Mhe Rostam ametuambia sasa ni kazi yetu kutekeleza

nguvumali

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,893
Points
1,250

nguvumali

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2009
4,893 1,250
Rostam asemacho hasa kuhusu ccm Ni kitu cha hakika,kwakua amekua mwanachama kiongozi na mtu wakaribu kwa mwenyekiti wa chama hiko, usijaribu kupuuza mawazo yake, anajua kila kitu tangu akiingia kwenye halmashauri kuu hadi kuwa kingmaker wa Kikwete sio mchezo.
CCM WAZEE WA FITINA
 

Power G

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2011
Messages
3,909
Points
1,225

Power G

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2011
3,909 1,225
Rostam hawezi kukwepa dhambi ya uasisi wa siasa uchwara za ccm. Mchango wake katika siasa uchwara zilizoifikisha ccm mahali ilipofikia ni mkubwa sana. Laabda ndiyo maana anazifahamu na ana uhakika kwamba zipo.
 

pangalashaba

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2011
Messages
1,235
Points
2,000

pangalashaba

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2011
1,235 2,000
ukitaka siasa za ubaguzi,udini nenda Chadema hata uzazi wa mpango hawajui babu slaa hana hata haya na kitoto chake kichanga wengine ndo kabisa mabachela.
<br />
<br />
hicho ulichoandika ni pumba tupu!!! nenda kwenye threads za kusifia ccm,huko utakutana wenzio kina mwita25,ms na faidha mbweha.. shetani we,tokaaa!!
 

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Messages
3,149
Points
1,195

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2011
3,149 1,195
HOTUBAYA ROSTAM AZIZ KWA WAZEE WA IGUNGA - TABORA

UTANGULIZI

WAZEE wangu, kwanza kabisa kabla ya kueleza kile ambacho kimenisukumakuzungumza nanyi leo, napenda kuanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi warehema kwa kutuwezesha kufikia siku hii ambayo inatukutanisha waja wake.

Wazee wangu wa Igunga, baada ya kufanya hivyo napenda pia kutumia fursa hiikuwashukuru ninyi nyote mmoja mmoja na katika umoja wenu kwa kuitikia witowangu, kijana wenu, niliyewaomba nije nizungumze nanyi siku hii ya leo.

Nafanya hivyo nikitambua vyema kwamba, kama si nyinyi wazee wangu na wenginewengi ambao hatuko nao hapa leo kwa sababu mbalimbali, ambao mmekuwa na imanikubwa nami nisingeweza kufikia hapa nilipofika sasa.

Wazee wangu, waasisi wa taifa letu walitufundisha kutambua na kuheshimu ukwelikwamba; ‘Uongozi ni Dhamana’ dhana ambayo kila ninapokaa na kutafakari huwainanirejesha nyuma na kukumbuka jinsi nyinyi mlivyokaa katika umoja wenu nakuniteua mimi, miongoni mwa vijana wenu wengi, kuwa mwakilishi wa Jimbo laIgunga tangu mwaka 1994.

Katika kipindi hicho chote cha utumishi wangu, nyinyi wazee wangu mmekuwamhimili muhimu ambao umeniwezesha kutimiza wajibu wangu kwa bidii kubwa,maarifa na nidhamu ya hali ya juu nikitambua namnaambavyo mmekuwa na imani kubwa juu yangu.

Ari na moyo wa imani, ushirikiano na mshikamano ambao wazee wangu mmekuwa naokwangu ndiyo ambao kwa kiwango kikubwa umetuwezesha kufanya kazi kwa pamoja,tukishinda changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikilikabili jimbo letu katikakipindi chote ambacho mmeendelea kuniamini kuwa mbunge wenu kwa miaka 18 sasa.

Wakati nikitambua na kuheshimu ukweli kwamba katika kipindi chote cha ubungewangu mmekuwa na imani kubwa nami na kuniunga mkono kwa dhati, naamini kwambakwa upande wangu pia nimejitahidi kwa kadiri nilivyoweza, kutimiza matarajio yawananchi wa Igunga.

Miongoni mwa mafanikio makubwa tuliyoyafikia kupitia ushirikiano wetu nauongozi wa pamoja ni kwamba, mwaka 1994 Igunga ilikuwa ni wilaya ya mwisho kwamaendeleo mkoani Tabora lakini leo ndiyo ya kwanza, taa za barabarani, bima yaafya kwa kila kaya, zahanati kila kijiji na shule nyingi kuliko idadi ya katazilizomo kwenye wilaya.

Wazee wangu, nayasema haya nikitambua kwamba, kama ilivyo katika maeneombalimbali hapa nchini, mafanikio makubwa tuliyoyapata katika nyanja za elimu,afya, makaazi bora na kilimo katika kipindi chote ambacho mmendelea kuniaminikuwa mbunge wenu kwa miaka 18 sasa.

Wakati nikitambua na kuheshimu ukweli kwamba katika kipindi chote cha ubungewangu mmekuwa na imani kubwa nami na kuniunga mkono kwa dhati, naamini kwambakwa upande wangu pia nimejitahidi kwa kadiri nilivyoweza, kutimiza matarajio yawananchi wa Igunga.

Wazee wangu, nayasema haya nikitambua kwamba, kama ilivyo katika maeneombalimbali hapa nchini, mafanikio makubwa tuliyoyapata katika nyanja za elimu,afya, makaazi bora na kilimo katika kipindi hicho chote hayajaweza kumalizachangamoto zote za maendeleo ambazo zinatukabili.

Wazee wangu, ingawa nimekuwa na kawaida ya kukutana na kuzungumza nanyi marakwa mara, mmoja mmoja na wakati mwingine katika umoja wenu, wito wangu wa leouna makusudi ambayo kwa kiwango kikubwa ni tofauti na yaleambayo tumeyazoea.

Japokuwa ujumbe ninaotaka kuzungumza nanyi wazee wangu, si mgeni sana masikionimwenu, tofauti ya leo na mikutano yetu mingine iliyopita ni uamuzi ambaonimekusudia kuufanya na ambao nitayatangaza muda mfupi ujao.

YATOKANAYO

Wazee wangu, naamini mmekuwa mkifuatilia kwa karibu hali ya siasa nchini nahususani afya ya kisiasa na matukio mengine ndani ya ChamaCha Mapinduzi (CCM) ambacho mimi ni mwanachama wake na Mjumbe wa HalmashauriKuu ya Taifa (NEC) nikiuwakilisha Mkoa wetu wa Tabora.

Naamini kwamba katika kufuatilia kwenu mtakuwa mmebaini kuwapo kwa matukioambayo kwa namna moja au nyingine yamekuwa yakitokea huku yakiligusa jina languna wakati fulani nafasi yangu kama kiongozi wa chama hicho.

Wazee wangu, nayasema hayo kwa sababu mara kwa mara ninapokutana nanyi nikiwakatika ziara zangu jimboni na wakati mwingine mnapowasiliana nami kwa njia mbalimbalimmekuwa mkionesha kuguswa kushitushwa na kutaka kujua kulikoni kuhusu mambohayo yanayotokea.

Mimi, kama mnavyonijua nyote, ni mtu muwazi na mkweli. Siku zote nimekuwamwepesi sana wa kuwaeleza kuhusu kila kinachotokea ili kuwaondoa hofu na wakatihuo huo kuwahakikishia kwamba masuala yasiyo na msingi hususani yale yanayogusasiasa za kitaifa hayawezi kutuondoa katika mstari sahihi wa kuwahudumiawananchi wa Igunga, mkiwamo nyinyi wazee wangu ambao mmeniamini na kunitumakuwawakilisha.

Nyinyi wenyewe ni mashahidi wazuri kwamba tangu matukio yanayogusa jina languyaanze kutokea miezi michache tu baada ya Serikali ya Awamu ya Nne inayoongozwana Rais Jakaya Kikweti kuingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka 2005,tumekuwa tukiyapuuza na tukaendelea kufanya kazi pamoja kwa bidii.

Bado naamini na nitaendelea kuamini kwamba tulifanya uamuzi sahihi wa kuyapuuzamatukio hayo kwani mbali ya kuendelea kutimiza malengo mbalimbali yaliyokuwamokatika Ilani yetu ya Uchaguzi ya CCM, pia mliendelea kuniamini kwa nafasi yanguya kuwa mwakilishi wenu bungeni na hata mkaniruhusu nibebe jukumu jingine kubwala kuwa Mjumbe wa NEC ninayewakilisha mkoa wetu wa kihistoria wa Tabora.

Wazee wangu, nyinyi ndiyo watu mnaolifahamu vyema jimbo letu la Igunga nahakika nyinyi ni sehemu muhimu ya watu wanaojua historia ya kisiasa ya Mkoa waTabora kwa miaka mingi hata kabla ya kuja kwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini.

Hakuna shaka hata kidogo kwamba, Tabora ni kitovu hasa cha uasisi wa siasa zavyama vingi hapa nchini. Ni wazi kwamba huwezi ukazungumzia chimbuko la vyamavya upinzani tunavyoviona hapa nchini leo pasipo kugusa mkoa huu ambao umekuwachimbuko la wanasiasa wenye mizizi hapa na nchini kwa ujumla.

Majina ya wanasiasa wa aina ya wazee wetu, hayati Chifu Said Abdallah Fundikirana Christopher Kassanga Tumbo, Kasela Bantu (Mungu awalaze mahala pema peponi),James Mapalala, Profesa Ibrahim Lipumba na mengi mengine yana mizizi yao katikaMkoa wetu wa Tabora.

Kutokana na ukweli huo basi ni wazi kwamba,nikiwa Mbunge wa Igunga kwa vipindi vinne mfululizo na wakati huo huo nikiwaMjumbe wa NEC kwa vipindi vitatu mfululizo, moja ya kazi ambazo nimezifanya kwauaminifu na kwa bidii kubwa huku nikiungwa mkono na kushirikiana nanyi ni ileya kuhakikisha kwamba mkoa huu pamoja na kuwa kitovu cha upinzani unaendeleakubakia kuwa ngome muhimu ya kisiasa ya CCM.

Si vibaya tukakumbushana kwamba, wakati nachaguliwa kuwa mjumbe wa NEC wa Mkoamwaka 1997, jimbo moja katika mkoa wetu lilikuwa likishikiliwa na upinzani. Leohii Tabora ni mkoa pekee miongoni mwa mikoa iliyotuzunguka ambao haukupotezajimbo hata moja kwenda upinzani katika Uchaguzi Mkuu wa 2010. Mafanikio hayatuliyafikia kwa pamoja kutokana na ushirikiano wenu wazee wangu.

Wazee wangu, Waswahili wanasema usione vyaelea, vimeundwa. Kazi ya kuijenga CCMkatika mazingira yenye mizizi hasa ya upinzani nikiwa mbunge na hususani M-NECkutoka Mkoa wa Tabora haijapata kuwa rahisi na itaendelea kuwa ngumu na ambayomapambano yake ni makali sana.

Wazee wangu, kwa namna ya pekee kabisa napenda kuchukua fursa hii kuwashukurunyinyi wazee wangu wa Igunga na wananchi wenzangu wote wa Mkoa wa Tabora kwakushikamana na kuifanya kazi hiyo kwa bidii, uaminifu na mafanikio makubwa.

Matunda ya kazi hiyo kubwa yanaonekana.
Pamoja na kuwa kitovu cha kihistoriacha siasa za upinzani, Tabora ndiyo mkoa pekee katika eneo hili ambaounaongozwa na wabunge wote kutoka CCM baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana nahata kabla ya hapo.

Kwa sababu hiyo basi, wazee wangu, sote katika umoja wetu ukiacha mafanikiomakubwa tuliyopata katika jimbo na Wilaya yetu ya Igunga, tunayo mambo mengineya msingi ya kujivunia. Kwa moyo wa dhati na kwa unyenyekevu mkubwa napendakuwapongeza kwa namna mlivyojitoa kukipigania na kukitetea chama chetu kwa arina nguvu ya kipekee.

KUJIVUA GAMBA

Wazee wangu, chama chetu chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake, Rais JakayaKikwete kimeamua kwa kauli na nia moja kujitathmini na kufanya mabadilikomakubwa ya kimfumo yenye lengo la kukiwezesha kiendelee kubakia chamakinachoaminiwa na kuungwa mkono na Watanzania walio wengi.

Dhamira ya mwelekeo huo wa kufanya mabadiliko ya ndani ya chama chetuilitangazwa rasmi na Mwenyekiti wetu Rais Kikwete wakati wa kilele chamaadhimisho ya miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM, mjini Dodoma.

Katika hotuba yake hiyo, Rais Kikwete aliyafananisha mabadiliko hayo na tabiaya kawaida na ya asili ya nyoka na wanyama wengine kadhaa ya ‘Kujivua Gamba’.

Wazee wangu hatua ya kwanza ya utekelezaji wa azimio hilona mwelekeo huo sahihi ilifanyika mjini Dodoma wakati wa kikao cha Kamati Kuuya Taifa ya CCM ambacho mimi nilikuwa mjumbe wake.

Wakati wa kikao hicho, wajumbe wote wa Kamati Kuu na wale wa Sekretarieti yachama chetu wa wakati huo kwa kauli moja tulikubaliana kujiuzulu, lengo likiwani kumpa Mwenyekiti wetu fursa nzuri ya kufanya mabadiliko ya uongoziyatakayotoa nafasi ya kupata mwelekeo mpya wa Chama.

Wazee wangu, tulifanya hivyo tukionesha kuunga mkono kwa asilimia 100 kileambacho bado naendelea kuamini kuwa ni mawazo sahihi na yenye mwelekeo thabitiya Mwenyekiti wetu ambayo kwa kiwango kikubwa yalikuwa yakiakisi matokeo yaUchaguzi Mkuu wa urais, ubunge na udiwani wa Oktoba mwaka jana.

Niliseme kwa maneno machache tu hili. Ingawa ni kweli kwamba Uchaguzi Mkuu wamwaka jana umekirudisha madarakani chama chetu kwa kukipa ushindi mkubwa katikauchaguzi wa urais, ubunge na udiwani kwa TanzaniaBara na Zanzibar,kiwango cha ushindi tulichopata kimeonyesha waziwazi dalili za wananchikupunguza imani yao kwetu kuilinganisha na ilivyokuwa mwaka 2005.

Tungekuwa ni chama cha siasa cha ovyo iwapo tungepuuza kupungua kwa kura zarais kutoka zaidi ya asilimia 80 tulizopata mwaka 2005 hadi kufikia aislimia 61mwaka jana kiwango ambacho ni pungufu kwa asilimia 20 ya kura katika kipindicha miaka mitano tu, hasa ikizingatia ukweli kwamba mgombea urais ni mtu yuleyule.

Tungekuwa ni chama cha siasa kilichokosa umakini iwapo tungekaa pasipo kuchukuahatua zozote za kujiimarisha baada ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu kuonesha wazikukua kwa upinzani ambao umeongeza idadi ya wabunge na madiwani katika pandezote mbili za muungano.

Matokeo hayo ya uchaguzi ambayo hapana shaka yamekitikisa chama chetuyalitukumbusha wasia ambao tuliachiwa na Baba wa Taifa aliyesema; ‘Bila ya CCMMadhubuti Nchi Yetu Itayumba’.

Wazee wangu, kwa sababu ya kutambua ukweli kwamba hakuna haki isiyo na wajibukama nilivyosema awali, mimi na wenzangu tuliokuwa katika Kamati Kuu tulionaulazima, haja na umuhimu wa kukubali kwa kauli moja wito wa kututaka tujiuzuluikiwa ni hatua moja ya kujipanga na kukijenga upya chama chetu.

KUJIVUA GAMBA KWAPOTOSHWA

Wazee wangu, kilichotokea baada ya kujiuzulu kwetu kila aliye ndani na nje yachama chetu amekisikia na anakifahamu. Chama kilipata safu mpya ya uongoziiliyotokana na kuundwa kwa Sekretarieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wetu mpya,Mhe. Wilson Mukama, na Kamati Kuu iliyokuwa na sura tofauti na ile ya awali.

Wakati tukitafakari na kuangalia mustakabali mpya wa kisiasa ndani ya chamachetu, ghafla yalianza kutokea mambo ambayo chokochoko zake zilianza kusikikatangu tukiwa ndani ya Kamati Kuu ambayo ilijiuzulu baadaye.

Mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ambachokilichagua wajumbe wapya wa Kamati Kuu na kuidhinisha uundwaji wa Sekretarietimpya, dhana ya kujivua gamba ambayo naamini Mwenyekiti wetu aliianzisha kwa nianjema ilianza kuenezwa ikichukua tafsiri na mwelekeo tofauti na ule wa awali.

Wajumbe wawili wa Sekretarieti, Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), Mhe. JohnChiligati, na Katibu wa Idara ya Itikadi na Uenezi, Mhe. Nape Nnauye,walisikika wakitangaza kwamba Halmashauri Kuu ya Taifa ilikuwa imefikia uamuziwa kuwapa siku tisini wale walioitwa watuhumiwa wanaokabiliwa na tuhuma zaufisadi ndani ya chama kujitoa katika nafasi zao za uongozi vinginevyowatafukuzwa na chama.

Wazee wangu, baada ya kushinikizwa sana na vyombo vya habari wawataje kwamajina wanasiasa waliokuwa wakituhumiwa kwa ufisadi ambao ni wajumbe wa NEC naambao wanapaswa kujiuzulu nyadhifa zao, wajumbe hao wa Sekretarieti walikwendambele zaidi.

Baada ya awali kuwaeleza waandishi wa habari kwamba majina ya watuhumiwa haoyalikuwa yakifahamika kutokana na kuhusishwa katika kashfa tofauti kama zile zaRichmond, EPA na ununuzi wa rada, mwishoniviongozi hao walikaririwa wakiyataja majina ya wanasiasa watatu kuwa ndiyoambao walikuwa wakilengwa na maamuzi hayo.

Wazee wangu, nilishangazwa na kushitushwa na namna porojo na fitina za kisiasazilivyofinyangwa kwa mara nyingine tena baada ya kusikia jina la mbunge wenuambaye ni mimi, likitajwa kuwa miongoni mwa yalematatu ya viongozi waliokuwa wakitakiwa eti kupima wenyewe na kisha kuchukuauamuzi wa kujiuzulu nafasi zao za uongozi ndani ya NEC katika kipindi cha sikutisini.

Niliseme hili mapema. Mshangao na mshituko wangu haukusababishwa na kutajwa kwajina langu, la hasha, bali namna uamuzi halisi waNEC na hususani dhana nzima ya ‘kujivua gamba’ ilivyoweza kupindishwa nawajanja wachache na kisha kuendeshwa kwa maslahi binafsi ya kikundi fulani chawatu.

Pili, nilishangazwa na kushitushwa na hatua ya viongozi wa chama changu ambachonimekitumikia kwa bidii na uaminifu mkubwa kufanya juhudi kubwa hata kukivishakikao kitukufu cha NEC uamuzi ambao msingi wa hoja zake ni vita vya kimakundiya kisiasa yaliyo ndani ya CCM kwa upande mmoja na propaganda za vyama vyasiasa vya upinzani na vyombo vya habari kwa upande mwingine.

Tatu, nilishangazwa na kushitushwa na ujasiri ambao umekuwa ukioneshwa nabaadhi ya viongozi wetu wapya wa Sekretarieti wanaolitaja jina langu nakulihusisha na kile wanachokiita ufisadi ambao hata ukweli wa kimazingira nakihistoria ukiachilia mbali ushahidi wa wazi umeshathibitisha kwamba ni porojoza kisiasa zilizotokana na makovu na matarajio ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005na ule ujao wa 2015.

