Mhe. Rais wakumbuke pia wakuu wa mikoa wastaafu

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Mhe. Rais ana Mamlaka ya uteuzi katika nafasi mbaimbali kama alivyopewa kwenye Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Rais ninakuomba uwakumbuke Wakuu wa Mikoa Wastaafu katika Wenyeviti na Wakurugenzi wa Mashirika mbalimbali katianchi hii ili pia wapate kusukuma maaisha yao ya kila siku. Wakuu hawa wamefanya kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa katika kuleta maendeleo katika Mikoa mbali mbali katika nchi hii. Orodha yao ni kama ifuatavyo:- 1.Mhe. Anatory Tarimo 2.Mhe Isidori Shirima. 3. Mhe. Mohamed Babu. 4. Mhe.Stephen Mashishanga. 5. Mhe. Kandoro 6. Mhe.Tumainieli Kiwelu na wengineo. Mhe.Rais wakumbuke maisha ni magumu huku mitaani.
 
Unaumwa mkojo? Muda wote huo wametumikia taifa unaona hawajatosheka unataka tena wapewe majukumu ile hali kuna watu wanasaka ajira. !

Kama baba yako ni mmoja kati ya uliowataja ni bora umshauri mkalime matango mbeya.
 
Manani zao, mtu alikuwa analipwa mshahara mzuri huku akijisifu ana elimu nzuri. Na mara kwa mara walikuwa wanahimiza watu wakajiajiri, wao kinawashinda nini? Wajiajiri ili tuone walichokuwa wanatuhimiza.
 
Mhe. Rais ana Mamlaka ya uteuzi katika nafasi mbaimbali kama alivyopewa kwenye Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe Rais ninakuomba uwakumbuke Wakuu wa Mikoa Wastaafu katika Wenyeviti na Wakurugenzi wa Mashirika mbalimbali katianchi hii ili pia wapate kusukuma maaisha yao ya kila siku. Wakuu hawa wamefanya kazi kwa weledi na uaminifu mkubwa katika kuleta maendeleo katika Mikoa mbali mbali katika nchi hii. Orodha yao ni kama ifuatavyo:- 1.Mhe. Anatory Tarimo 2.Mhe Isidori Shirima. 3. Mhe. Mohamed Babu. 4. Mhe.Stephen Mashishanga. 5. Mhe. Kandoro 6. Mhe.Tumainieli Kiwelu na wengineo. Mhe.Rais wakumbuke maisha ni magumu huku mitaani.
Hao ma RC ni wanasiasa au waajiriwa wastaafu?
 
Back
Top Bottom