Mhe. Rais Watanzania tunaitaji kusikia zaidi ya hotuba yako kwa vyombo vya ulinzi na usalama

covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
4,859
10,557
Mhe. rais km mpambanaji namba 1 kwenye taifa letu la tanzania lenye kila aina ya maliasili tulizobarikiwa na mungu. tunahitaji kusikia kitu kutoka kwako tunahitaji kufahamu hapa tulipo tuna fanyaje na huko mbele tunaendaje.

Katika kipindi hiki kigumu mno kwa dunia na sisi tukiwemo janga hili limesha tunyoosha,

Secta nyingi kwa sasa zipo hoi na nyingine zinachechema, tunahitaji kujua na utupe muelekeo na muongozo juu ya...

1. Nchi yetu imeathirika vipi kiuchumi na kiafya uchumi umedororo kwa asilimia ngapi ipi mikakati ya serikali kwa sasa tunafanyaje?

2. Vipi hali yetu ya secta ya afya tunaweza kumudu kuhudumia washukiwa na wagonjwa wa corona kwa kiwango kipi serikali imejipanga vipi. vipi hali ya magonjwa mengine km malaria , hiv na n.k vipi bajeti ya afya itabaki ileile au itaongezwa kwa kiwango gani na itatoka wapi hizo pesa za kuongezea..?

Je vikinga maambukizi barakoa, sanitizer na n.k vinapatikana mitaani kwa wingi na gharama nafuu maana tumeamua kuto kulockdown nchi je serikali inamikakati gani kuhakikisha raia wake wapo salama ktk shughuli zao za kila siku?

3. Mhe. rais corana imesimamisha uchumi wa mamilioni ya watanzania mfano, kwa mujibu wa wizara ya maliasili na utalii secto hii pekee ilitoa ajira za direct laki 6 na zile za indirect zaidi ya milioni 2 sasa kwa sasa secta hii ipo kwenye coma watu wote hao hawapo kwenye ajira tena,

Hiyo ni secta moja bado elimu zaidi ya walimu 89,000 elfu walikuwa wanafundisha private schools sasa wapo likizo zisizo na malipo achilia mbali hilo hapo hatujagusia michezo mbalimbali imesimama ziii, vikundi vya catering services kuanzia wapambaji, wapishi, mc na n.k zipo athari kubwa sana.

Hakika hali si nzuri ila ni serikali pekee inaweza kutufariji maelfu hawa kwa kusema mikakati mliyonayo na msaada wenu juu ya watanzania hawa.

4. Kwa vyovyote vile bajeti yetu 2019- 2020 na ya 2020-2021 zimeshaathirika kwa janga hili serikali ituambie tunafanyaje sasa..? km tutakopa wapi au itakuwaje..

5. Ukweli utatuweka huru km serikali yako mhe. mara nyingi umekuwa ukisema wewe ni mkweli na unapenda watu wakweli naomba taarifa ambazo tumekuwa tukipewa ziwe za kweli.

Mkanganyiko mwingi unajitokeza na kutuacha njia panda. mfano taarifa za watu waliopna mara 100 mara 11 tumuamini nani? sisi km watanzania hatutaki kuhoji uhaminifu wa serikali yk kwa raia ila tunaamini wahusika watajirekebisha ukweli muhimu hata km unaumiza ila ndio ukweli.

Mwisho tanzania ni moja na sisi pia tuwe wamoja na wenye nia ya dhati ktk kupambana na corona ktk kipindi hiki kigumu.

#Chukua taadhari kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya corona.
 
Bila shaka unataka kusikia yafuatayo
1. Serikali italipa 80% ya mshahara kwa waliopoteza ajira
2. Serikali itatoa fedha kusaidia biashara zilizo athirika na corona
3. Serikali itatoa fedha za kujikimu kwa watu waliokuwa wamejiajiri na sasa hawana kazi
...
Kwa kifupi tu ni kwamba HAIWEZEKANI
KILA MMOJA APAMBANE NA HALI YAKE
 
Bila shaka unataka kusikia yafuatayo
1. Serikali italipa 80% ya mshahara kwa waliopoteza ajira
2. Serikali itatoa fedha kusaidia biashara zilizo athirika na corona
3. Serikali itatoa fedha za kujikimu kwa watu waliokuwa wamejiajiri na sasa hawana kazi
...
Kwa kifupi tu ni kwamba HAIWEZEKANI
KILA MMOJA APAMBANE NA HALI YAKE
dah .. hii nchi ya ajabu.
 
Back
Top Bottom