Mhe. Rais... unaweza kuanzia hapa?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,399
39,550
HabariLeo; Wednesday,November 07, 2007 @00:01

TUNAUNGA mkono agizo lililotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnary, ya kutaka maelezo kutoka kwa wenyeviti wa wilaya na Halmashauri ya Manispaa juu ya upotevu wa fedha unaofikia Sh milioni 360 zilizotolewa na Serikali Kuu kwa ujenzi wa madarasa chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM).

Tunasema hivyo kwa sababu kiwango hicho cha fedha si kidogo, na kama zingetumika ipasavyo zingesaidia kupunguza kwa kiasi fulani tatizo la upungufu wa madarasa.

Kinachosikitisha ni kwamba fedha hizo haziko benki na wala madarasa yaliyosudiwa kujengwa hayapo. Dalili zilizopo zinaonyesha kwamba fedha hizo zimekombwa benki na kutumika kwa malengo tofauti na ya binafsi.

Mnary amenukuliwa akisema uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba kuna baadhi ya watumishi wa halmashauri hizo ambao wanamiliki kampuni hewa, wanazozilipa fedha za walipa kodi kwa kazi ambayo haikufanyika.

Matarajio yetu ni kwamba agizo lake litatekelezwa katika kipindi alichokiweka na sheria itachukua mkondo wake kwa watu binafsi na kampuni ambazo zitabainika kuhusika na mtandao huo wa ujenzi wa madarasa hewa.

Kwetu sisi tukio la upotevu wa fedha za MMEM Bukoba linatonesha donda la matukio mengine kadhaa ya aina hiyo, yaliyotokea siku za nyuma katika sehemu nyingine nchini na kusababisha hasara inayokisiwa kuwa ya mabilioni.
Kama hiyo haitoshi, Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) nao unagubikwa na tuhuma kadhaa kama hizo ambazo mara kadhaa zinawahusisha maofisa wa halmashauri, wakuu wa shule, madiwani na kampuni binafsi.

Wakati wachache hao wakitunisha mifuko na matumbo yao kutokana na wizi wa fedha za umma, kwa upande mwingine wa sarafu waathirika ni taifa zima kutokana na kushindwa kufikia lengo la kuboresha elimu ya vijana wetu ambao ni taifa la kesho.

Sisi tunaamini tunastahili kuungana mikono kupambana dhidi ya ufujaji huu wa rasilimali chache za umma wa Watanzania wengi masikini ambao watoto wao watajikuta wakikosa hata elimu ya msingi kama hatutachukua hatua za haraka. (call about understatement)Bukoba wametuonyesha njia. Tuwaige mfano kwingineko kwa kufichua ubadhirifu wa fedha za MMEM na MMES.
 

Kinachosikitisha ni kwamba fedha hizo haziko benki na wala madarasa yaliyosudiwa kujengwa hayapo. Dalili zilizopo zinaonyesha kwamba fedha hizo zimekombwa benki na kutumika kwa malengo tofauti na ya binafsi.

Mnary amenukuliwa akisema uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba kuna baadhi ya watumishi wa halmashauri hizo ambao wanamiliki kampuni hewa, wanazozilipa fedha za walipa kodi kwa kazi ambayo haikufanyika.


Uchunguzi wa awali umeonyesha kuna ubathirifu tayari, badala ya kuwaita Takukuru na Polisi wawasweke rumande, kesi ifunguliwe na uchunguzi ufanywe; mkuu wa wilaya anatoa amri apewe maelezo. Hayo maelezo yatathibisha nini zaidi kile ambacho tayari ameonyesha anakifahamu (kwa mujibu wa uchunguzi wake wa awali)..!! Hivi haya maigizo yataisha lini...wafanyakazi waibe kwa kiwango gani au uchunguzi gani "wa awali" ufanyike kabla sheria haijachukua mkondo wake?

Mkuu wa wilaya mpaka kwanza apate umaarufu wa kisiasa kabla hajahusisha wasimamizi wa sheria.
 
Yebo Yebo, ndio maana naona kuwa kwa vile ni vigumu Rais kuanza kutikisa huko juu basi aanze angalau huko chini. Vunja Halmashauri, tikisa watu wajue mambo haya hayavumiliki tena. Unajua hizi pesa zinavyotafunwa huwa naona aibu kusikia ati tunaomba wahisani watusaidie kununua mahindi wakati wa njaa.

