Mhe. Sitta alipua Bomu, kuhusiana na Mishahara wa watumishi wa Serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhe. Sitta alipua Bomu, kuhusiana na Mishahara wa watumishi wa Serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by PascalFlx, Jun 28, 2011.

 1. P

  PascalFlx Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 68
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Sitta ajitosa mjadala wa posho[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta amejitosa kwenye mjadala wa posho ulioanza bungeni hivi karibuni akieleza kuwa suala la kujadili posho za wanasiasa na watendaji wengine linatakiwa kuanzia ngazi ya chini.

  Alisema juzi katika mdahalo ulioandaliwa na Jumuia ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuwa fedha nyingi zimekuwa zikipotea na hata wananchi wanapojaribu kuhoji hakuna maelezo yanayotolewa kwao na baadhi ya watendaji wa serikali zikiwamo za vijiji.

  Sitta, ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM) alisema kuwa malumbano yanayoendelea bungeni kuhusu posho za wabunge na watumishi wengine wa serikali hayana msingi na badala yake wanataaluma ndio wangetakiwa kulipwa vizuri tena kwa fedha nzuri kuliko wanasiasa.

  Alisema kuwa wanataaluma wangepaswa kulipwa zaidi kuliko wanasiasa kutokana na kuwa wamehangaikia taaluma zao kwa miaka mingi kuliko wanasiasa, akieleza kuwa siasa ni kitu cha kujitolea.

  "Sioni sababu ya wabunge kuendelea kujadiliana na kubishana juu ya suala hili la posho.

  “Kinachotakiwa ni kumlipa vizuri mtu aliyehangaikia taaluma yake tena kwa muda mrefu, inafaa apewe mshahara mzuri kulingana na taaluma yake, lakini kwa nchi yetu wataalamu wanalipwa mishahara midogo ambayo haikidhi hata mahitaji yao ya msingi.

  "Matokeo yake, wengi wakishamaliza elimu yao wanakimbilia nje ya nchi kufanya kazi au kugeukia siasa,” alisema Sitta na kuongeza:

  Sitta ambaye alikuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliuambia mdahalo huo wa kujadili masuala ya Jumuia ya Afrika Mashariki ulioandaliwa na Jumuia ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe kuwa hali hiyo haina budi kubadilishwa.

  “Inashangaza kuona fedha nyingi zinapotea kuanzia vijijini na watendaji wake wamekuwa wakijilipa na kufanyia mambo yao bila kushirikisha wananchi na hata kutowasomea mapato na matumizi ya kijiji husika bila ufuatiliaji na wala hakuna jambo lolote linaloweza kufanyika,”alisema.

  Pia, aliwataka wananchi hususani vijana kuwa wawajibikaji zaidi na kuweka uzito katika mambo ya msingi ya taifa na kuhakikisha wanakemea wala rushwa na wale wanaojitajirisha kwa maslahi yao na kuwanyonya watu wa hali ya chini.

  Alisema ndani ya Serikali ya Tanzania kuna tatizo la uwajibikaji na watumishi wengi wamekuwa wakifanya kazi kwa mazoea na kujisahau kuwa wanatakiwa kuwahudumia wananchi katika masuala ya kimaendeleo.

  Kwa upande wao, wanafunzi walishiriki mdahalo huo walihoji ni jinsi gani wananchi wa Tanzania walivyoandaliwa katika kuleta ushindani katika Jumuia ya Afrika Mashariki kwani kila mara wameonekana kuwa nyuma katika ajira kwenye jumuia hiyo.

  “Katika hili, wanasiasa wameonekana kuwa ndio wanaoharibu mfumo mzima kutokana na kuweka siasa zaidi mbele badala ya kutenda kazi ya kushirikisha wananchi hasa wa hali ya chini,”alisema Christian Makala, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Kitivo cha Sheria.

  Alisema wanasiasa wengi wanapokuwa majukwaani hasa wakati wa kuomba kura wanaonekana wazalendo, lakini pindi wanapopata madaraka ikiwamo kuingia bungeni hubadilika na kujisahau na kukubaliana na mambo kwa maslahi ya vyama vyao.

  by Lilian Lucas, Morogoro
   
 2. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  mnafiki tu huyo ka wanasiasa woote ni wanafiki hamna lolote kwa nini alivyokuwa spika wasingejadili hili? Na ktk kipindi chake si ndio marupurupu ya wabunge yaliongezwa? Aaache unafki
   
 3. M

  Mwananzengo Member

  #3
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wanasiasa ndivyo walivyo, wanauma na kupuliza. Si ndiye huyuhuyu wakati akiwa Spika posho ziliongezwa, mbona hakuwatetea wanyonge? Unafiki mtupu!!
   
 4. M

  Mwananzengo Member

  #4
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wanasiasa ndivyo walivyo, wanauma na kupuliza. Si ndiye huyuhuyu wakati akiwa Spika posho ziliongezwa, mbona hakuwatetea wanyonge? Unafiki mtupu!!
   
