Mhe. Tundu Lissu, Please Acha Kumsulubu Spika Wetu! Unammaliza Kabisa Hadi Ameshindwa Kazi!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,463
113,529
Wanabodi,

Leo nimepata fursa ya kuliangalia bunge live asubuhi hii kupitia TBC-1,
Spika wa Bunge, Mhe. Anne Makinda ameshindwa kabisa kuliendesha Bunge!, amepwaya sana na ameendesha kikao cha leo bila confidence kabisa na mwisho wa maelezo yake, akamtaja Mhe. Tundu Lissu kama ndiye mbunge anayeongoza kwa kuleta vurugu bungeni, na Lissu aliponyanyuka kuomba muongozo wa Spika, akamvurumishia tena Spika Makombora mazito, na kama angeendela kidogo tuu!, Spika Makinda ange break down kwa machozi!. (Naamini akifika ofisini kwake, atajifungia kidogo na kuimalizia hasira yake the same way wanawake wote wanamalizaga hasira zao!).

Kwa kuzingatia sifa kuu iliyomfanya Mhe. Mama Makinda kuchaguliwa kuwa spika, huku Mhe. Tundu Lissu akiujua fika uwezo wa Madam Spika, kwanini anaendelea kumsulubisha kila apatapo fursa?!. This is not fair!.

Kwa vile Mama Makinda amepewa uspika ajili ya gender issue, kwa uzi huu, namuomba Mhe. Tundu Lissu na wabunge wengine wa Kambi ya Upinzani, wanapokuwa na hoja za msingi, wamuaddress Madam Spika with courtesy of addressing a decent, honorable lady, ili ku restore confidence yake kuliendesha Bunge ambapo kwa sasa, ameshindwa kabisa, kwa hasira, amezuia hoja zote binafsi, hivyo leo Bunge limekutana asubuhi tuu kwa kipindi cha maswali na majibu na kuahirishwa, natumaini kesho na keshokutwa itakuwa vivyo hivyo!, huu ni ufujaji bure wa rasilimali za Taifa!.

Nawauliza wajameni, hivi hiki anachofanya Mhe. Lissu na wabunge wengine wa upinzani, kumsubulu Madam Spika ambaye ni mwanamke bila huruma, ni sawa kweli?!.

Kiafrika, wanawanake ni ni watu wa kubembelezwa na kuonewa huruma!, hivi hawa wabunge wa upinzani ni watu wa aina gani wasio hata na huruma kwa wanawake?!, leo ilibakia kidogo tuu madam spika angelia!, jee hiki wanachofanya ni sawa kweli?!. Ni haki?!

Nawaomben wabunge wa upinzani tumtendee haki Spika wetu aendesha Bunge kwa haki na kujiamini!. Pia tunamuomba Tundu Lissu aache kumuonea Spika mwanamke, asubiri tupate tena Spika mwanaume mwenzake ndio wapambane, Kiafrika sio vizuri kwa mwanaume kupambana na mwanamke, huku ni kumuonea.

Atakapokuja kutokea Spika mwamume kama Spika Sitta ndio Lissu apambane na sio kumyanyasa Mwanamke.

Pasco.


Source: m.m. mwanakijiji wa youtube



Source: ITV TANZANIA ya youtube
 
Last edited by a moderator:
Leo nimemuonea huruma yule mama kweli hasa hoja ya kuwa kuna rufaa za toka mwaka 2011 hadi leo juu ya maamuzi yake hazijashughulikiwa, naona kawa mkali akiwa hana majibu , kutumikishwa ni kazi kubwa kweli kweli
 
Wewe Pasco kwani spika wetu ndio amekuwa wa kwanza duniani kuwa mwanamke ,yeye anaendekeza ukada na wenziwe wanajua hilo na kwa taarifa yake wamesema kuanzia sasa hawatatoka watapambana naye uso kwa uso na ujuavyo Mbunge analindwa na sheria ya kibunge asemacho ndani ya bunge hakiwezi kumpelekea kesi ya jinai abadirike tuu spika afuate kiti kinataka afanye nini period
 
Naomba katiba mpya itamke kwamba spika wa bunge ni lazima achaguliwe na wabunge. Maana nilichokiona hapa ni kwamba muhimili wa bunge haupo kabisa.
 
Pasco na wakuu wengine,mnaweza kutupa hayo makombora ambayo madam spika ameyapata toka kwa Lissu?

Tafadhali wengine tupo mbali na tv,na inaonyesha madam amenyanyaswa sana na akina Lissu.Tusaidieni Lissu amesema maneno gani hasa
 
Last edited by a moderator:
Makinda na team yake ama waamue kuongoza Bunge la wawakilishi wa wananchi wa Tanzania (wa vyama vyote na wale wasio na cham) au aendelee kuongoza kikao cha CCM kwa mgongo wa bunge. Uhuni aliofanya Ndugai haukubaliki kabisa.
 
Naomba katiba mpya itamke kwamba spika wa bunge ni lazima achaguliwe na wabunge. Maana nilichokiona hapa ni kwamba muhimili wa bunge haupo kabisa.

Hata ya sasa inasema hivyo na hata madam spika alichaguliwa kwa kishindo na haohao wabunge akimbwaga Mabere Marando wa chadema kwa mbali.Labda kuna kitu kingine ulikuwa unamaanisha?
 
Back
Top Bottom