenyekiti wa Chanma
Makamu/ Mwawaziri ndio wajumbe wa kamati/halmashauri za chama
Hapo utatenganishaje chama na serikali?
 
huyu babu anazeeka vibaya,anasema eti wale washabiki wa cdm na wandishi wa habari waliomtukana aliposema kuwa cdm itafutwa waendelee tu kumtukana kwa kuwa matusi hayaui.ANA LAANA SANA HUYU MZEE

kama hajalewa pombe atakua anausingizi
 
ni ujinga fulani ameuongelea yani bado hajakata tamaa na propaganda zake,ajiulizi kwa nini anatukanwa badala yake anaomba watu waendelee kumtukana,kweli ccm hakuna viongozi ni 00
 
M4C na mauaji yanayo endelea kutokea kwenye mikutano ya vyama

Wanatumia TV ya SSM? Haina mashiko!!! Yuko peke yake au na wengine? Sidhani kama atathubutu maana jana Tendwa, msajili wa SSM alikoma ubishi maana Sungusia na yule mwenzake including Masako walimkomesha!!! Mzee alitaka kukimbia kabisa maana vigongo vilikuwa vikali mno!!! Ila tu nilimwonea huruma kwa kuwa njia anayotaka kufuata ya usuluhishi siyo!!! Ni fix tu.
 
Anasema Registraa wa vyama vya siasa ni wa serikali sio wa CCM na maamuzi yake ya kufuta chama hawawezi kuhijiwa mahakamani.

Swali: serikali inatokana na chama gani?
Raisi = Mwenyekiti wa Chanma
Makamu/ Mwawaziri ndio wajumbe wa kamati/halmashauri za chama
Hapo utatenganishaje chama na serikali?

Nilisema Tanzania hakuna demokrasia, ni udikteta tu!! Hii katiba mpya inatakiwa ishughulikie mambo mengi sana kama kweli waliotuwakilisha si wasaliti!!
 
Isasikitisha kuona mzee kama huyu anakuwa kama hajazaliwa tanzania kana kwamba hajui mauaji yaliofanywa na polisi kule mwembe chai. Pia anakituhumu chama cha democrasia na maendeleo ndo kina sababisha mauaji hayo hajayataja ya mwembe chai kwa sababu ameisahau CUF. Kasahau pia chama chochote cha kisiasa kinachokuwa kinakikaribia chama tawala ndo kinakutana na mikasa ya mauaji ya wafuasi wake kwa umakini tatizo sio chadema bali chama chochote kinacho kikaribia chama tawala kwa maana hiyo tatizo ni chama taw.
Tungekuwa na serikali makini angehojiwa kwa mauaji yanayotokea kwani amekuwa akibwabwaja kwa muda mrefu sasa kwamba CHADEMA kitasambaratika; je, haiwezi kuwa kuwaua wanachama kuwa ni mbinu mojawapo ya kuwatisha na kukisambaratisha chama? Kwa vyovyote mtu huyu ana damu ya wana CHADEMA kadhaa waliouwawa kutekwa nyara na kuteswa na vyombo vya dola vilivyochakachuliwa na chama chake.
 
Mh wasira na chama chako cha CCM nendeni kwenye kioo mkamuone ADUI yenu...hata watoto wamewachoka!mmetumia vibaya dhamana tulizowapa,mkitaka tuwapende tuambieni waliosaini MIKATABA mibovu kama ya IPTL,RITES,RADA,RICHIMOND,DOWANS na wezi wa hela za EPA mmewachukulia hatua gani...!msijidanganye kuamini adui yenu ni CHADEMA,adui yenu nisisi watanzania kwa umoja wetu lazima 2015 tuwaonyeshe kuwa rasilimali zetu zinapaswa kuwanufaisha watanzania wote...!
 
Anasema Registraa wa vyama vya siasa ni wa serikali sio wa CCM na maamuzi yake ya kufuta chama hawawezi kuhijiwa mahakamani.

Swali: serikali inatokana na chama gani?
Raisi = Mwenyekiti wa Chanma
Makamu/ Mwawaziri ndio wajumbe wa kamati/halmashauri za chama
Hapo utatenganishaje chama na serikali?
Huyu jamaa anazungumza kama kwamba ametoka usingizini! Ama kweli ufisadi ni sumu yenye ulevi mkali kweli kweli! Kwani huyu msajili ni nani uamuzi wake usihojiwe na yeyote? Hajapigiwa kura na wananchi na alichaguliwa kwa misingi ambayo watanzania hawaijui tena na mtu mmoja ambaye ni Mwenyekiti wa chama tawala! Inawezekana ni uteuzi wa kuhongwa kama wa baadhi ya watendaji wa serikalini.
Ni hatari kuwa na watu kama Tendwa na Wassira kwa maana uamuzi wao wa kinazi unaweza sababisha vita nchini kwani vyama kama vya CHADEMA, CUF na hata CCM yenyewe vilipofika ni wananchi tu ndiyo wanaweza kuvifuta kwa sanduku la kura. Yeyote atakayetokea kuvifuta kinazi anaweza sababisha nchi kuingia vitani.
 
Back
Top Bottom