 5. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mzee Six, kasema vizuri sana!! we have to overhaul the system nzima tena bila kuoneana aibu!! watu wengi wanaishi kiujanja ujanja tu. Lazima tuweke masharti makali, kama mtu hataki kufanya kazi ya umma anataka ujanja ujanja, ajiengue siyo kuleta tabu kwa watu wengine.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,582
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  I have never trusted this guy
   
 7. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu si ndiye aliyejenga ofisi ya spika jimboni kwake mkoa wa Tabora kwa pesa za walipa kodi, hivi watu wanaotumia vibaya raslimali za taifa wana tofauti gani na mafisadi, huyu ni fisadi huyu.

  Na maadhimisho ya posho za wabunge yalipitishwa na bunge lake huyu.
   
 8. i

  ilitalakimura Member

  #8
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hiyo kweli kabisa kaka,huyu mnafiki mkubwa ya CCJ yamemshinda anataka kuhamisha hoja,hafai tena hafai kabisa....
   
 9. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Red Devil, sasa si angekuwa hivi hata wakati ni spika... Huyu anawapalia makaa wenzake kwa kuwa yeye sasa yu kijiweni, wamemtenga si mwenzao. Wana siasa niwatu hatari sana!!! Ndumilakuwili na wanafiki sana....
   
 10. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #10
  Jun 28, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 584
  Trophy Points: 280
  siasa sa imekuwa SIHASA, dah! huyu si ndo aliewaongezea wabunge posho na masurufu kibao enzi zake mpaka wazee wa dsm wakalalamika mbele ya JK?? mbona ivyo tena? aaaagh!!....na hawa wazee wa dsm hiv wana mamlaka gani? maana likitokea jambo JK anakimbilia kwao fasta kwenda kupashana habari.
   
 11. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #11
  Jun 28, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,222
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  No comments!!!!!
   
 12. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Siamini! Akiwa spika, Dr. Slaa alipoanzisha hoja ya kupunguza posho za wabunge alisimamia kudai kuwa ni kidogo sana posho hizo na mahitaji ya wabunge ni mengi. Leo anatuambia nini huyu Sitta?! Unafiki tusikubali
   
 13. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  tusubiri tuone yeye atakwenda wapi maana ccm ndiyo hiyo inachungulia kaburi hakuna cha gamba, wala fisadi atakayeenguliwa ndani ya ya chama. kwa maneno mengine hakuna dawa, wala maombezi yayofaa kukinusuru chama.
   
 14. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Kwani aliyeongeza posho na mishahara ya wabunge si ni yeye, Mnafiki mkiubwa!!
   
 15. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135  TUKO PAMOJA! Si huyu alipopata uspika tu aligombania "maslahi ya Wabunge" na kutowa vigezo kwa Mabunge mengine? Si yeye alietaka Jumba la Fahari kwa Spika/ Wacha tu Wanasiasa wanatufanya mtaji wao, hadi hapo huu uogozi utakapofanywa kama kazi ya wito kama ualimu na udaktari.
   
 16. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2011
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Naomba nirudie niliyowahi kusema.

  Ni enzi ya Sitta ndo mishahara na posho ziliongezeka bila kiwango. Sitta alijitahidi kuwaonyesha akina Kikwete na Lowasa kwamba pamoja na kuninyima u-PM, bado nina chombo kikubwa cha maamuzi juu yenu.

  Ni kama aliunda serikali yake ndani ya Bunge. Na ndo chanzo cha umaarufu wake kwa wabunge.

  Aliwahi kusema kwamba wabunge lazima waishi vizuri. Leo hii eti naye kaona ukweli!
   
 17. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,085
  Likes Received: 7,315
  Trophy Points: 280
  Kwanza huyu ndie aliekingia kifua mpaka marupurupu yakaongezeka, tena kwa kushangaa kabisa wale wanaoyahoji,
  anachoongea sasa ni nini?
   
 18. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,719
  Likes Received: 1,628
  Trophy Points: 280
  huyu anaendana na upepo alikuwa amepotea sasa karudi kundini basi Mzee Six tunakupokea endelea kutetea haki za wanyonge. Hivi Tanzania yetu ni kweli kuna wanyonge? basi kama wapo hawajitambui kuwa ni wanyonge ndio maana wabunge waliowengi wanaendeleza ubabe kwanihawatetewei kila kukicha vitu juu
   
 19. T

  T.K JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sitta aliutetea sana ule mfuko wa mbunge ambao sina hakika kama unakuwa audited, sasa hakuona umuhimu wa kuwapa kipaombele wale anaowatetea leo?.
   
 20. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  tukiacha hayo mapungufu yake,vipi lakini hoja yake ina mashiko??hili nadhani ndiyo muhimu kulijadili
   
Loading...