Wazee wangu, nyinyi ni mashahidi kwamba, mbali ya mimi mwenyewe kujitokezakupitia vyombo vya habari na kueleza wazi kwamba sijapata kujihusisha katikavitendo vyovyote vya ukiukwaji wa maadili ya uongozi au vya rushwa, hakunaushahidi wowote uliotolewa unaonihusisha na kashfa yoyote miongoni mwa zilezilizotajwa.

Wazee wangu, ni wazi kwamba kama chama chenye siasa chenye dhamana yakuwaoongoza Watanzania kutoka katika lindi la ufukara, maradhi, matatizo yamakaazi na mengineyo siku zote tunapaswa kuwa makini katika kuhakikisha kwambachangamoto za kuwaongoza na kuwakomboa wananchi waliotupa dhamana hazitikiswina mawimbi ya matakwa ya nyakati ama ya vyombo vya habari au wapinzani wetu wakisiasa walio nje ya CCM.

Ni kwa sababu ya kulitambua hilo na hasa kuyatambua madhara yanayoweza kukipatachama chetu na nchi yetu iwapo tutaendekeza siasa za kupakana matope pasipo nasababu za msingi, kuchafuana kusikokoma na kulipizana kisasi ndiyo maananimeona nitumie fursa hii kuzungumza nanyi wazee wangu ili kuweka kumbukumbusahihi.

MAAMUZI YANGU

Wazee wangu, nimetafakari sana na kimsingi nimefikia hatua ya kupima yaleambayo yamekuwa yakisemwa na kuandikwa juu yangu na ambayo kwa mtazamo wanguunaoungwa mkono na wanafamilia yangu, marafiki zangu na washirika wangu wakibiashara walio ndani na nje ya nchi, naona umefika wakati muafaka wa kuchukuahatua.

Kwa sababu ya kutambua uzito wa hatua ninazokusudia kuzichukua, nilionahalitakuwa jambo la hekima hata kidogo iwapo ningefanya hivyo pahala penginepopote bali hapa Igunga mbele ya nyie wazee wangu.

Baada ya kukaa na wanafamilia yangu, marafiki na washirika wangu wa kibiasharaniliona halitakuwa jambo la busara hata kidogo kuendelea kuvutana na viongoziwa chama changu na wanachama wenzangu wa CCM katika mambo ambayo yanawezakumalizwa kwa njia muafaka.

Wazee wangu, sina budi niwaeleze kwamba, mbali ya athari za kisiasa nakifamilia, vita vya ovyo vya kisiasa kama hivi tunavyoviendesha na kuviendelezandani ya CCM na ndani ya nchi yetu huwa vina athari kubwa katika ulimwengu wakibiashara. Athari kama hizo za kibiashara huingia ndani zaidi kuliko vichwavya habari vya magazeti vinavyolenga kuchafuana, na athari hizo huwa kubwazaidi kwa mtu kama mimi kwa sababu tofauti na wengine wengi hapa nchini, mimini mfanyabiashara wa kimataifa.

Katika ulimwengu wa kibiashara wa leo, vita hivi ambavyo vinaweza kuonekanakuwa ni vidogo tu vyenye malengo ya kuchafuana kisiasa, vinakuwa na atharikubwa katika uhusiano wa kibiashara kuliko hata wale wasioelewa wanavyowezakukadiria. Ndiyo maana nimeona ni afadhali sasa niwape nafasi wale wanaoendeshasiasa hizi uchwara na zisizo na tija waendelee na siasa zao hizo ambazo kwabahati mbaya kwao, mimi sina muda nazo na siwezi kuwa sehemu yake. Na mimi kwaupande wangu niendelee na maisha yangu.

Kutokana na ukweli huo na sababu zote hizo basi,kwa moyo wa dhati na kwa nia thabiti, hatua ya kwanza niliyoiona kuwa ninapaswakuichukua ilikuwa ni hii ya kuitikia wito unaotokana na msukumo wa ndani yanafsi yangu wa kuamua kukomesha kabisa malumbano na mivutano isiyo na manufaakwangu binafsi, kwa viongozi wa chama changu na chama chenyewe.

Msukumo huo si mwingine bali ni ule wa kuamua kuachia nafasi zangu zote zauongozi ndani ya chama, nikianzia na ile ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifanikiuwakilisha Mkoa wa Tabora na hii ya ubunge wa Igunga ambazo kama si kwabaraka za chama changu nisingelikuwa nazo.

Napenda kuliweka hili sawa sawa. Uamuzi wangu wa kuachia nafasi zangu zote zauongozi nilizopata kwa tiketi ya CCM haukutokana na walahaumaanishi kukubaliana na shinikizo lililopotoshwa kuhusu azma ya utekelezajiwa dhana ya kujivua gamba, la hasha, bali dhamira ya dhati ya kuachana na siasahizi uchwara (gutter politics) na kutumia muda wangu kushughulika na biasharazangu.

Aidha, nimefikia uamuzi huo lengo likiwa ni kuwajengea heshima na imani machonimwa wanachama na wananchi wengine, viongozi wangu ambao naamini baada ya mimikujitoa watapata fursa ya kutafakari upya changamoto nyingine mbadalazinazowakabili ambazo msingi wake ni dhamana kubwa walizo nazo za kukiongozachama chetu na nchi yetu kupitia Serikali yake.

Wakati nachukua uamuzi huu, natambua vyema kwamba, watatokea watu ndani yachama chetu na nje ambao watafanya kila juhudi kupotosha au kupindisha ukwelikuhusu hatima yangu ya kisiasa baada ya kujiweka kando na kujipa mimi mwenyewena chama changu fursa ya kutafakari kwa kinamajaaliwa yangu na ya nchi yangu katika siku zijazo.

Nafanya hivyo nikiwa na imani thabiti kwamba, uamuzi wangu huu, hususani ule wakuachia nafasi yangu ya ubunge, yatakipa fursa nyingine CCM ya kuendeleakuliongoza jimbo letu la Igunga katika kipindi cha miaka minne ijayo kabla yaUchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Kwa upande mwingine, uamuzi wangu huu naona ni fursa kwa viongozi wa Chama changu cha CCM kutafakari na kuamua njiawanayoiona wao ni sahihi kuichukua kwa hatima na mustakabali wa chama chetu naambayo wanaamini itakipa nguvu mpya ya kisiasa dhidi ya vyama vya upinzani.

Sambamba na hilo, ninayo imani thabiti kwamba, uamuzi wangu wa kubakia kuwamwanachama wa kawaida na mtiifu wa CCM utakuwa chachu kwa chama changu na kwaSerikali yake kuwatumikia wananchi kwa Ari Zaidi, Kasi Zaidi na Nguvu Zaidi.

Mwisho kabisa, nikimalizia naomba nitumie fursa hii kutoa heshima za pekee kwaRais Jakaya Kikwete kwa kazi kubwa aliyoifanyia na anayoendelea kuifanyia nchiyetu. Amefanya mengi na makubwa kuiendeleza nchi yetu na watu wake kulikoinavyothaminiwa na kufahamika. Kazi yake kubwa inashindwa kuthaminiwa nakufahamika kutokana na siasa chafu tunazoziendesha Tanzania.Wasia wangu kwa wanasiasa wenzangu, waandishi wa habari na Watanzania wenzangukwa ujumla ni kuwa tunahitaji kuisaidia nchi yetu kwa kufanya siasa zenyemwelekeo wa kujenga ambazo ndiyo hasa zinapaswa kuwa siasa kwa maana halisi yaneno hilo.

Wazee wangu, baada ya maelezo hayo, nawashukuru sana kwa kunisikiliza nakunielewa.

Ahsanteni sana.

Mwisho
 

mashikolomageni

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2010
Messages
1,567
Points
1,195

mashikolomageni

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2010
1,567 1,195
Kazi kwa wanaigunga maana wakiendelea na CCM watapotoshwa tena kwanza huyo Kafumu ndiyo jamii ya Jairo maana wamekuwa wakishirikiana kuiba fedha za wananji wa Tz anapaswa afundishwe na wana Igunga
 

Forum statistics

Threads 1,365,390
Members 521,200
Posts 33,345,364
Top