Mhe. Simbachawene mbunge wa Kibakwe hajui falsafa ya maisha bora kwa kila Mtanzania

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,197
2,000
Akihutubia bunge kwa hisia kali mchana huuakichangia bajeti ya mwaka huu wa fedha mbunge huyo alisema serikali imesambazaumeme vijijini ili kutekeleza sera ya kuwapa maisha bora kila mtanzania kituambacho siyo kweli kwa sababu Mtera aliwaahidi kuwapatia umeme wa grid kabla yabunge hili ambalo limebakiza siku 12 kwisha kitu ambacho hajatekeleza.

Maisha bora kwa kila mtanzani ni sera nzuri sana,tunaomba kumfahamisha Mh. Simbachawene kuwa yeye ndiye mchawi ambaye anafanyasera hii isitekelezeke hapa kwenye jimbo lake la Kibakwe.

Kutekeleza sera hii serikali kuu inakusanya kodi kwakutumia chombo chake ambacho ni TRA , kodi hiyo hupelekwa wizara ya fedhaambapo fedha hizo hugawanywa katika halmashauri zote Tanzania kulingana namiradi yao ya maendeleo walivyojipangia, serikali kuu hurudisha fedha nyingihalmashauri kwa sababu huko ndiko kuna watu.

Halmashauri huongozwa na mwenyekiti na madiwani kwaupande mmoja kama wasimamizi pia kuna mkurugenzi na wakuu wake wa idara kama watekelezaji wa mipango ya maendeleo.

Mh. Simbachawene akielewa wazi kabisa inatakiwa madiwani wawe na kiwango cha elimu chenye haja ili waweze kuwasimamia vizuri watendaji ambao wote wamesoma ali-engenear mpango wa kumweka Nyaulingo kuwa mwenyekiti wa halmashauri wakati Nyaulingo huyo ni mwalimu wa UPE hana elimu yakutosha kumsimamia mkurugenzi na timu yake, ni Simbachawene huyo alifanikisha kumtosa Mh.Dr. Maiseli (marehemu) ili asipate nafasi hiyo wakati ndiye alikuwa mtu mwafaka wa kusimamia sera ya maisha bora kwa kila mtanzania iweze kutekelezwa katika jimbo letu.

Matokeo yake sasa watekelezaji ambao ni Mkurugenzi nawatumishi wengine wanawazidi ujanja madiwani ambao karibu wote hawana elimuwanaiba hela nyingi za miradi na kufanya miradi isikamilike, ndio maanawatumishi hao wana nyumba nzuri za kwao binafi na magali mawili mawili wakati madiwani wanalala guest wawili wawili.

Kwa hali hii maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekanaje?

Mh. Simbachawene mpishe Eng. Mwang`inge aitekeleze vizuri sera hii wewe umeshindwa huna jipya.

Kimwanyula
KIBAKWE

 

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,197
2,000
Huyo Mwikola ajiangalie Msimbachawene asije akamfanya kama alivyomfanya Mwagoha
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom