Mhe. Shy-Rose Bhanji: Amuunga mkono J.Mnyika kuhusu udhaifu wa Rais

kutokuchukuliwa uamuzi mgumu kwa wale waliotufikisha hapa ndio haswa kiini cha haya. kinachotakiwa ni kuwa wepesi kukubali na kupokea maoni ya kambi upinzani. kwa kweli inafurahisha wanavyopanga hoja zao. wako safi inapendeza wanafaa.hivyo basi wabunge wajikite kwenye hoja. kesho utawaona wale ambao ni mashabiki wasio na nguvu ya hoja watakavyo shangilia kama vile wamo harusini. tunahitaji bunge lenye sura ya kitaifa zaidi.
 
Hoja ya kitoto kabisa hii...hii inanikumbusha wakati nipo darasa tatu tunga msamiati kutumia neno dhaifu.
aisee jamaa yenu ni dhaifu mbaya zaidi ndani ya bunge legelege likiongozwa cha chama cha kipuuzi.....2012 Super quote of the year. J.Mnyika.
 
huyu mama majeruhi ya kura za maoni.....

anyway asante kwa kutusaidia, ila hukuliona hili mpaka mnyika kalisemea... au unataka sifa usiyostahili?
 
Niliwahi kunasa ujumbe wa huyu Dada akisema anataka kujiunga Chadema. Naweza pia kuiweka hapa jamvini tuijadili.
 
Kauli ya mh.Mnyika ni msaada mkubwa kwa taifa na ccm yenyewe endapo raisi atakubali kujitafakari upya.Ndani ya ccm si rahisi kumkosoa hadharani na pengine hata kwenye vikao vya ndani mwenyekiti wa chama na ambaye pia ni raisi wa nchi hata kama hawaridhishwi na utendaji wake.Naamini wako wana ccm ambao bila shaka nao watakuwa wamefurahishwa na kauli hii kwani huenda hata wao wanatamani sana kusema yaliyo moyoni ila wanakuwa na hofu ya kufukuzwa.
Hata hivyo neno dhaifu siyo tusi na raisi ni kama binadamu wengine wenye madhaifu mbalimbali.Udhaifu kwa maoni yangu unajionesha ktk mambo kadha yanayohusu maamuzu magumu kwa mfano:-
1.Falsafa ya kujivua gamba
2.kusamehe wezi wa EPA tena mbele ya bunge kwa kuwataka warudishe fedha walizoiba kanakwamba walikopa.
3.Kutokuchukua hatua kwa haraka na kwa wakati kwa wasaidizi wake mpaka baada ya shinikizo kwa mfano mawaziri wanaoboronga kama ilivyokuwa kufuatia taarifa ya CAG hivi karibuni.
4.Utekelezaji wa maazimio mbalimabili ya bunge hasa kuhusu kashifa za richmond,jairo,n.k.
Hiyo ni mifano michache tu ambayo ukiitafakari unaweza kukubaliana na kauli ya Mnyika.
 
Niliwahi kunasa ujumbe wa huyu Dada akisema anataka kujiunga Chadema. Naweza pia kuiweka hapa jamvini tuijadili.

Naomba uweke hapa ndugu yangu ili tujifunze zaidi kumhusu Shy-Rose Bhanji
 
kweli hii hoja imejaa umbea na taarabu mana ata comment ni za kitaharabu na mipasho tu
toa hii
 
Hoja ya kitoto kabisa hii...hii inanikumbusha wakati nipo darasa tatu tunga msamiati kutumia neno dhaifu.

Haya ngoja nitunge yangu. "Baba yangu ameonyesha udhaifu mkubwa kwa kushindwa kututimizia mahitaji yetu muhimu ya maisha".
 
leo wamemtoa nje ya bunge kwa kusema rais ni dhaifu, lakini siku akifa (god forbid), hao utawasikia na masifa yao... Alikuwa mchapa kazi na tumempoteza mtu mwenye ujasili wa kusimamia anachokiamini... Siipendi kabisa hii kitu
hii kauli nayo ni dhaifu,na mkewe pia ni dhaifu?????????
 
Hayawi hayawi huwa!
Mbunge wa Afrika Mashariki, Mhe. Shyrose katika mtandao wa Welcome to Facebook - Log In, Sign Up or Learn More amefunguka na kuandika kama ifatavyo katika hii nukuu:- "Mbona serikali
hawakumuelewa Mnyika
Bungeni. Kwani si kweli
kuwa binadamu wote tuna
udhaifu?!"

Msemo huu unathibitisha kuwa:-

1. Rais ni dhaifu
2. Waziri Mkuu ni dhaifu; jambo Zitto Kabwe alithibitisha zamani.
3. Mawaziri na manaibu wao ni dhaifu
4. Wakurugenzi ni dhaifu
5. Ma-DC ni dhaifu
6.
7.
8.
9.
10.
......wote ni dhaifu na wamechaguliwa au teuliwa na Rais dhaifu ambaye pia ni Mwenyekiti dhaifu wa chama dhaifu.

Ikumbukwe Mbunge huyu (Shy-Rose Bhanji) alichagulia katika upande wa CCM lakini haoni haja yoyote ya kutetea pumba na ndio maana ameamua kusema jambo hili ambalo limesababisha baadhi ya wanachama wenzake wa CCM kujiandaa kuandamana kama njia moja ya kupaka chadema tope pamoja na Mbunge Mhe John Mnyika.

Kwa upande wa chadema kauli kama hizi ni mitaji mikubwa katika siku za usoni hasa katika vuta ni kuvute za Kisiasa.

Source:http://m.facebook.com/shyrose.bhanji.7

Ngoja niwasiliane na MODs kutafuta kanuni ya JF tutakayotumia kukutimua kama alivyotimuliwa Mnyika kwa kosa la kutumia kauli chokonozi, ya kukera na kumdhalilisha Mheshimiwa Dr. Dr. Dr. Dr. Mkuu wa nchi, Serikali yake na chama chake cha nambari wani.
 
Back
Top Bottom