Mhe. Spika, umeshaipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuhusu Wabunge 8 wa CUF?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,175
25,446
Ijumaa ya Novemba 10,2017 ulitolewa uamuzi wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa Wabunge 8 wa Chama cha Wananchi (CUF). Uamuzi huo ulitolewa na Jaji Lugano Mwandambo wa Mahakama hiyo kufuatia maombi ya Wabunge hao 8 'waliovuliwa' uanachama kuiomba Mahakama 'kuilinda hali iliyopo' (to maintain status quo) kupisha kuamriwa kwa shauri la msingi.

Shauri la msingi la Wabunge hao 8 wa CUF wa upande wa Maalim Seif S. Hamad, pamoja na mambo mengine, linajikita katika kupinga uamuzi wa linaloitwa Baraza Kuu la CUF chini ya Prof. Ibrahim H. Lipumba kuwavua uanachama wao wa CUF kwa makosa ya kinidhamu. Kufuatia kuvuliwa kwao uanachama, walipoteza sifa za kikatiba kuwa Wabunge na hivyo kuondolewa.

Jambo la kusikitisha ni kuwa Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF wa Wabunge 8 wa CUF ulitolewa wakati tayari Wabunge hao 8 wa Viti Maalum walishavuliwa uanachama wao na hata kuondolewa kwenye Ubunge wao. Tayari hata Wabunge wapya 8 walishateuliwa na kuapishwa.

Nimejitokeza kuuliza tu kama Ofisi ya Spika wa Bunge imeipata nakala ya Uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania niliousema hapo juu na kama kuna hatua zozote zilizochukuliwa. Huu ndio muda wa kuilaumu ile haraka ya kuteua Wabunge wapya 8 na kuwaapisha bila angalau kusubiri Uamuzi wa Maombi madogo ya kumaintain status quo ambayo yalijulikana na wadau wote kuwa yapo.

Kuna jambo la kufanyika ili kuheshimu Uamuzi wa Mahakama. Ni kwakuwa kuzuia kuvuliwa uanachama wa CUF kunamaanisha kuwa Wabunge 8 wa CUF waliopo Mahakamani katika shauri bado ni wanachama wa CUF. Hivyo, kwakuwa waliteuliwa kwa mujibu wa katiba na sheria, bado ni Wabunge halali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hawakupoteza sifa za kuwa wabunge kwakuwa uanachama wa CUF, Mahakama Kuu imesema, bado wanao.
 
pengine hajafahamu maana ya zuio,manake na hizo mahkama zetu nazo zinatoa matamshi yasiyowekwa wazi, zuio hapa lina maana kua "kilichozuiwa kiendelee kuwa na hadhi na hali yake iliyokuwa kabla bila ya kuathirika" kwa kauli ya mahkama wabunge wale 8 bado ni wabunge rasmi mpaka uamuzi tafauti utakapotolewa.

kwa walivyo hawa wanaweza kujifanya kesi tu ndo ilozuiwa
 
Wakubwa hawakosei bali wanasahau,taasisi ya bunge ilipaswa tumia busara subiri maamuzi mahakama.
 
28 Reactions
Reply
Back
Top Bottom