Basi aanzie hapo....
 
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania kwa Vyama vyenye Uwakilishi Bungeni (TCD), Bw. John Cheyo amemtaka Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, kuelekeza mpambano ya rushwa katika vyama vyote na chaguzi zote zijazo ili kukata mizizi ya tatizo hilo.

"Kwa kweli hotoba yako ya jana ni nzuri sana, mapambano hayo ya rushwa yaende mpaka chaguzi za udiwani na ule Mkuu. CCM ikikubali rushwa iwamalize basi vyama vya upinzani vitachakazwa kabisa," alisema.

Bw. Cheyo alisema siasa si kutukanana bali ni hoja na kwamba hoja hizo zisielekezwe kwa mtu bali kwa chama na sera.

Bw. Cheyo ambaye alitumia muda mrefu kupongeza hotuba ya Kikwete, alisema siasa za kutukanana ni hatari na lazima zipigwe marufuku ili nchi iendelee kuwa na amani na utulivu na kwamba ni jambo jema kwa vyama vyote kuwekeza katika amani .

Alisema kwa kuwa TCD ndio eneo pekee ambapo vyama vinaweza kukaa pamoja na kujadili mapungufu mbalimbali, ni vizuri Serikali kusaidia zaidi badala ya kazi hiyo kuachiwa wafadhili pekee.

Alisema kwa kuwa Rais Kikwete amekubali kufanya marekebisho aliyoyaita ya kutosha na yanayoeleweka ni bora mikataba ya madini ikawa wazi kwa kila mwananchi na kuondoa usiri usiokuwa na lazima.

Alisema Rais Kikwete kuwawekea hadharani wana CCM kuhusu rushwa ni dalili njema ya kutaka kukiimarisha chama hicho na kwamba anafurahishwa na hilo.

Hotuba hiyo ya Bw. Cheyo iliyotafsiriwa kuwa ni ukomavu wa kisiasa na wana CCM wengi ilijibiwa papo hapo na Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete na kusema "hiyo ni changamoto kwa CCM kuwa TCD inasaidiwa zaidi na wafadhili na sio sisi, tumekusikia
Bwana Cheyo."
 
Mimi kwa maoni yangu ni bora aanze kusafisha nyumba yake kwanza kabla ya kupigia kelele nyumba za wenzake. CCM ndio chama kikongwe kuliko vyama vingine vyote na ndio chama kilicho madarakani. Sio siri kwamba CCM si safi na hili lilianza kusemwa na Baba wa Taifa miaka mingi iliyopita. Hivyo kukemea rushwa katika vyama vya upinzani kutakuwa na nguvu zaidi kama CCM itakuwa safi vinginevyo itaonekana ni juhudi za kutotaka kuwajibika kuisafisha CCM.
 
Bw. Cheyo alisema siasa si kutukanana bali ni hoja na kwamba hoja hizo zisielekezwe kwa mtu bali kwa chama na sera. Bw. Cheyo ambaye alitumia muda mrefu kupongeza hotuba ya Kikwete, alisema siasa za kutukanana ni hatari na lazima zipigwe marufuku ili nchi iendelee kuwa na amani na utulivu na kwamba ni jambo jema kwa vyama vyote kuwekeza katika amani .

Alisema Rais Kikwete kuwawekea hadharani wana CCM kuhusu rushwa ni dalili njema ya kutaka kukiimarisha chama hicho na kwamba anafurahishwa na hilo.
 
Nani kamtukana nani!? Slaa, Mrema au Zitto? Na tusi lipi lililotumika lilikuwa la nguoni au la hewani? Huyu Cheyo si bure labda naye anataka kurudi CCM ili akapewe ulaji...:)
 
Aiiii na nyie kila kitu lazima muingize siasa wakati mwingine haina maana. Sasa kwenye issue kama hii ya wizi wa pesa za madarasa hivyo vyama ni vya nini? Hapa kupambana na ruswa ni kute rushwa ndogo na rushwa kubwa. Mnafikiria ni watoto wangapi watakosa elimu kwa sababu ya wizi wa pesa za madarasa? Takuru njia ni nyeupe kwa issue kama hiyo hapo juu. Kama pesa haziko bank na madarasa hayapo maelezo yanatakiwa ya nini? SIo hiyo wilaya tuu bali naamini kunawilaya libao zinamatatizo kama hayo. Serikali iwawajibishe maramoja wahusika bila kuangalia ni nani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom