Mhe. Rais, vitabu vya taasisi ya elimu ni vibovu kweli

Mapigomoto

Member
Jan 21, 2016
19
45
MHE. RAIS VITABU VYA TAASISI YA ELIMU NI VIBOVU KWELI


Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliunda tume ya kuchunguza ubovu wa vitabu vya Taasisi ya Elimu na kwa nini ilitokea hivyo.


Mhe. Rais, vitabu vya Taasisi ya Elimu kama ilivyoelezwa na kujadiliwa bungeni, vitabu hivyo ni vibovu kweli kweli. Tume hiyo kuwatafuta waliohusika ni sawa. Lakini kwa nini walifanya hivyo sio hoja.


Endapo Taasisi ya Elimu itafanya kazi hiyo kwa utaratibu mwingine hautaleta manufaa yoyote kwa taifa letu. Taasisi ya Elimu hadi sasa ina miaka minne tangu ipewe jukumu la kuandika vitabu vya shule lakini hakuna vitabu vilivyokubalika. Kila inapojaribu, hutoa vitabu vibovu ambavyo huwa vinachomwa moto. Miaka minne hiyo yote shuleni bado hatujapata vitabu. Kwa kweli shule ni vitabu. Wanafunzi bora tutawapataje? Taasisi ya Elimu inahangaika na masilahi ya pesa tu na sio vitabu bora. Hawakujua kuwa vitabu vyao ni vibovu na kuvipeleka shuleni mpaka walipoambiwa na wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wabunge. Ni wazi kuwa wataalamu wa Taasisi ya Elimu wana matatizo ya kitaaluma.


Mapendekezo ya kupata vitabu bora ni kama ifuatavyo:

(a) Serikali iunde Kamati ya kuhakiki ubora wa vitabu na machapisho mengine ya kufundishia shuleni iliyohuru. Wanakamati lazima wawe ni walimu ambao ni bora katika masomo husika. Kazi ya kamati hiyo iwe ni kutoa alama ya ubora wa kila kitabu kinachohakikiwa.

(b) Wizara ya Tamisemi iunde kamati ya kuchagua vitabu vya kutumika shuleni kulingana na taarifa ya kamati hapo juu ya kuhakiki ubora wa vitabu.


Hivyo waandishi wa vitabu waruhusiwe kuandika vitabu ila vipite kwenye machujio hayo mawili. Waandishi, Taasisi ya Elimu, PATA na wadau wengine wakitumia mfumo huo, vitabu vitakavyoenda shuleni vitakuwa bora. Hili litakuwa suluhisho la vitabu vibovu shuleni.
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
4,856
2,000
Sijuagi hili zengwe kwnn lilimwacha yule maza salama
Ilitakiwa apite nalo leo kila tukiviona vitabu tunamkumbuka prof.
 

Rutorial k

JF-Expert Member
Jun 8, 2014
905
1,000
kazi yao ni matamko tu...wanjidai wanajua kila kitu kumbe wapi!! pengine hata hao wandishi walikuwa wanashinda njaa....kazi ya elimu inahitaji motivation mnoo..wao wanabana matumizi...wajinga ndio waliwao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom